HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 4 July 2018

MAMLAKA YA CHAKULA NA DAWA (TFDA) YAWEZESHA MKOA WA KATAVI KUWA NA VIWANDA VINGI VYA UZALISHAJI VYAKULA

 Picha ya pamoja baina ya Wajasiriamali Wadogo wa Usindikaji wa Vyakula mkoani Katavi, Watumishi wa TFDA, na wawezeshaji kutoka Taasisi za Serikali katika Ufunguzi wa mafunzo ya siku mbili, tarehe 2 – 3 Julai 2018 katika Ukumbi wa Mkutano wa Idara ya Maji katika Halmashauri ya Mpanda. Waliokaa kutoka kushoto ni Mgeni Rasmi, Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi, Bw. Huruma I. Mwalutanile (wa tatu); Kaimu Mkurugenzi wa Usalama wa Chakula kutoka TFDA, Bw. Justin Makisi (wa nne); Mganga Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Dkt. Omari Sukari (wa pili); Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji Mali wa Mkoa wa Katavi, Inj. Awariywa Nko (wa tano); Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya  Manispaa ya Mpanda, Bi. Enelia Lutungulu (wa sita) na Kaimu Meneja wa SIDO Mkoa wa Katavi, Bi. Salome Mwasomola (wa kwanza). Waliosimama mbele, msitari wa pili kushoto ni Meneja wa TFDA Kanda ya Magharibi, Dkt. Edgar Mahundi (wa pili).
 Baadhi ya washiriki wakiwa katika picha ya pamoja baina ya Wajasiriamali Wadogo wa Usindikaji wa Vyakula mkoani Katavi, Watumishi wa TFDA, na wawezeshaji kutoka Taasisi za Serikali katika Ufunguzi wa mafunzo ya siku mbili, tarehe 2 – 3 Julai 2018 katika Ukumbi wa Mkutano wa Idara ya Maji katika Halmashauri ya Mpanda.
Mgeni Rasmi, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya  Manispaa ya Mpanda, Bi. Enelia Lutungulu (aliyesimama) akiwasilisha hotuba ya kufunga mafunzo ya Wajasiriamali Wadogo wa Usindikaji wa Vyakula mkoani Katavi (hawapo pichani) yaliyofanyika tarehe 2 – 3 Julai 2018 katika Ukumbi wa Mkutano wa Idara ya Maji, Halmashauri ya Mpanda. Waliokaa kutoka kulia, ni Kaimu Mkurugenzi wa Usalama wa Chakula kutoka TFDA, Bw. Justin Makisi na Meneja wa TFDA Kanda ya Magharibi, Dkt. Edgar Mahundi (wa pili).

Na James Ndege - Katavi
TFDA imeendesha mafunzo ya siku mbili kwa wajasiriamali wadogo wa usindikaji wa vyakula mkoani Katavi ikiwa ni mojawapo ya mikakati yake ya kuwezesha ukuaji wa Sekta ya  viwanda nchini. Mafunzo yamehusisha wajasiriamali 120 wa mkoa wa Katavi  hayo kuanzia tarehe 2 – 3 Julai 2018 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Mpanda uliopo mjini Mpanda.
Mafunzo hayo yalifunguliwa na Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi, Bw. Huruma I. Mwalutanile aliwaasa washiriki kutumia fursa hiyo kwa ukamilifu ili waweze kukidhi vigezo muhimu vya kisheria na kuzalisha bidhaa bora, salama na zenye ufanisi ili kukidhi soko la ndani na nje ya nchi jambo litakalochangia ukuaji wa uchumi wa nchi lakini pia kulinda afya ya jamii kwa kuwa TFDA ipo karibu na kundi hili muhimu katika uanzishaji wa viwanda nchini kwa kutatua changamoto zao.
“Ili kuwawezesha wajasiriamali wadogo nchini kutatua changamoto zinazowakabili katika usajili wa majengo na bidhaa zao, uongozi wa mkoa kupitia halmashauri zake umeanza kutenga maeneo maalum ya wajasiriamali kuzalishia bidhaa zao”, Kaimu Katibu Tawala huyo alisisitiza.
Aidha, Mgeni Rasmi katika kufunga mafunzo hayo ambaye alikuwa Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Bi. Enelia Lutungulu aliwapongeza wajasiriamali kwa kujitokeza kwa wingi katika mafunzo hayo na kuwaasa kuzingatia ushauri wa wataalam katika kuzalisha bidhaa zao ili zisajiliwe na TFDA na kupata soko la ndani na nje ya nchi. “Naahidi kuyafikisha maazimio yenu katika uongozi ili yale yanayopaswa kufanyiwa kazi na Serikali yafanyike, nanyi pia mna wajibu wa kutekeleza yanayowahusu ambapo tukishirikiana kwa pamoja, suluhisho la changamoto hizo zitabadilika kuwa fursa” alihitimisha kiongozi huyo.
Washiriki wa mafunzo hayo waliwasilisha maazimio sita kwa Mgeni Rasmi wakati wa kufunga mafunzo, yanayoonesha namna changamoto zao zinavyoweza kutatuliwa katika ngazi ya mkoa kwa kushirikisha wadau wote ambao ni Uongozi wa Mkoa, Taasisi za Serikali zinazowezesha wajasiriamali wa uzalishaji vyakula, Vyama vya Wafanyabiashara na wazalishaji wenyewe ambapo waliweka lengo la usajili wa bidhaa za wajasiriamali hao kuwa kufikiwa ndani ya miezi sita kuanzia Julai, 2018.

Katika mafunzo hayo, TFDA ilishirikisha Taasisi nyingine za Serikali za Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) ili kuwawezesha wajasiriamali kutambua mambo muhimu yanayotakiwa katika kuzalisha bidhaa zinazokubalika. Mafunzo hayo ni endelevu na Katavi imekuwa mkoa wa 22 nchini kupata mafunzo ya aina hiyo.

Washiriki KATAVI:
1. Huruma I. Mwalutanile (RS Katavi) -  Kaimu Katibu Tawala – Katavi
2. Dkt. Omari Sukari – (RS Katavi) – Mganga Mkuu wa Mkoa
3. Enelia J. Lutungulu (Manispaa – MC) – Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa 
4. Salome C. Mwasomola – Kaimu Meneja SIDO Mkoa wa Katavi
5. Eng. Awariywa M. Nko (RS – Katavi) - 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad