HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, July 14, 2018

DAWASCO TEMEKE KUMALIZA KERO ZA MIVUJO YA MAJI

Shirika la Majisafi na Majitaka Dar es salaam (Dawasco), limejipanga kuondoa kero ya mivujo ya Maji katika mitaa yote ya Wilaya Temeke ambayo imekuwa ikiripotiwa na wakazi pamoja na viongozi wa serikali za mtaa katika wilaya hiyo.

Hayo yamebainshwa na Meneja wa Dawasco Mkoa wa Temeke Bw. Xavery Ndondole katika kikao chake na viongozi wa serikali za mitaa cha kujadili huduma ya Maji katika wilaya hiyo ambapo ameeleza kwamba mivujo mingi inatokana na miundombinu chakavu inayoshindwa kuhimili msukumo wa Maji yaliyoongezeka katika maeneo mengi.

“Maji ni huduma ya msingi na hayana mbadala ni lazima tuzuie upotevu wa Maji ili wananchi wengine wasioyapata wapate kuyatumia hivyo nawaomba tushirikiane kwa kutoa taarifa muda wowote pale unapokutana na mivujo ya aina yoyote katika eneo lako na sisi Dawasco tutafika fika na mafundi wetu kwa wakati” alisema Ndondole

Hata hivyo mwenyekiti wa Kata ya Keko Bw. Shilingi S. Shilingi ameeleza kuwa kumekuwa na tabia ya baadhi ya Mafundi kutoka Dawasco kufanyia ukarabati mivujo mikubwa peke yake na kupuuzia taarifa za mivujo midogo midogo katika mitaa nakulekea madimbwi na mitaro kujaa.

“Mivujo imekuwa kero na hata gari zenu zinapita huko mitaani kwetu wanafika ila bado kuna mabwawa, mivujo ni mingi ila mafundi wenu wanafanyia kazi mivujo mikubwa lakini midogo wanaacha bila kufanya chochote nahii ndo mingi huko kwetu” alisema Shilingi.

Pia katika kikao hicho uongozi wa Dawasco Temeke umewaomba viongozi hao wa serikali za mitaa kutoa ushirikiano kwa wananchi wanaohitaji huduma ya Maji kwa kuwapa fomu za utambulisho ili waweze kuunganishiwa huduma ya Maji kwa wakati.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad