HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, 19 June 2018

TIB CORPORATE WATUMIA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA KUPOKEA MAONI YA WATEJA WAO
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

BENKI ya  TIB Corporate imewataka wateja wake kutoa maoni yao juu ya huduma wanazopatiwa katika benki hizo ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya utumishi wa umma.

TIB wamewataka wateja wa benki hiyo kuelezea changamoto wanazokutana pindi wanapokuja kupata huduma ili waweze kuzifanyia kazi.

Akizungumza na wateja wa benki ya TIB Mkurugenzi  Mkuu wa TIB Corporate Bank , Frank Nyabundege amesema kuwa wiki hii ya utumiashi wa umma wataitumia kwa ajili kupokea maoni ya wateja wao kuhusiana na huduma wanazozipata.

Nyabundege amesema kuwa wiki hii ni muhimu sana kwa uongozi wa TIB kufahamu na kupata maoni kutoka kwa wateja wao ambapo itawasaidia kuzitatua na kuona wapi walikosea ili kuweza kufanyia marekebisho.

Wakielezea huduma wanazozipata katika benki ya TIB Denis Kabogo kutoka Mbeya amesema kuwa benkk hiyo ina huduma nzuri ila anawaomba waongeze matawi sehemu mbalimbali za nchini ikiwemo mkoa wao wa Mbeya, Naye Mteja wa muda mrefu na Mbunge Ahmed Salum amesema kuwa anafurahia sana huduma za benki ya TIB na amewataka waongeze ufanisi hususani katika kutumia huduma za kifedha kupitia mitandao ya simu kwani ni njia rahisi sana pale unapokua na hela nyingi inakua rahisi kuziamishia kwenye akaunti moja kwa moja.

Wiki ya maadhimisho ya utumishi wa umma imeanza Juni 19 hadi Juni 22 nchini ambapo mashirika na taasisi mbalimbali nchini zimekuwa zikiadhimisha kwa kupokea maoni mbalimbali kutoka kwa wateja wao.

Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya TIB Corporate Frank Nyabundege akizungumza na wateja wa benki hiyo katika kuadhimisha wiki ya utumishi wa umma na kuwataka kusema changamoto zao ili waweze kuzifanyia kazi.
Mteja na mbunge Ahmed Salum akizungumza mbele ya uongozi wa Benki ya  TIB Corporate leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Matawi na Masoko Benki ya TIB Corporate Theresia Soka akizungumza na wateja katika kuadhimisha wiki ya utumishi wa umma nchini leo Jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa Benki ya TIB Corporate.
Wateja wa Benki ya  TIB Corporate.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad