HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, June 19, 2018

SANGA APIGA MARUFUKU MALORI KUPITA KATIKA MIUNDOMBINU INAYOTENGENEZWA

Naibu Waziri wa Mifungo na Uvuvi na Mbunge wa Mkuranga ,Abdallah Ulega akishiriki unjenzi wa daraja katika kijiji cha Mipeko katika ziara ya kukangua mirandi mbalimbali.

Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii.

MKUU wa Wilaya ya Mkuranga Filberto Sanga amemshukuru Rais na viongozi wote ambao wanashiriki katika ujenzi wa taifa.

Pia amehaidi kutoa ushirikiano wakandarasi ili waweze kutekeleza miradi na amezuia malori kupita katika kijiji cha Kitoga kwa muda wa miezi miwili hadi ujenzi wa daraja hilo utakapokamilika. 


Akizungumza leo Sanga pia amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi Julai 12 kuupokea Mwenge wa uhuru ambao utafungua miradi mingi ya kimaendeleo.

Kwa upande wa Mbunge wa Mkuranga na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akiwa katika ziara yake katika jimbo la Mkuranga ameendelea kukagua ujenzi wa barabara katika kata za Tambani, Mipeko, Mkuranga, Kimanzichana, Mkamba na kata ya Kisegese.

Ulega ameeleza kuwa ziara hiyo imelenga kukagua ukarabati wa barabara mara baada ya mvua kunyesha, na amesema kuwa wamekagua katika kata mbalimbali na wameridhishwa na utendaji kazi unaofanywa na wakandarasi katika kutekeleza mradi huo kwani fedha iliyotolewa na kinachofanyika vinawiana.


Aidha Ulega amemshukuru Rais Magufuli kwa kuangalia mahitaji ya wananchi na kuyafanyia kazi na kuahidi kuwa kama wasaidizi wake watamuunga mkono katika kulipeleka taifa katika hali nzuri ya uchumi na kuhakikisha wananchi wanapata huduma zote muhimu.

Amewataka wananchi kutunza miundombinu hiyo ili kuwarahisishia shughuli mbalimbali na kuweza kudumu kwa matumizi ya kizazi kijacho.
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Filberto Sanga akishiliki ujenzi wa daraja katika kijiji cha Mipeko katika ziara ya kukangua mirandi mbalimbali iliyo fanyika leo mkoa wa Pwani.(Picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii)
Naibu Waziri wa Mifungo na Uvuvi Abu na Mbunge wa Mkuranga,Abdallah Ulega akizungumza na baadhi ya wananchi wa kijiji cha Mihekela alipo tembelea na kukangua barabara ya kijiji hicho na kumuomba meneja TARURA kujenga barabara hiyo Kwa kiwango ubora na na kuhakiksha sehemu korofi zinaimarika.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega  (kushoto) akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Filberto Sanga  (kulia) mara baada ya kukagua miradi ya barabara.
Muonekano wa daraja la Mipeko Wilayani Mkuranga ambalo lipo katika katengeneza.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad