HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Saturday, 28 July 2018

WANACHUO KUTOKA SOKOINE NA MUHIMBILI WATEMBELEA MAMLAKA YA MAABARA YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI

 Mtumishi wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali,  Bw. Boniface Majinyali (kulia) akiwaonyesha kwa vitendo namna uchunguzi wa sumu unavyofanyika kwenye maabara baada ya wanachuo hao kutembelea maabara hiyo.
 Baadhi ya viongozi wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, wahadhiri na wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine (SUA) na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS)mara baada ya kumaliza kutembelea maabara.
 Picha ya pamoja ya baadhi ya viongozi wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, wahadhiri na wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine (SUA) na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS)waliotembelea maabara kwa ajili ya kujifunza namna chunguzi zinavyofanyika.
 Wanachuo kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine na Muhimbili wakifuatilia maelezo ya utangulizi kuhusu majukumu ya Mamlaka yaliyowasilishwa na Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Biashara, Bw. George Kasinga (hayupo pichani). 
 Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Biashara, Bw. George Kasinga (aliyesimama kushoto) akimtambulisha, Profesa Paulo Gwakisa, kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine (wa pili kulia) kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) walipotembelea ofisi za Mamlaka.
Mtumishi wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Bw. Alois Ngonyani (kulia) akiwafahamisha wanachuo kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine (Morogoro) na Muhimbili (Dar es Salaam) kuhusu uchunguzi unaofanywa kwenye maabara ya mazingira mara baada ya kutembelea maabara hiyo. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad