HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, 11 June 2018

WATU SABA WAKAMATWA HIFADHI YA SAADAN KWA TUHUMA ZA KUFANYA UWINDAJI HARAMU KWA KUTUMIA SILAHA

Na Linda Shebby,  Chalinze
JESHI la Polisi  Mkoa wa Pwani kwa kushirikiana na  Shirika la Hifadhi ya Taifa (TANAPA) wamewakamata  watu saba katika hifadhi  ya Saadan ambao  wamekutwa wakimiliki silaha ambazo walikuwa  wakizitumia  kufanyia uwindaji  haramu   katika hifadhi hiyo  bila ya kuwa na kibali.

Huku wakituhumiwa kumuua myama mmoja adimu anayepatikana kwenye hifadhi hiyo ya Saadan pekee    aliyemtaja kwa jina  Pongwe 

Akizungumza leo Kamanda wa  Polisi  Mkoa wa  Pwani Jonathan Shanna amewataja watuhumiwa waliokamatwa  kuwa ni Hadija Rashid ( 32 )mkazi wa Mkange   amekamatwa na Magobore mawili, Amina Athumani (30) mkazi wa Gama  amekamatwa na  risasi tisa  za Short Gun, Mohamed Athuman  (65) mkazi wa Manda  ambaye amekamatwa  magobore mawili Yusuph Salum( 62) ,pamoja  na Salum  Ramadhan( 96)mkazi wa  Manda amekamatwa na magobore  mawili. 

Kamanda Shanna amewataja watuhumiwa wengine kuwa ni  Athumani Abdully (26), Siwatu Bakari(40) na Mussa  Abdully wote wakazi wa Manda  na walipokamatwa kila mmoja alikiwa na gobore moja.

Kutokana na tukio hilo Kamanda Shanna ametoa siku moja kwa raia wanaomiliki silaha isivyo halali kuzisalimisha mara moja.

Katika tukio la pili Jeshi  la Polisi  mkoani hapa  wamekamata gari lilikokuwa  limeibiwa  katika eneo la vigwaza  mapema mwaka huu lenye namba za usajili T 265 BZC aina ya  Mitsubish Canter tukio hilo lilitokea  baada ya kundi la watu sita.

Huku mmoja wao akijifanya ni Mwalimu wa Shule  ya sekondari Vigwaza akiwa na wenzake walimfuata dereva  aitwaye Omari Nyange(39) na kumwambia kuwa  wanataka kumkodi ili wakahamishe vyombo dereva huyo alikubaliana na watu hao  na walipoanza safari ya kwenda eneo la Madafu walimbadilikia na kumkaba  kisha  kumpora  gari  hilo na yeye kumtupa nje.

Baada ya taarifa hizo kufika katika Jeshi la Polisi walianza upelelezi na Juni 6 mwaka huu wakalikamata  katika Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro baada ya mwizi mmoja kukamatwa aliyetajwa kwa jina la Kasimu Nasoro(40) ambaye amekiri kuhusika na tukio hilo.

Amefafanua amekiri kuwa baada ya kuiba gari hilo walilibadilisha namba  na kufunga namba za bandia  ambazo ni T 525 ABM na kulisafitisha hadi Mangula.

Ambako walitengeneza kadi bandia  na kwenda kuliuza  kwa kiasi cha Sh. 8,000,000 kwa Florida  Stanslaus  mkazi wa Mang'ula  Morogoro.

Katika tukio la tatu Jeshi la Polisi  katika mzani wa Msata Wilaya ya Kipolisi Chalinze wamekamata  madumu matupu yanayodaiwa kukamata gari aina ya fuso lililokuwa linaendeshwa na dereva likiwa limebeba vyuma chakavu ambavyo havikulipiwa ushuru wa serikali ambapo walitozwa faini kiasi cha Sh. milioni 2,000,000 na maofisa wa kuhifadhi na kutunza mazingira kwa kosa la kukwepa ushuru.
 Kamanda wa polisi mkoani Pwani ACP Jonathan Shanna akionyesha pembe ya mnyama ajulikanae kama pongo na silaha mbalimbali ambazo zimekamatwa katika misako inayoendelea.
Kamanda wa polisi mkoani Pwani ACP Jonathan Shanna akionyesha gari lililokuwa limeibwa na kubadilishwa namba za usajili (bandia).
Baadhi ya silaha zilizokamatwa na jeshi la polisi mkoani Pwani

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad