HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, June 11, 2018

VIONGOZI WA UMMA 946 MALI ZAO KUANZA KUHAKIKIWA JUNI 18 MWAKA HUU

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
SEKRETARIETI ya Maadili ya Viongozi wa Umma imesema inatarajia kuhakiki  mali za viongozi wa umma 946 kwa lengo la kujiridhisha na uhalisia mali hizo na tamko walilojieleza.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Kamishina wa Maadili Jaji Mstaafu Harold Nsekela amesema kuwa lengo la uhakiki huo ni ni kuthibitisha uhalisia wa mali hizo kulinganisha tamko la rasilimali  na madeni la kiongozi.
"Mali za kiongozi wa umma zinatakiwa kuonesha thamani halisi ya mali hizo na  uhalali wa mali zilivyopatikana,"amesema.
Jaji Mstaafu Nsekela amesema uhakiki utafanywa na maofisa wa sekretarieti ya maadili na kila kiongozi anayetakiwa kuhakikiwa ataandikiwa barua kwanza ili kujua rasilimali na madeni yake yatakayohakikiwa.

Pia waandae nyaraka mbalimbali za mali hizo na waweze kuwaonesha maofisa wa sekretarieti hiyo.
Amefafanua uhakiki huo utaanza Juni 18 mwaka huu, hivyo kila kiongozi mara baada ya kupata barua ya uhakiki wa mali zake ajiaandae.

Amesema kuwa lengo la barua hiyo ni kuepusha watu wenye nia ovu kwa kutumia mchakato huo wa uhakiki kutapeli viongozi na maofisa wa sekretarieti watakaohusika na uhakiki waoneshe vitambulisho vyao.

"Na viongozi ambao hawataridhika na utambulisho huo wanaweza kuwasiliana na ofisi ya Sekretarieti ya Maadili kupitia simu namba 0222111810/11,"amesema.
Kamishina wa Maadili Jaji Mstaafu, Horold Nsekela akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana uhakiki wa mali za viongozi kujiridhisha na matamko waliondika katika mkutano wa uliofanyika jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad