HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, July 16, 2018

BEI YA UFUTA WILAYA YA KIBITI YAZIDI KUPAA

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
 Wakulima wazidi kuneemeka kwa mfumo wa stakabadhi ghalani.
HALMASHAURI ya Wilaya Kibiti imezidi kuwaneemesha wakulima wa ufuta kutokana na bei ya mnada kupanda ni baada ya serikali kuagiza zao hilo kuuzwa kwa mfumo wa stakabadhi ghalani na kufanya wakulima kunufaika na kilimo hichio.

Hayo yamesemwa na  Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Gulamhussein Kifu  wakati wa mnada wa tano wa zao la Ufuta katika wilaya hiyo amesema kuwa mnada huo ni wa tano na bei bado imekuwa ikiongezeka kutoka 2750  katika mnada wa kwanza  hadi kufikia sh.3115 katika mnada wa tano  kwa kilo moja ya Ufuta.

Amesema kuwa licha ya kuwa mnada kuwa mzuri kwa wakulima wanatakiwa kuhifadhi  Ufuta bora ili wafanyabiashara bidhaa bora.

Kifu amesema kuwa wakulima wataopatikana kutia doa pamoja na vyama ushirika hawataacha salama.

Amesema mnada huo ukiharibiwa na watu wachache kwa makusudi binafsi kutafanya wafanyabiashara wakimbie soko.

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti Alvera Ndabagoye katika minada Mitano wa wameuza kilo zaiidi ya Milioni 1.6. 

Amesema mafanikio hayo ni dhahiri kuwa uzalishaji wa ufuta utaongezeka katika msimu ujao ,kwani wakulima walikata tamaa kutokana na bei  ndogo waliyokuwa wakiuza kwa walanguzi.

Aidha amesema kuwa baadhi ya wakulima kupeleka ufuta katika maghala bila kuusafisha na kusababisha malalamiko kwa wafanyabiashara.

"Kitendo cha kupeleka ufuta bila kusafisha ni makosa na tabia hiyo iachwe mara moja na kila mkulima asafishe ufuta wake"amesema Ndabagoye.

Amesema chama chochote cha msingi au mkulima wataobainika kupeleka ufuta bila kusafisha watachukuliwa hatua  za kisheria pamoja na kufunga ghala husika.
 .Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Gulamhussein Kifu akihutubia katika mnada huo uliofanyiaka katika ofisi ya mkuwa wilaya.
 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kibiti Khatib Chaurembo akizungumza katika Mnada wa  Ufuta kuhusiana na kuhifadhi ufuta katika mazingira bora.
 Mkurugenzi wa Mtendaji  wa Kibiti Alvera Ndabagoye akizungumza katika  mnada huo.
 Watunza funguo Afisa Ushirika wa Wilaya na Mwenyekiti wa AMCOS ya Kibiti wakifungua sanduku la tenda.
Baadhi ya wafanyabiashara, wakulima na watumishi waliohudhuria mnada huo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad