HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, 28 July 2018

PROF MBARAWA AKAGUA MRADI WA MAJI WA MTO RUFIJI

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
WAZIRI wa Maji na Umwagiliaji Prof Makame Mbarawa ametembelea mradi mkubwa maji wa bwawa katika Mto Rufiji utakaoweza kusaidia matumizi ya maji kwenye kambi ya ujenzi wa mradi wa umeme katika maporomoko ya maji ya mto Rufiji (Stiegler's Gorge)

Mradi huo unaotekelezwa Wizara ya Maji na Umwagiliaji kupitia  Mamlaka ya Maji safi na Maji taka (DAWASA) na umeweza kugharimu kiasi cha Milioni 604.9 ukiwa ni muendelezo wa mradi mkubwa wa maji unaoendelea Kisarawe.

Akizungumza baada ya kutembelea maporomoko ya Mto Rufiji Prof Mbarawa amesema kuwa mradi huo wa maji utakuwa na uwezo wa kuzalisha maji lita 209,000( laki mbili na elfu tisa) kwa ajili ya matumizi ya kambi ya ujenzi wa mradi wa umeme katika maporomoko ya maji ya mto Rufiji (Stiegler's Gorge).

Amesema, mradi huo wa maji utawasaidia wakandarasi kusa na miundo mbinu wezeshi itakayowapatia maji muda wote wa matumizi yao ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanusi mkubwa.

"Miundo mbinu wezeshi itawapa fursa wakandarasi wafabye kazi kwa ufanisi mkubwa sana kwa  sababu maji yatakuwa yanapatikana muda wote na kila siku na hili litasaidia katika kuhakikisha mradi wetu wa ujenzi wa bwawa la umeme kumalizika kwa muda ulipangwa,"amesema Prof Mbarawa.

Prof Mbarawa ameeleza kuwa, mradi huo wa maji utakuwa na matanki makubwa mawili, mabomba ya kusambazia maji  na unatarajia kuchukua urefu wa Km 1463 kutoka mahali maji yanapopatikana.

Kwa upande wa Kaimu Mkurugenzi wa DAWASA Dr Suphian Masasi amesema kuwa mradi huu utakuwa na manufaa kwa taifa kiujumla kwakuwa huduma ya maji itapatikana kwa uhakika kipindi wakandarasi wanaendelea na shughuli zao.

Dr Masasi meeleza kuwa kabla ya kuanza kusambaza maji hayo waliweza kufanyia marekebisho baadhi ya miundi mbinu iliyokuwa chakavu ikiwemo ukarabati wa eneo la chanzo pamoja na ufungaji wa pampu moja mpya itakayokuwa na uwezo wa kuchota maji mtoni kiasi cha lita 2.41 kwa sekunde.

Katika ukarabati huo pia uliweza kuhusisha bomba la kusafirishia maji (GS pipe) kipenyo cha nchi 3, ujenzi wa bomba jipya la plastic(HDPE) la kusafirishia majighafi kutoka mto Rufiji hafi kwenye tanki na kituo cha kusafisha maji, ukarabati wa kituo cha kusafisha maji, ujenzi wa kituo cha kusukuma maji, ujenzi wa bomba la kusafirishia maji, ukarabati wa matanki mawili ya zamani ya lita 12,500 na 22,500 na ufungaji wa dira za maji , air valve 4 na gate valve 4.

Dr Suphian amesema mradi huo unatarajiwa kumalizika Agosti 15 mwaka huu baada ya kukamilika kwa asilimia 85  mpaka sasa.
 Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof Makame Mbarawa akifunga bomba la kisasa la kusafirishia maji  kwenye eneo la kambi lenye jumla ya Km 1463,kipenyo cha nchi 1.5 na nchi 3 kwenye eneo la ujenzi wa mradi wa umeme katika maporomoko ya maji ya mto Rufiji (Stiegler's Gorge).
 Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof Makame Mbarawa akifunikia bomba la kusafirishia majighafi kwenye eneo la kambi lenye jumla ya Km 1463,kipenyo cha nchi 1.5 na nchi 3 kwenye eneo la ujenzi wa mradi wa umeme katika maporomoko ya maji ya mto Rufiji (Stiegler's Gorge).
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof Makame Mbarawa akiwa pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Dr Suphian Masasi wakiwa wanakagua  bwawa la kusafishia maji yanayotoka katika Mto Rufiji kwa ajili ya matumizi ya wakandarasi waujenzi wa mradi wa umeme katika maporomoko ya maji ya mto Rufiji (Stiegler's Gorge).
 Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof Makamd Mbarawa akirusha maji katika moja ya bwawa la kusafishia maji yanayotoka katika Mto Rufiji kwa ajili ya matumizi ya wakandarasi waujenzi wa mradi wa umeme katika maporomoko ya maji ya mto Rufiji (Stiegler's Gorge).
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof Makame Mbarawa akiwa anakagua mradi mkubwa wa maji katika Bwawa la Mto Rufiji utakaoweza kuwasaidia wakandarasi kupata maji ya uhakika kwenye ujenzi wa mradi wa umeme katika maporomoko ya maji ya mto Rufiji (Stiegler's Gorge) akiambatana na Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Maji Taka (DAWASA) Dr Suphian Masasi.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad