HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Monday, 16 July 2018

Serikali Yapongezwa Kwa Kuwainua Wanawake Sekta ya Madini

 Msanifu majengo wa Kampuni ya InterConsult Ltd Bw. Beno Matata akieleza mikakati ya kampuni hiyo katika kuhakikisha kuwa inasimamia mradi  wa ujenzi wa Kituo Maalum kitakachotumika kuwajengea uwezo wanawake wanaojishughulisha na uchimbaji wa madini, Kituo hicho kitawanufaisha wachimbaji hao ikiwa ni sehemu ya Juhudi za Serikali kupitia Wizara ya Madini kuinua wachimba hao.
 Msanifu majengo wa Kampuni ya InterConsult Ltd Bw. Beno Matata akimkabidhi Meneja wa SUMA JKT Kanda ya Kati Mhandisi David Palangyo ramani ya jengo la ghorofa tatu linalojengwa na SUMA JKT katika chuo cha madini Dodoma ikiwa ni sehemu ya mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Endelevu wa Rasilimali Madini (Sustainable Management of Mineral Resources Project- SMMRP), mradi huo unatekelezwa na Wizara ya Madini ikiwa ni sehemu ya mikakati ya kuimarisha sekta hiyo na kukuza uchumi.
 Msanifu majengo wa Kampuni ya InterConsult Ltd Bw. Beno Matata akionesha mipaka ya eneo kitakapojengwa kituo maalum kitakachotumika kuwajengea uwezo wanawake wanaojuhusisha na uchimbaji wa madini kupitia chama cha wachimbaji wanawake (Women Mining Association),jengo hilo lenye gorofa tatu linajengwa katika chuo cha madini Dodoma.
 Msanifu majengo wa Kampuni ya InterConsult Ltd Bw. Beno Matata akiongoza timu ya wataalamu wa Wizara ya Madini na Mkandarasi ambaye ni SUMA JKT kukagua eneo litakapojengwa jengo la kisasa lenye gorofa 3 linalojengwa chuo cha madini Dodoma likilenga  kuwajengea uwezo wanawake wanaojuhusisha na uchimbaji wa madini kupitia chama cha wachimbaji wanawake (Women Mining Association).
  Msanifu majengo wa Kampuni ya InterConsult Ltd Bw. Beno Matata akimkabidhi Meneja wa SUMA JKT Kanda ya Kati Mhandisi David  Palangyo ramani ya jengo la kisasa la gorofa 3 linalojengwa chuo cha madini Dodoma likilenga  kuwajengea uwezo wanawake wanaojuhusisha na uchimbaji wa madini kupitia chama cha wachimbaji wanawake (Women Mining Association).
Timu ya Wataalamu kutoka Wizara ya Madini, Kampuni ya InterConsult Ltd, SUMA JKT na Chuo cha Madini wakitoka eneo litakapojengwa jengo la gorofa 3 katika chuo cha madini mjini Dodoma litakalotumika kuwajengea uwezo wanawake wanaoshiriki katika uchimbaji wa madini.
(Picha zote na Frank  Mvungi- MAELEZO)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad