HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, July 4, 2018

MWIJAGE AZINDUA KLINIKI YA BIASHARA SABASABA








WAZIRI wa viwanda  na Biashara Charles  ametoa angalizo kwa watu ambao wamepewa shamba la kupanda miwa mkoani kigoma kuhakikisha kuanza kazi hiyo na  akikuta shamba hilo bado halijaendelezwa atawanyan'ganya na kutoa fursa kwa wengine.

Alisema lengo la serikali nikutaka kuona ifikapo mwaka 2022 Tanzania inadhalisha tani laki sita na kuwezesha nchi kuwa na sukari ya kutosha ikilinganishwa na ilivyo sasa.

Waziri mwijage aliyasema hayo jijini Dar es Salaam jana katika uzinduzi wa wa Kliniki ya Biashara yenye lango la kusaidia ukuaji wa biashara, na kuimarisha mazingira wezeshi ya biashara kwa wafanyabiashara

Alisema kuwa kuna uwazishwaji wa mashamba matatu mapya kwa ajili ya kuzalisha miwa ambayo wamepewa wafanyabiashara katika maeneo ya Bagamoyo, Morogoro, pamoja na mkoani Kigoma.

Akizungumzia uzinduzi wa Kliniki hiyo ya  biashara Waziri Mwijage amezitaka mamlaka husika kufanya kazi katika sura ya kibinadamu kwa wafanyabishara na si kuwapelekea polisi jambo ambalo mfanyabiashara anatakiwa apewe elimu.

Ameongeza kuwa katika kuelekea Tanzania viwanda  wamefika pazuri na wanaendelea kuhamasisha kujenga viwanda vya dawa pamoja na mafuta ya kula ambayo hivi sasa yanaagizwa zaidi kutoka nje ya ya nchi.

Kwa upande wake Naibu waziri wa Biashara na Viwanda Zanzibar Hassan Hafidh akizingumza katika maonesho hayo amesema amefarijika mno kuona asilimia kubwa ya bidhaa zilizopo hapo ni za watanzania.

Naye Naibu waziri wa viwanda na biashara Stellah Manyanya ameeleza kuwa lengo kubwa ni kukimbia kuelekea mafanikio na amehaidi kuendeleza suala ambalo waziri amelianzisha na ameshauri wananchi kutoa maoni pindi wanapokutana na mambo yasiyo sawa na kupewa msaada.

Pia amewaomba wananchi kutambua dhamira ya dhati ya serikali na kuiunga mkono na kuwa wawazi na amewataka kulipa kodi kwa wakati.

Naye katibu wa wamiliki wa wenye viwanda Tanzania CTI Leodgar Tenga amemshukuru Mwijage kwa kufungua kliniki hiyo na kueleza kuwa wenye viwanda wanachukia sana urasimu na wapo pamoja katika kupeleka nchi kwenye uchumi wa kati.

Aidha ameishukuru serikali ya awamu  ya tano chini ua uongozi wa Rais Magufuli na Wizara husika na amehaidi kutoa ushirikiano kwa serikali katika ujenzi wa viwanda na wameomba uendelevu wa kliniki hiyo.
 Waziri wa Viwanda na Biashara,Cherles Mwijage akizindua kliniki ya Biashara katika Maonesho ya kimataifa yanayo fanyika Sabasaba jijini Dar as Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii)
Waziri wa Viwanda na Biashara,Charles Mwijage akizungumza na wadau mbalimbali wa biashara katika hafla ya  ukizindua  wa kliniki ya Biashara uliofanyika katika maonesho ya kimataifa yanayo fanyika Sabasaba jijini Dar as Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad