HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, July 14, 2018

UTUNZAJI WA FUKWE KUTALETA WATALII WENGI NCHINI- TTB


 Wafanyakazi wa Bodi ya Utalii Nchini (TTB) pamoja na wafanyakazi wa Ramada Resort Dar es Salaam wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumalizika kwa usafi uliofanyika kwenye fukwe ikiwa na lengo la kuzitumia kama vivutio kwa watalii.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Bodi ya Utalii Nchini (TTB) kwa kutambua umuhimu wa vivutio vingi zaidi nchini mbali na wanyama pori wamekeza msisitizo zaidi katika utalii wa fukwe na majiji hususani Dar es Salaam. TTB wameanza na wadau wa mahoteli ya kitalii Jijini Dar es Salaam kwa kufanya usafi kwa pamoja kwenye fukwe ilyopo Hotel ya Ramada na fukwe za jirani. Kwa pamoja TTB na wadau wengine watakutana katika kikao kitakachofanyika Julai 19 mwaka huu kitalenga zaidi kutafuta njia mbadala ya kuzuia takataka zisiingie baharini.

Akizungumza baada ya kumaliza usafi, Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Nchini (TTB) Ernest Mwamwaja amesema lengo kuu la kufanya usafi huu ni katika kuhakikisha wanaboresha fukwe zote na majiji ili kuweza kuwa kivutio kwa watalii nchini. Mwamwaja amesema kuwa, ukiachilia mbuga za wanyama ambazo zipo nchini, fukwe za bahari kwa upande mwingine zinatakiwa ziwe safi ili kuvutia zaidi watalii pindi wanapokuja nchini.

Amesema kuwa, kama watalii watakuwa wanavutiwa na mazingira ya Fukwe ifikapo mwaka 2020 tunaweza kufikia wastani wa watalii Milioni 2 kwa mwaka pamoja na pato la taifa kuongezeka kutoka Dola Bilion 2.1 hadi 4.2 kwa mwaka.

 Kaimu Meneja wa Utalii Bodi ya Utalii Nchini Joseph Sendwa amesema kuwa kikao na wadau kitakachofanyika mwezi huu kitaleta maboresho makubwa sana katika sekta ya utalii kwakuwa kwa pamoja watatoka na azimio la kuhakikisha wanafanya usafi katika fukwe zote ikiwemo kwenda maeneo ya makazi ya watu yanayopita mkondo wa bahari ambapo kumekuwa na changamoto kubwa ya wananchi kutupa taka ovyo.

Mbali na hilo, Sendwa amesema wameanzia katika fukwe ya Ramada ila wataenda sehemu zote za Dar es Salaam ikiwemo pia kutoa elimu kwa wananchi kuhusiana na utunzaji wa mazingira.
 Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Nchini(TTB) Ernest Mwamwaja akiwa pamoja na Mkurugenzi wa Masoko wa Ramada Resort Dar es Salaam Barath Swarup wakifanya usafi kwa pamoja katioa fukwe ya Hotel hiyo uliofanyika kwa ushirikiano wa pamoja leo Jijini Dar es Salaam.
Usafi ukiendelea ndani ya fukwe Ramada Resort Dar es Salaam  wakiwa pamoja na Raia wa Ufaransa anayeishi katika Visiwa vya Reunion JeanMart Francois akishirikiana na Wafanyakazi wa TTB na Ramada kufanya usafi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad