HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, 19 June 2018

VYUO VIKUU VYATAKIWA KUJIKITA KATIKA SERA YA UCHUMI WA VIWANDA

Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii
Vyuo Vikuu nchini vimetakiwa kuhakikisha vinafundisha kozi zitakazozalisha wataalamu wengi  watakaoendana na Sera ya Serikali ya awamu ya tano ya uchumi wa viwanda.

Rai hiyo imetolewa leo  na Mkuu wa Chuo kinachotoa mafunzo ya Tehama cha Power Computer LTD (PCTL), Avelin Malamsha, wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya kozi mpya wanaotarajia kuitoa yenye lengo la kuwajenga vijana kiajiliwa katika hadhi ya kimataifa na viwanda.

Amesema, wadau wa sekta ya elimu wanapaswa kujitafakari kwa kuanzisha kozi zitakazozalisha wataalamu katika sekta ya viwanda na uwekezaji nchini kwani elimu ni jambo kubwa kwa sasa na linashika kasi nchini ambayo tunategemea itazalisha wasomi wengi watakaokuja kusaidia nchi.

Malamsha ameongeza kuwa, ili kuendana na Sera hiyo ya Tanzania ya viwanda na upatikanaji wa ajira chuo hicho cha PCTL kimeanzisha kozi mpya ya kimataifa ya Tehama (ICDL) itakayowajengea uwezo vijana kidigitali na kuajiria sehemu yoyote duniani.

Amesema, Tanzania ya viwanda na ajira itakuwepo pale ambapo kila mmoja akielewa mchango wake katika hili, pia itakuwepo kama tutakuwa na rasilimali watu wa kutosha na sahihi, “PCTL kama chuo tukaona kwamba tuna wajibu kuijenga Tanzania ya hiyo viwanda na kupunguza tatizo la ajira kupitia kozi yetu mpya ya ICDL," alisema.

Naye Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Kimataifa linalotoa Cheti cha kozi hiyo ya ICDL, Edwin Masanta alisema baada ya kuona mapungufu yaliyopo nchini wameona ni vema kuileta kozi hiyo.

"ICDL inaongeza nafasi ya ajira kwa vijana kwani inatoa wataalamu wengi katika masuala ya komputa kwenye vigezo vya kuajiliwa popote duniani," alisema.
Mkuu wa Chuo cha mafunzo cha PCTL, Avelin Malamsha akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kuhusu program za kompyuta zinavyoweza kusaidia Tanzania kuimarika na kukua katika viwanda na kuongeza ajira kwa vijana. Kulia ni mkuu wa Itifaki kwa wanafunzi, Daniel Ngumbuke na Mkurugenzi wa PCTL nchini, Edwin Masanta.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad