HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, 29 June 2018

WAZIRI LUKUVI KUONGOZA MKUTANO MKUU WA MWAKA WA SHELTER AFRIQUE - KENYA

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; William Lukuvi amekutana na viongozi wakuu wa  Kampuni ya kuwezesha upatikanaji  wa nyumba za bei nafuu – Shelter Afrique jijini Dar es Salaam.
Waziri Lukuvi alikutana na viongozi hao kwa kikao maalum ofisini kwake – Dar es Salaam. Viongozi hao ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo; Bwn. Femi Adowele na Katibu wake; Francesca Kakooza.
Aidha, Suala mahususi lililowakutanisha viongozi hao lilikuwa ni kuhusu maandalizi ya Mkutano Mkuu wa 37 wa Kampuni hiyo unaotegemewa kufanyika hivi karibuni nchini Kenya, ambapo Waziri Lukuvi ni Mwenyekiti wa Mkutano huo.
Kwa ujumla changamoto za nchi za kiafrika katika kuwapatia wananchi wa kawaida makazi nafuu zinafanana na kilio kikubwa katika nchi wanachama, ambazo ni  kuwepo makazi holela hata baada ya nchi hizo kujikomboa kutoka ukoloni mkongwe. 
Shelter Afrique imedhamiria kuweka juhudi katika kuipa kipaumbele sekta ya Nyumba kwa kuwa ni sekta mtambuka katika kuharakisha ukuaji wa uchumi na maisha bora ya watu.
Mambo mbalimbali katika sekta ya Nyumba yanatarajiwa kuzungumziwa katika Mkutano huo wa 37, hususan katika jitihada za kupatikana kwa makazi bora na nafuu katika nchi wanachama, ambapo changamoto Kuu imekuwa ni Rasilimali fedha.
Tanzania ni nchi mojawapo Mwanachama wa Shelter Afrique kati ya nchi 44 za barani Afrika .
Tanzania ilijiunga na Shelter Afrique mwaka 2003 na Mkutano wa 32  ambao ulifanyika N’djamena, Chad 2013, uliopitishwa na Azimio Namba GM/ 2013/005 la kuongeza Hisa kwa kila nchi mwanachama kwa lengo la kukuza mtaji wa Kampuni hiyo na kuiwezesha kuweka nguvu zaidi katika masuala ya uendelezaji nyumba barani Afrika. 
Mkutano wa mwaka huu wa 37, unategemewa kufanyika Nairobi, Julai 20, 2018.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad