HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, 19 June 2018

WASAFI TV RASMI NDANI STARTIMES

 KAMPUNI ya Star Media (T) Ltd kupitia chapa yake ya StarTimes imetangaza rasmi uwepo masafa ya Wasafi TV katika king'amuzi cha Startimes kupitia king’amuzi chake, uzinduzi huo umefanyika leo June 19 katika Hotel ya Slipway, Masaki jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na vyombo vya habari Meneja wa Masoko na Matangazo wa StarTimes, David Malisa ameeleza kuwa  chaneli hiyo mpya ya burudani itaweza kutazamwa na watu wengi zaidi Tanzania kwa sababu StarTimes ndicho king’amuzi chenye watumiaji wengi zaidi nchini.

Malisa  ameeleza kuwa kuanzia sasa Wasafi TV itapatikana pia katika ving’amuzi vyao vya Antenna, hivyo watumiaji wa Antenna wanaweza kutazama chaneli hiyo mpya ikiwa na vipindi vipya ambavyo vitatangazwa baadaye. Pia wateja wanaweza kulipia kifurushi chochote cha Antenna na kuipata Wasafi TV na malipo hayo yanafanywa unaweza kulipia NYOTA kwa 7000 tu mwezi mzima, MAMBO Tsh 13,000 tu kwa mwezi na UHURU kwa 24,000 tu. 

imeelezwa kuwa Wasafi TV imekuja na lengo kubwa la kuwainua vijana tofauti na ambavyo watu wengi wanafikiria. Ndoto kubwa walizonazo vijana huko mtaani sasa wanaelekea kuzitimiza. Pia Wasafi TV kitakuwa chombo cha kukuza sanaa nchini, kwa sababu wasanii wanajuana  na wana uwezo wa kusaidiana wenyewe kwa wenyewe.

Mbali na kutazama chaneli ya Wasafi TV wateja wa StarTimes wanaweza kuendelea kutazama mechi zote za Kombe la Dunia katika kiwango safi kabisa cha picha, HD t kwa lugha ya Kiswahili. 

Naye msanii wa kizazi kipya Naseeb Abdul ambaye ni mmiliki wa Wasafi Tv amefurahi kuingia makubaliano na Startimes na kwa sasa chaneli ya Wasafi itaonekana kupitia chaneli 444.

Aidha ameeleza kuwa kupitia chaneli hiyo watazamaji wajiandae kupata burudani na waendelee kutoa ushirikiano katika kukuza na kupeperusha bendera ya Tanzania kupitia sanaa.
Msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Wasafi TV kuunganishwa kwenye king’amuzi  cha Startimes katika ukumbi wa Hotel ya Slipway jijini Dar es  Salaam.
Msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' (kushoto) akisaini mpira wa Startimes Tanzania bara baada ya kumalizika kwa uzinduzi wa Wasafi TV kwenye king'amuzi cha Startimes. Katikati ni Meneja wa Masoko na Matangazo wa StarTimes, David Malisa na kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Maudhui ya Startimes, Zamarad Nzowa.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad