HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, June 29, 2018

Unesco wakabidhi kijiji digitali cha Ololosokwan kwa serikali

SHIRIKA la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) wamekabidhi rasmi kijiji cha digitali cha Ololosokwan katika sherehe kubwa iliyofanyika kijijini hapo na kuhudhuriwa na viongozi wa serikali na mashirika ya Umoja wa Mataifa.
Katika kukabidhiana huko Unesco imesema kwamba itaendelea kutoa msaada katika mtandao wa intaneti kwa miezi sita ijayo.
Katika hotuba yake iliyosomwa kwa niaba na Dk. Abdul Rahman Lamin, Ofisa msimamizi wa ofisi ya Unesco, Ann Therese Ndong-Jatta alisema kwamba wakati wanakabidhi facility hizo wamefurahishwa na ushirikiano mkubwa waliopewa katika mradi huo.
Kijiji cha digitali cha Ololosokwan ni moja ya vijiji vinne ambavyo vimefadhiliwa huku vikitoa huduma muhimu za elimu, afya na biashara kuendeshwa kidigitali.
Kijiji hicho cha digitali ambacho ni matokeo ya ushirikiano kati ya UNESCO na kampuni ya Samsung imelenga kutoa elimu kwa kutumia njia ya mtandao, kufaniklisha tiba mtandao na pia kutumia mtandao wa kompyuta katika kuwezesha biashara.
Ofisa huyo alisema kuna haja ya kuendeleza ushirikiano uliopo ili mradi uweze kuendelea kuchangia maendeleo ya wakazi wa eneo hilo.
Aidha aliitaka serikali kuhakikisha kwamba inaendeleza ushawishi kwa wananchi wa eneo hilo la Ngorongoro kutumia vyema teknolojia ya kisasa katika kufanikisha maisha endelevu ya zana zilizopo.
“UNESCO inajisikia furaha kwa kutambua kwamba kupitia mradi wa kijiji cha digiti, wilaya ya Ngorongoro imekuwa miongoni mwa waanzizilishi wa matumizi ya Tehama katika kufanikisha elimu na afya nchini Tanzania. “ alisema Ndong-Jatta .
Alisisitiza kuwa kuwapo kwa kijiji hicho kunaambatana na mamchakato wa sasa wa serikali ya awamu ya tano ya kuwa na taifa lenye uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.
“Nataka kuhakikishia wilaya ya Ngorongoro, kijiji cha Ololosokwan na serikali ya Tanzania kwamba UNESCO itaendelea kutoa msaada wa kiufundi na kuhakikisha kwamba kunakuwa na maendeleo endelevu kwa kijiji hichi” alisema Ndong-Jatta.
Akipokea mradi huo Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mh. Mrisho Gambo alisema kwamba serikali ina mipango endelevu ya kuhakikisha kwamba kijiji hicho kinaendelea kuwa cha mfano.
Alisema kijiji hicho kitapitiwa na umeme ili kuongeza nguvu ya nishati iliyopo sasa inayotegemea umeme jua.
Aidha alisema kwamba serikali imefurahishwa na mradi huo ambao umelenga kusaidia wananchi wa eneo hilo hasa katika afya, uchumi na elimu.
Alisema eneo hilo linachangamoto kubwa kutokana na  utamaduni wa wafugaji wa kimasai ambapo elimu ya watoto wote wakiwamo wa kike .
Alisema wataendelea kukabiliana na changamoto zilizopo za wafugaji katika elimu kuhakikisha kwamba watoto wa kimasai wanapata elimu pamoja na tabia iliyopo ya uhamaji.
Pia alisema wapo tayari kushirikiana na watu wote wanaotaka kusaidia maendeleo ya Tanzania kwa kuzingatia matakwa ya nchi ya maendeleo.
Alishurukuru Unesco na Samsung kwa kusaidia jamii ya ufugaji kufanya zaidi ya kufuga Ng’ombe hasa kwa kuhakikisha kila kitu katika Ng’ombe kuna kazi zao.
Alishukuru kwa kusaidia kuwepo kwa utaalamu wa kutengeneza vifaa vya kitalii kwa kuwa na eneo la kisasa lenye bidhaa za kitamaduni zinazochangia kukuza uchumi wa Ololosokwan.
Naye Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro, Mh.  Rashid Taka alisema kwamba anashukuru kuwapo kwa mradi huo na kwamba wameupokea mradi na kuahidi kuufanya kuwa endelevu.
Alisema kwa mujibu wa utaratibu uliowekwa ni mali ya jamii na kwamba uongozi wa wilaya utaweka macho kuhakikisha kwamba uendeshaji wa kijiji unakwenda unavyostahili kuwa.
Naye Dkt.  Felix Sukums wa MUHAS amesema kwamba wataendelea kuboresha huduma ya afya kwa njia ya mtandao kwa kutoa huduma masafa na ushauri wa kitaalamu kwa njia ya mtandao mara tu tatizo la mtandao litakapomalizwa kwa kushirikiana na UNESCO tiba mtandao 
Naye Naibu Katibu Mkuu Elimu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Avemaria Semakafu ameshukuru kwa Unesco kukabidhi kijiji cha digitali na kulitaka shirika hilo kusaidia elimu ya watu wazima kwa kutumia kituo hicho.
Amesema kwamba wizara ya elimu imejifunza mno kuhusu teknolojia inavyoweza kutumiwa katika elimu ya masafa.
Anasema kijiji hicho kimefunza mengi kutokana na mafanikio makubwa yanayoonekana katika matumizi ya teknolojia.
 Mwakilishi wa Mkurugenzi wa UNESCO kanda ya Afrika Mashariki, Bw. Abdul Rahman Lamin akisaini kitabu cha wageni katika Zahanati ya Ololosokwan wilayani Ngorongoro huku akibadilishana mawazo na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mh. Mrisho Gambo (kushoto) walipotembelea zahanati hiyo pamoja na mambo mengine kuangalia ufanisi wake ambapo ziara hiyo iliambatana na hafla ya Unesco kukabidhi kijiji digitali cha Ololosokwan kwa serikali wilayani Ngorongoro mkoani Arusha. Wengine ni kulia aliyeketi ni Naibu Katibu Mkuu Elimu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Bi. Avemaria Semakafu pamoja na na Kaimu Katibu Mkuu wa Tume ya Taifa wa UNESCO nchini Tanzania, Dkt. Moshi Kimizi ( wa pili kulia)
 Kaimu Katibu Mkuu wa Tume ya Taifa wa UNESCO nchini Tanzania, Dkt. Moshi Kimizi (wa pili kushoto aliyeketi) akisaini kitabu cha wageni katika Zahanati ya Ololosokwan kabla ya kuanza ziara fupi ya kutembelea kituo hicho cha afya na kuangalia ufanisi wake ambapo ziara hiyo iliyoambatana na hafla fupi ya Unesco kukabidhi kijiji digitali cha Ololosokwan kwa serikali wilayani Ngorongoro mkoani Arusha. Wengine katika picha ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mh. Mrisho Gambo (kushoto), Naibu Katibu Mkuu Elimu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Bi. Avemaria Semakafu (kulia aliyeketi) pamoja na Mwakilishi wa Mkurugenzi wa UNESCO kanda ya Afrika Mashariki, Bw. Abdul Rahman Lamin (wa pili kulia).
 Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mh. Mrisho Gambo akipata huduma ya matibabu kutoka kwa Mtaalamu wa Magonjwa ya Kinywa wa Zahanati ya Ololosokwan, Dkt. Godson Mbise wakati Mh. Gambo alipotembelea zahanati hiyo pamoja na mambo mengine kuangalia ufanisi wake ambapo ziara hiyo iliyoambatana na hafla fupi ya Unesco kukabidhi kijiji digitali cha Ololosokwan kwa serikali wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.
 Mkurugenzi wa Tehama MUHAS na Mratibu wa Huduma ya Tiba Mtandao, Dkt. Felix Sukums (aliyeipa mgongo kamera) akibadilishana mawazo na Mganga Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Dkt. Emmanuel Mallange (wa pili kushoto), Mwakilishi wa Mkurugenzi wa UNESCO kanda ya Afrika Mashariki, Bw. Abdul Rahman Lamin (wa pili kulia) pamoja na Kaimu Katibu Mkuu wa Tume ya Taifa wa UNESCO nchini Tanzania, Dkt. Moshi Kimizi (kulia) nje ya jengo la huduma ya kinywa katika zahanati ya Ololosokwan wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.
 Mkurugenzi wa Tehama MUHAS na Mratibu wa huduma ya tiba mtandao, Dkt. Felix Sukums (kulia) akibainisha changamoto zinazoikabili kitengo cha ‘Ultra Sound’ katika Zahanati ya Ololosokwan kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mh. Mrisho Gambo (wa pili kushoto) wakati wa ziara fupi ya kutembelea kituo hicho cha afya  cha kijiji cha digitali na kuangalia ufanisi wake ambapo ziara hiyo iliambatana na hafla ya Unesco kukabidhi kijiji digitali cha Ololosokwan kwa serikali wilayani Ngorongoro mkoani Arusha. Wengine ni Kaimu Katibu Mkuu wa Tume ya Taifa wa UNESCO nchini Tanzania, Dkt. Moshi Kimizi, Mwakilishi wa Mkurugenzi wa UNESCO kanda ya Afrika Mashariki ofisi ya Nairobi, Bw. Abdul Rahman Lamin pamoja na Mganga Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Dkt. Emmanuel Mallange (wa pili kushoto).
 Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mh. Mrisho Gambo (wa tatu kushoto), Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Mh. Rashid Mfaume Taka (wa pili kushoto), Diwani wa kata ya Ololosokwan, Mh. Yannick Ndoinyo (kushoto), pamoja na Naibu Katibu Mkuu Elimu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Bi. Avemaria Semakafu (kulia) na ujumbe ulioambatana na Mh. Gambo wakikagua ujenzi wa nyumba za watumishi wa zahanati ya Ololosokwan zinazojengwa na wananchi wa Ololosokwan wakati wa ziara fupi ya kutembelea kituo hicho cha afya na kuangalia ufanisi wake iliyoambatana na hafla ya Unesco kukabidhi kijiji digitali cha Ololosokwan kwa serikali wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.
 Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mh. Mrisho Gambo (kushoto) akiwa ameambatana na Ofisa Programu Msaidizi wa Unesco, Hamidun Kweka mara baada ya kuwasili eneo la tukio wakielekea kukagua shule ya mtandao inayotumia umeme wa jua kabla ya kuelekea kwenye hafla ya Unesco kukabidhi kijiji digitali cha Ololosokwan kwa serikali wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.
 Mwakilishi wa Mkurugenzi wa UNESCO kanda ya Afrika Mashariki, Bw. Abdul Rahman Lamin (kulia) na Kaimu Katibu Mkuu wa Tume ya Taifa wa UNESCO nchini Tanzania, Dkt. Moshi Kimizi wakiwasili kwenye eneo la tukio la Unesco kukabidhi kijiji digitali cha Ololosokwan kwa serikali wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.
 Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Mh. Rashid Mfaume Taka (wa tatu kulia) akijadiliana jambo na Kaimu Mkuu wa Ofisi za Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Faith Shayo (kushoto) kuhusiana na protokali kabla ya kuanza hafla ya makabdhiano ya kijiji cha digitali cha Ololosokwan baina Serikali na Unesco wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.
 Mwanafunzi Rehema Lucas wa kidato cha nne wa Shule ya Sekondari Emanyata akitoa maelezo  kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mh. Mrisho Gambo na Mwakilishi wa Mkurugenzi wa UNESCO kanda ya Afrika Mashariki, Bw. Abdul Rahman Lamin (hawapo pichani) kuhusu program ya masomo mbalimbali ikiwemo  somo la Biology inayopatika ndani ya kompyuta mpakato (laptop) katika shule ya mtandao inayotumia umeme wa jua kabla ya kuelekea kwenye hafla ya Unesco kukabidhi kijiji cha digitali cha Ololosokwan kwa serikali wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.
 Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mh. Mrisho Gambo na Mwakilishi wa Mkurugenzi wa UNESCO kanda ya Afrika Mashariki, Bw. Abdul Rahman Lamin pamoja na wanafunzi wa shule ya sekondari Emanyata wanaonufaika na kijiji cha digitali cha shule ya mtandao inayotumia umeme wa jua wakimsikiliza Mwanafunzi Rehema Lucas (hayupo pichani) kabla ya kuelekea kwenye hafla ya Unesco kukabidhi kijiji cha digitali cha Ololosokwan kwa serikali wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.
 Ofisa Programu Msaidizi wa Unesco ambaye pia ni Mratibu wa kijiji cha digitali, Hamidun Kweka akifafanua jambo kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mh. Mrisho Gambo na Mwakilishi wa Mkurugenzi wa UNESCO kanda ya Afrika Mashariki, Bw. Abdul Rahman Lamin kuhusiana na kijiji cha digitali cha shule ya mtandao inayotumia umeme wa jua kabla ya kuelekea kwenye hafla ya Unesco kukabidhi kijiji cha digitali cha Ololosokwan kwa serikali wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.
 Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mh. Mrisho Gambo na Mwakilishi wa Mkurugenzi wa UNESCO kanda ya Afrika Mashariki, Bw. Abdul Rahman Lamin wakitoka ndani ya kijiji cha digitali cha shule ya mtandao inayotumia umeme wa jua kuelekea kwenye hafla ya Unesco kukabidhi kijiji cha digitali cha Ololosokwan kwa serikali wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.
 Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mh. Mrisho Gambo na ujumbe wake wakipata maelezo kutoka kwa Ofisa Programu Msaidizi wa Unesco, Bw. Hamidun Kweka kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na jamii ya wamasai katika kituo cha mafunzo ya kazi za mikono na utamaduni cha jamii ya wamasai (Community Arts Space-CAS) kilichojengwa na Umoja wa Ulaya (EU) kwa ushirikiano wa Unesco kwenye kijiji cha Ololosokwan wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.
 Mwakilishi wa Mkurugenzi wa UNESCO kanda ya Afrika Mashariki, Bw. Abdul Rahman Lamin (kulia) akijaribu moja ya bidhaa za shanga zinazotengenezwa na wakinamama wa kimasai katika kituo cha mafunzo ya kazi za mikono na utamaduni cha jamii ya wamasai (Community Arts Space-CAS) kilichojengwa na Umoja wa Ulaya (EU) kwa ushirikiano wa Unesco kwenye kijiji cha Ololosokwan wilayani Ngorongoro mkoani Arusha huku Kaimu Mkuu wa Ofisi za Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Faith Shayo akionyesha moja ya bidhaa iliyotengenezwa kwa shanga na kuandikwa UNESCO.
 Kaimu Mkuu wa Ofisi za Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Faith Shayo akiteta jambo na Mwakilishi wa Mkurugenzi wa UNESCO kanda ya Afrika Mashariki, Bw. Abdul Rahman Lamin wakati wa hafla ya Unesco kukabidhi kijiji cha digitali cha Ololosokwan kwa serikali wilayani Ngorongoro mkoani Arusha. Wengine meza kuu kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya ya Ngorongoro, Emmanuel Sukums pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Mh. Rashid Mfaume Taka.
 Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mh. Mrisho Gambo akizungumza na wananachi wa kijiji cha Ololosokwan pamoja na wageni waalikwa (hawapo pichani) wakati wa hafla ya Unesco kukabidhi kijiji cha digitali cha Ololosokwan kwa serikali, wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.
 Mwakilishi wa Mkurugenzi wa UNESCO kanda ya Afrika Mashariki, Bw. Abdul Rahman Lamin akizungumza kwa niaba ya Ann Therese Ndong-Jatta wakati wa hafla ya Unesco kukabidhi kijiji cha digitali cha Ololosokwan kwa serikali iliyofanyika katika kijiji cha Ololosokwan, wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.
Naibu Katibu Mkuu Elimu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Bi. Avemaria Semakafu akitoa salamu za Wizara ya Elimu pamoja na za Mbunge wa Jimbo la Ngorongoro ambaye pia ni Naibu Waziri wa Kilimo,Ufugaji na Maendeleo ya Uvuvi, Mh. William Ole Nasha wakati wa hafla ya Unesco kukabidhi kijiji cha digitali cha Ololosokwan kwa serikali iliyofanyika katika kijiji cha Ololosokwan, wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.
 Mkurugenzi wa Tehama MUHAS na Mratibu wa huduma ya tiba mtandao, Dkt. Felix Sukums akitoa salamu za MUHAS wakati wa hafla ya Unesco kukabidhi kijiji cha digitali cha Ololosokwan kwa serikali iliyofanyika katika kijiji cha Ololosokwan, wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.
 Diwani wa kata ya Ololoskwan, Mh. Yannick Ndoinyo akitoa neno la shukran kwa niaba ya wananchi wake kwa mgeni rasmi na Unesco kwa ushiriki wao wakati wa hafla ya Unesco kukabidhi kijiji cha digitali cha Ololosokwan kwa serikali iliyofanyika katika kijiji cha Ololosokwan, wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.
 Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Abudl Rahman Lamin (wa tatu kushoto) akimwakilisha Ann Therese Ndong’ Jatta, Mkurugenzi wa UNESCO kanda ya Afrika Mashariki akimkabidhi rasmi ripoti ya mradi wa kijiji cha kidigitali (Unesco-Samsung Digital Village) kwa Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Mh. Rashid Mfaume Taka (wa tatu kulia) kwa ajili ya uendelezaji baada ya majaribio wakati wa hafla iliyofanyika katika kituo cha mafunzo ya kazi za mikono na utamaduni cha jamii ya wamasai (Community Arts Space-CAS) kilichojengwa na Umoja wa Ulaya (EU) kwa ushirikiano wa Unesco kwenye kijiji cha Ololosokwan wilayani Ngorongoro mkoani Arusha. Wengine wanaoshuhudia tukio hilo ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mh. Mrisho Gambo Naibu Katibu Mkuu Elimu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Bi. Avemaria Semakafu (waliosimama kwa nyuma), Kaimu Mkuu wa Ofisi za Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Faith Shayo (kushoto), Kaimu Katibu Mkuu wa Tume ya Taifa wa UNESCO nchini Tanzania, Dkt. Moshi Kimizi (wa pili kushoto), Diwani wa kata ya Ololosokwan, Mh. Yannick Ndoinyo (wa pili kulia) pamoja na Mwenyekiti wa Kitongoji cha Ololosokwan, John Pyando (kulia).
 Kikundi cha wakinamama wakimasai wakitoa burudani kwa wageni waalikwa wakati wa hafla ya Unesco kukabidhi kijiji cha digitali cha Ololosokwan kwa serikali iliyofanyika katika kijiji cha Ololosokwan, wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.
 Baadhi ya wanakijiji wa Ololosokwan waliohudhuria hafla ya Unesco kukabidhi kijiji cha digitali cha Ololosokwan kwa serikali iliyofanyika katika kijiji cha Ololosokwan, wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.
 Baadhi ya wazee wa kijiji cha Ololosokwan waliohudhuria hafla ya Unesco kukabidhi kijiji cha digitali cha Ololosokwan kwa serikali iliyofanyika katika kijiji cha Ololosokwan, wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.
 Mwakilishi wa Mkurugenzi wa UNESCO kanda ya Afrika Mashariki, Bw. Abdul Rahman Lamin akipokea zawadi ya Mbuzi kutoka kwa wakinamama wa kimasai wanaofanya shughuli zao katika kituo cha mafunzo ya kazi za mikono na utamaduni cha jamii ya wamasai (Community Arts Space-CAS) kilichojengwa na Umoja wa Ulaya (EU) kwa ushirikiano wa Unesco kwenye kijiji cha Ololosokwan wilayani Ngorongoro mkoani Arusha. Kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu wa Tume ya Taifa wa UNESCO nchini Tanzania, Dkt. Moshi Kimizi.
 Kaimu Mkuu wa Ofisi za Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Faith Shayo akipokea zawadi kutoka kwa Mwakilishi wa kikundi cha wakinamama wakimasai wanaofanya shuhghuli zao katika kituo cha mafunzo ya kazi za mikono na utamaduni cha jamii ya wamasai (Community Arts Space-CAS) kilichojengwa na Umoja wa Ulaya (EU) kwa ushirikiano wa Unesco kwenye kijiji cha Ololosokwan wilayani Ngorongoro mkoani Arusha. Kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu wa Tume ya Taifa wa UNESCO nchini Tanzania, Dkt. Moshi Kimizi.
Naibu Katibu Mkuu Elimu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Bi. Avemaria Semakafu akivalishwa zawadi ya hereni zilizotengenezwa na wakinama wa kimasai wanaojishughulisha katika kituo cha mafunzo ya kazi za mikono na utamaduni cha jamii ya wamasai (Community Arts Space-CAS) kilichojengwa na Umoja wa Ulaya (EU) kwa ushirikiano wa Unesco kwenye kijiji cha Ololosokwan wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.
Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mh. Mrisho Gambo katika picha ya pamoja na wananchi, viongozi wa serikali na mashirika ya Umoja wa Mataifa walioshiriki mara baada ya hafla ya Unesco kukabidhi kijiji cha digitali cha Ololosokwan kwa serikali iliyofanyika katika kijiji cha Ololosokwan, wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad