HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, July 12, 2018

MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA ATOA MAFUNZO KWA WASIMAMIZI WA UCHAGUZI

Na Monica Laurent, Dar es salaam.
Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa imetoa mafunzo maalumu kwa watumishi wa ofisi yake ili kuwajegea uwezo wa kufanya uangalizi wa uchaguzi mdogo unaotarajiwa kufanyika tarehe 12 Agosti 2018 katika jimbo la Buyungu na kata 79.
Mafunzo hayo yamefanyika leo Julai 11, 2018 katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ambapo mada mbalimbali zimewasilishwa zikiwemo mada juu ya Elimu ya Maadili ya Vyama vya Siasa, Haki na wajibu wa Vyama vya Siasa, wajibu wa Msajili wa Vyama vya Siasa, matendo yanayokatazwa na Sheria ya Gharama za Uchaguzi na Sheria ya Vyama vya Siasa, Umuhimu wa kujaza fomu za gharama za Uchaguzi. 
Akizungumza wakati wa kufungua mafunzo hayo, Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Mhe. Jaji Francis S.K. Mutungi amewawataka watumishi hao kufanya kazi kwa ueledi na kwa kufuata sheria za nchi.
“ kila mmoja wetu atambue kuwa ofisi yetu imepewa dhamana kubwa ya kusimamia Sheria ya Gharama za Uchaguzi ya mwaka 2010 na Sheria ya Vyama vya Siasa ya mwaka 1992 ili kudumisha demokrasia ya vyama vingi nchini, ni wajibu wetu kufanya kazi kwa ueledi na kwa  mujibu wa sheria” amesisitiza Jaji Mutungi
Naye Bi. Piencia C. Kiure mmoja wa wakufunzi katika mafunzo hayo ambaye ni Msajili Msaidizi anayeshughulika na masuala ya Gharama za Uchaguzi na Elimu kwa Umma amesisitiza umuhimu wa wagombea na vyama vya Siasa kurejesha fomu za Gharama za uchaguzi zinazobainisha mapato na maksio ya kiwango cha matumizi wakati wa uteuzi,kampeni na uchaguzi ndani ya muda  uliotengwa kisheria ili kuepuka ukiukwaji wa sheria ya Gharama za Uchaguzi.
Watumishi pia wamesisitizwa kuhakikisha wanavikumbusha vyama vya siasa na wagombeakunadi sera za vyama kwa kusimamia maadili ya vyama vya siasa ili kuendelea kudumisha amani ya nchi.
Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ni taasisi yenye  wajibu wa kisheria wa kufanya uangalizi wa mwenendo wa chaguzi zinazofanyika kwa ajili ya  kuhakikisha kuwa wagombea na vyama vya siasa vinatekeleza matakwa ya sheria kwa kuepuka vitendo ambavyo vimekatazwa na sheria hizi ili kuimarisha demokrasia ya vyama vingi.

Picha na1: Msajili wa Vyama vya Siasa Mhe. Jaji Francis S.K.Mutungi akionyesha kitabu chenye kuelimisha uma juu ya makatazo yaliyomo katika Sheria ya Gharama za Uchaguzi wakati wa Mafunzo ya Watumishi yaliyofanyika leo Julai 11, 2018 katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa
Picha na 2: Bi. Piencia Kiure, Msajili Msaidizi anayeshughulikia masuala ya Gharama za Uchaguzi na Elimu kwa Umma akitoa mwongozo wa namna sahihi  ya ujazaji wa  fomu za gharama za uchaguzi kwa wagombea na vyama vya siasa ambazo hubainisha mapato na matumizi wakati wa uchaguzi.
Picha na 3: Mwanasheria Mwandamizi kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa Bi. Monica Mwailolo , mmoja wa wakufunzi akiwakilisha mada  wakati wa mafunzo.
Picha na 4& 5: Baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Msajili wa Vyaa vya siasa wakati wa Mafunzo

Msajili wa Vyama vya Siasa Mhe. Jaji Francis S.K.Mutungi akionyesha kitabu chenye makatazo juu ya Sheria ya Gharama za Uchaguzi
Msajili wa Vyama vya Siasa, Mhe. Jaji Francis S. K Mutungi akifungua mafunzo kwa watumishi wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Msajili Bi. Piencia Kiure, Msajili Msaidizi anayeshughulikia Gharama za Uchaguzi na Elimu kwa Umma
.(Picha zote na Emmanuel Massaka Globu ya jamii)
Msajili Msaidizi anayeshughulikia Gharama za Uchaguzi na Elimu kwa ummaPiencia Kiure, akitoa mwongo zo juu ya jinsi ya fomu za gharama za uchaguzi ambazo hubainisha mapato na matumizi ya wagomea na vyama vya siasa wakati wa uchaguzi.

Mwanasheria Mwandamizi Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa Bi. Monica Mwailolo akiwakilisha mada wakati wa mafunzo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad