HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, July 16, 2018

ZFDA YATEKETEZA TANI 95 ZA CHAKULA NA TANI MOJA YA DAWA ZA BINADAMU ZILIZOMALIZA MUDA WA MATUMIZI

Na Ramadhani Ali, Maelezo Zanzibar
Mamlaka ya Chakula na Dawa Zanzibar (ZFDA) imejidhatiti kuhakikisha kuwa bidhaa zinazoingizwa nchini zinawafikia wananchi zikiwa salama kwa matumizi kwa lengo la kulinda afya zao.

Mkurugenzi wa Idara ya Udhibiti wa Usalama wa chakula wa ZFDA Dkt. Khamis Ali Omar alieleza hayo katika jaa la Kibele wakati wa kazi ya kuangamiza tani 95 za bidhaa za mchele, sembe na Unga wa ngano pamoja na tani moja ya dawa za binadamu.

Alisema bidhaa za chakula zilizoangamizwa za mfanyabiashara Mohamed Mattar ziliharibika baada ya kuhifadhiwa kwa muda mrefu katika maghala yasiyorasmi na yaliyokosa sifa za kutumika kwa kazi hiyo.

Dkt. Khamis alieleza kuwa kutokana na maghala hayo kukosa viwango vinavyokubalika na kutosajiliwa na ZFDA, mfanyabiashara Mattar alikuwa  akiweka bidhaa zake kwa siri wakati wa usiku.

Akitaja viwango vya bidhaa zilizoangamizwa, Mkurugenzi wa Idara ya Udhibiti na uhifadhi wa chakula wa ZFDA alisema mchele ulikua tani 52, unga wa ngano tani 37 na sembe ilikuwa tani sita.

Alisema sehemu ya bidhaa hizo zilikuwa zikitolewa kama sadaka katika mwezi wa Ramadhani kama mbinu ya mfanyabiashara huyo kujaribu kukwepa gharama za kuangamiziwa bidhaa zake.

Mkurugenzi Idara ya Udhibiti na Usalama wa Chakula aliwataka wafanyabiashara wanapotaka kutoa sada ya chakula kuishirikisha ZFDA ili kuhakikisha ubora na usalama wa bidhaa itakayotolewa.

Mfamasia wa ZFDA Nassir Buheti alisema kiwango kikubwa cha dawa zilizomaliza muda wa matumizi zilitoka Taasisi za kiraia (NGO) kwa ajili ya kuangamizwa  na kiwango kidogo kilipatikana katika maduka ya kuuzia dawa.

Buheti alitoa wito kwa maafisa wa NGO wanaopata msaada wa dawa kutoka nje kuwa waangalifu katika kuzitumia na inapokaribia miezi mitatu kabla ya kumaliza muda wa matumizi na wakihisi haziwezi kumalizika wazipeleka ZFDA ili wazisambaza katika vituo vya afya vya Serikali ambako mahitaji ya dawa ni makubwa.
  Fundi wa mageti akikata geti la Ghala lililokua likihifadhiwa bidhaa za Mchele, Unga wa ngano na sembe uliomaliza muda na haufai kwa matimizi ya binadamu katika mtaa wa Migombani Mjini Zanzibar.
 Sshemu ya bidhaa ya Mchele na Unga wa Ngano na Sembe zikiteremshwa katika magari kwa ajili ya Kuangamizwa katika Jaa la Kibele Wilaya ya Kati Unguja.
 Gari ya Kijiko likiuharibu kwa kuufukia Unga wa Ngano uliokua haufai kwa matumizi ya Binadamu katika Jaa la Kibele Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
 Dawa za binadamu za aina mbali mbali za kuondosha maumivu na Virutubisho zilizo angamizwa katika  Jaa la Kibele Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja
 Gari la Kijiko likiangamiza Dawa za kuondosha maumivu na Virutubisho zilizoangamizwa katika  Jaa la Kibele Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
Mkurungezi Idara ya Udhibiti na Usalama wa Vyakula wa ZFDA Dkt. Khamis Ali Omar akizungamza na Waandishi wa habari wakati wa zoezi la kuangamizaji Bidhaa zisizofa kwa Matumizi ya Binadamu lililofanyika katika  Jaa la Kibele Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
Picha na Abdalla Omar Maelezo  -  Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad