HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, 28 July 2018

SERIKALI YAONDOA RIBA MIKOPO YA WANAWAKE, VIJANA NA WALEMAVU

 Mbunge wa Chato (CCM) na Waziri wa Madini Dkt. Medard Kalemani akimshukuru Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto  Dkt. Faustine Ndugulile kwa ziara yake alioyoifanya katika kata za wilaya ya Chato mkoa wa Geita iliyolenga kuangalia utoaji wa huduma za afya na maendeleo ya jamii wakati wa kuhitimisha ziara ya Naibu Waziri huyo ya siku mbili mkoani humo.
 Mwekahazina wa kikundi cha Jikomboe kilichopo wilayani Chato Mkoani Geita akiwasilisha risala yao kwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wkati wa kuhitimishwa kwa  ziara yake alioyoifanya katika kata za wilaya ya Chato mkoa wa Geita iliyolenga kuangalia utoaji wa huduma za afya na maendeleo ya jamii wakati wa kuhitimisha ziara ya Naibu Waziri huyo ya siku mbili mkoani humo.
 Baadhi ya wananawake wajasiriamali wakimsikiliza Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wakati akihitimisha ziara  yake alioyoifanya katika kata za wilaya ya Chato mkoa wa Geita iliyolenga kuangalia utoaji wa huduma za afya na maendeleo ya jamii wakati wa kuhitimisha ziara ya siku mbili ya Naibu Waziri huyo mkoani humo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto  Dkt. Faustine Ndugulile akiangalia malighafi inayotumika kutengeneza batiki wakati alipokitembelea kikundi cha wanawake wajasiriamali cha  Jikomboe kilichopo Wilaya ya Chato wakati akihitimishaziara  yake alioyoifanya katika kata za wilaya ya Chato mkoa wa Geita iliyolenga kuangalia utoaji wa huduma za afya na maendeleo ya jamii wakati wa kuhitimisha ziara ya siku mbiliua  Naibu Waziri huyo  mkoani humo.
Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW

 Na WAMJW CHATO - GEITA
Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imetangaza rasmi kuwa hakutakuwa na riba katika mikopo itakayotolewa kwa wanawake, vijana na walemavu katika ngazi ya Halmashauri.

Kauli hiyo imetolewa wilayani Chato na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile alipokitembelea kikundi cha wanawake wajasiriamali cha Jikomboe.

Dkt. Ndugulile ameongeza kuwa Serikali imedhamiria kuwasaidia Wanawake, vijana na walemavu kujikwamua kiuchumi hivyo imeona ni bora mikopo itolewe bila riba ili kuwapa fursa wanawake, vijana na walemavu kwa ajili ya kuanzisha miradi ya wingi ya kujikwamua kiuchumi.

Ameongeza kuwa suala la riba limekuwa kikwazo kwa makundi mengi kuweza kukopa na kurejesha mikopo kwa wakati.

"Niseme tu tumeliangalia suala hili kwa karibu ili tuwawezeshe wananchi hasa wanawake, vijana na walemavu kujikwamua kiuchumi" alisisitiza Dkt. Ndugulile.

Akisoma risala kwa niaba ya kikundi cha Jikomboe Mweka hazina wa kikundi hicho Bi. Deborah Jeremia  amesema kuwa walifanikiwa kupata mikopo wa Shilingi Millioni moja na kurejesha mikopo yote kwa wakati.

Kwa upande wake Mbunge wa Chato(CCM) na Waziri wa Nishati  Dkt. Medard Kalemani amesema kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Chato inashirikiana na Ofisi ya Mbunge katika kuwawezesha wanawake, vijana na walemavu kwa kuwapatia mafunzo ya ujasiriamali kutoka Baraza la Uwezeshaji wananchi kiuchumi.

"Tumewapatia mafunzo wanawake wajasiriamali kupitia Baraza la Uwezeshaji wananchi kiuchumi" alisisitiza Dkt.Kalemani. 

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad