HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, 29 June 2018

TRC WAZINDUA TRENI YA MIZIGO KUELEKEA KAMPALA

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
SHIRIKA la Reli Tanzania (TRC) limezindua treni ya mizigo kuelekea Nchini Uganda ikiwa imebeba shehena ya mzigo wa tani 2,400 wa Shirika la Chakula Duniani (WFP) na kunusuru takribani dola 96,000 sawa na shiilingi Milioni 211,200,000 za gharama ya usafirishaji.

Treni hiyo iliyoanza safari imezinduliwa na Kaimu Mkurugenzi Uendeshaji Focus Makoye Sahani na kusema utekelezaji huu ni maagizo ya Rais ws Jamhuri yw Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwa wakurugenzi wa Shirika la Reli na mamlaka ya bandari kuhakikisha treni ya mizigo inafanya kazi  akiwa katika ziara ya kikazi  nchini Uganda.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Sahani amesema kuwa treni hii ya mizigo ilisimama toka Agosti 2009 wakiwa chini ya mwekezaji   ila kwa juhudi zilizofanywa na mamlaka ya bandari na shirika la Reli limefanikisha kurejea kwa usafiri huo kuelekea nchini Uganda.

Sahani amesema kuwa, kwa mara ya hii ya kwanza wamepata ofa ya tani 2,400 toka kwa WFP utakuwa ni kwa treni tatu pia wanashukuru sana kwani njia ya reli ni usafiri mzuri na wenye uhakika na wameweza kushirikiana na Shirika la reli  Nchini Uganda na kufanikiwa kukarabati eneo la Km 9 kuelekea Kampala lililokuwa linasumbua.

"Tumeshirikiana na Shirika la Reli Uganda katika kufungua njia inayoelekea Kampala kwa kuwapatia vifaa vya kufungulia njia hiyo yenye km 9,"amesema Sahani.

Sahani amesema anaishukuru serikali ya Tanzania kwa kuweza kupata vichwa vya treni vipya na vifaa vingine ambavyo vitaboresha huduma zao za usafirshaji kuanzia sasa.

Mkuu wa Usafirishaji wa WFP Muhamad Mabuyu amesema kuwa wameokoa dola 40 kwa kila tani ambapo thamani yake ni zaidi ya Milioni 211 za kitanzania kama wangetumia usafiri wa njia ya barabara, na hiyo hela kwa sasa itatumika kununulia mahitaji mengine kwa ajili ya wahanga mbalimbali.

Mabuyu amesema, treni hii ya mizigo itatoka kuanzia katika hifadhi yao ya chakula bandarini Dar es Salaam na itafika moja kwa moja katika hifadhi yao ya nchini Uganda katika Jiji la Kampala," Tumeweza kutumia usafiru wa njia ya reli kwani ni rahisi na wenye uhakika kwakuwa mwaka 2017 tulisafirisha tani 16,000 kuelekea Mkoani Dodoma na haikupotea hata kiroba kimoja cha kilo 50."

Mabuyu amesema,mbali na tani hizo zinazoelekea Kampala, kuna tani zingine 15,000 zinaanza kuingia kesho ambazo pia tutatumia usafiri wa njia ya reli kuzisafirisha na iwapo wangetumia magari ya tani 30 wangeingia gharama kubwa sana ya magari 500 ila watatumia treni 19 kufikisha mzigo huo .

WFP wameweza kusifia huduma za TRC na kusema yeye kama mdau wa usafirishaji anaupongeza sana uongozi wa TRC na serikali kwa ujumla kwa kuweza kufanikisha huduma hii ya njia ya reli kurudi ikiwa ni baada ya miaka 10
 Kaimu Mkurugenzi Uendeshaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Focus Makoye Sahani akizungumza na waandishi wa habari kabla kuzindua treni ya mzigo  kuelekea nchini Uganda ikiwa ni baada ya miaka 10 toka kusitishwa kwa huduma hiyo ya usafirishaji.
 Mkuu wa Usafirishaji wa Shirika la Chakula Duniani Nchini Tanzania (WFP) Muhamad Mabuyu akizungumza na waandishi wa habari na kuelezea ubora na ufanisi mzuri wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) katika ufanisi wa usafishaji mizigo wakati wa uzinduzi wa treni ya mizigo kuelekea Nchini Uganda.
  Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji Focus Makoye Sahani akizindua treni ya mizigo na kuashiria kuanza kwa huduma hiyo baada ya kusimama kwa kipindi cha miaka 10.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad