HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, June 30, 2018

WATANZANIA KAENI MKAO WA KUKALIA KITI CHA NDEGE MPYA YA DREAMLINER 787–ATCL

Na Said Mwishehe, Globu ya jamii
WATANZANIA nchini wametakiwa kukaa mkao wa kukalia kiti cha ndege mpya ya Boeing Dreamliner 787 itakayokuwa na uwezo wa kubeba abiria 262 ambayo inatarajiwa kuwasili nchini hivi karibuni.

Hayo yamesemwa na Ofisa wa Idara ya Biashara wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) Lily Fungamtama wakati anazungumza na wananchi waliofika kwenye banda la ATCL lililopo kwenye Maonesho ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea Sabasaba jijini Dar es Salaam.

“Watanzania wakae mkao wa kukakilia kiti cha ndege mpya yenye uwezo wa kubeba abiria 262 .Ndege ambayo inauwezo wa kukaa angani muda mrefu,”amesema Fungamtama.

Ameongeza kuwa watanzania wana kila sababu ya kumuunga mkono Rais Dk.John Magufuli kwa kuhakikisha wanapanda ndege hiyo yenye uwezo wa kusafiri masafa marefu.

Amewahakikishia wananchi wote kuwa ATCL imejipanga kutoa huduma bora na za kisasa na kufafanua kuwa wafanyakazi wa ndege zao wamepikwa katika kutoa hduma bora na kuzingatia heshima na maadili ya mtanzania.

Ameongeza kuwa wafanyakazi wa ndege wameandaliwa vema kupitia chuo cha ATCL Training Institute ambacho jukumu lake ni kuandaa wafanyakazi wenye viwango bora vya kutoa huduma katika ndege za shirika hilo.

“ATCL tunatoa huduma katika kiwango cha juu kwa kuzingatia misingi ya maadili ya mtanzania.Tumejipanga vema kuwahudumia Watanzania wote na kwa sasa tunasubiri ujuo wa ndege mpya ya Dreamliner,”amesema.

Mmoja ya wananchi waliofika kwenye banda la ATCL ambaye jina halikupatikana alisikika akisema hajapanda ndege ya Bombardier lakini atahakikisha Dreamliner anaipanda.

“Hii Dreamliner lazima nitaipanda tu maana kutoka Tanzania hadi Mumbai nchini India tunasafiri angani bila kuchimba dawa.Lazima niipande tu na ni vema nikamuunga mkono Rais wangu kwa vitendo,’amesema.
 
Ofisa wa Idara ya Biashara wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) Lily Fungamtama akizunguza na wageni mbalimbali waliotembelea katika banda la ATCL katika maonyesho ya biashara ya TANTRADE viwanja vya Sabasaba. 
 
Ofisa wa Idara ya Biashara wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) Lily Fungamtama akizunguza na wageni mbalimbali waliotembelea katika banda la ATCL katika maonyesho ya biashara ya TANTRADE viwanja vya Sabasaba.
 
Mmoja wa akina mama ambaye jina lake halikupatikana akiwa katika picha huku akionyesha 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad