HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 3 July 2018

MKEMIA MKUU ATEMBELEA MAONESHO YA KIMATAIFA YA BIASHARA (SABA SABA)

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Profesa Joseph Bushweishaija (kushoto) akisalimiana na Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (katikati) mara baada ya Mkemia Mkuu wa Serikali kufika kwenye ofisi za Mamlaka hiyo zilizopo kwenye viwanja Saba Saba, Barabara ya Kilwa, Dar es Salaam leo. kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE), Bw. Edwin Rutageruka (aliyevaa tai nyekundu)
Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (kushoto) akimsikiliza Meneja Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Bi. Gaudensia Simwanza, mara baada ya kutembelea banda hilo kwenye viwanja vya Maonesho ya Kimataifa ya Biashara (Saba Saba) leo.
Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (kushoto) akiongea na watumishi wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) baada ya kuwatembelea kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Biashara (Saba Saba) yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (aliyevaa suti) akimsikiliza mtumishi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam alliyekuwa anamuelezea kuhusiana na uhifadhi wa mambo ya kihistoria ya kwenye vitabu kupitia muziki na makala za video alipotembelea banda la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. 
Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (wa pili kulia) akiongea na wadau waliopita kwenye banda la Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali na kuhitaji kufahamu majukumu ya Mamlaka kwa Serikali na jamii ya watanzania kwa ujumla.
Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (kushoto) akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE), Bw. Edwin Rutageruka (kulia) baada ya kufika kwenye Ofisi za Mamlaka hiyo kwa ajili ya kutembelea Maonesho ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea kwenye viwanja vya Saba Saba, Dar es Salaam. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad