Biashara ya dawa za kulevya zisipokomeshwa na kuachwa
ikaendelea nchini, athari zaidi ikiwemo
kuingiliwa kwa misingi ya kiutawala na wafanyabiashara wa dawa hizo kwa manufaa
yao wao wenyewe binafsi zitaendelea kujitokeza kwani dawa za kulevya limekuwa tatizo kubwa katika ulimwengu mkubwa
na hata katika nchi ya Tanzania.
Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu) Jenista Mhagama ameyasema hayo, wakati wa
kilele cha maadhimisho ya Kitaifa ya siku ya kupiga vita dawa za kulevya
duniani iliyokwenda kwa kaauli mbiu ‘Tujenge Maisha yetu, Jamii yetu na Utu
wetu bila Dawa za Kulevya’ iliyofanyika leo Mkoani Iringa.
Amesema matumizi na biashara ya dawa za kulevya yameendelea
kusababisha madhara makubwa sana katika nchi ya Tanzania yakiwemo ya kiafya,
madhara katika jamii inayotuzunguka, kiuchumi,
kimazingira, kisiasa na hata kiusalama.
Ameongeza kuwa matumizi ya dawa za kulevya ambayo kwa kiasi
kikubwa watumiaji wake ni vijana yanaathari kubwa na hatari ya kupoteza nguvu
kazi ya taifa letu hivyo, kwani wao ni tegemeo la taifa hasa katika kukuza
uchumi na kuleta maendeleo endelevu, .matuimizi ya dawa za kulevya yasipopigwa
vita na kuzuiliwa yataathiri uchumi wa nchi yetu, uzalishaji maadili, jamii na
usalama kwa ujumla wa taifa letu.
“Mapambano dhidi ya
dawa za kulevya ni vita kubwa inayohitaji nguvu ya pamoja kwani madhara yake ni
makubwa kwa jamii yetu hasa kwa vijana ambao ni nguvu kazi kwa taifa letu.., Ni
ukweli usiopingika kuwa maendeleo ya usatawi wa taifa duniani na hata katika nchi yetu yanategemea
sana nguvu kazi na hasa nguvu kazi ya
vijana”, amesema Mhagama.
Pia amesema, mabinti wengi ambao wako katika umri wa,
kusaidia kuongeza nguvu kazi katika nchi yetu wanakatishwa ndoto zao kwa
kutumia dawa hizi na hata kupata madhara yanawasababishia matatizo mbali mbali
jambo ambalo ni la kusikitisha sana
“Ni matarijio yangu kupitia maadhimisho haya ya siku ya leo
wananchi wa mkoa wa Iringa, watakumbushwa na kuhamasishwa kushirikiana na
serikali katika kupambana na vita hii kwani watumiaji wa dawa za kulevya ni
watanzania wenzetu, tunaishi nao kila siku, ni vijana wetu tuliowazaa ni watoto
wetu, hivyo ni wakati muafaka kwa kila mmoja wetu kusoma sheria kuhusu uuzaji
utumiaji wa dawa za kulevya sambamba na ufahahamu wa athari za dawa hizo hapa
nchini.
Amesema, kwa mujibu wa utafiti wa nguvu kazi wa mwaka 2014
inaonesha kuwa, nguvu kazi ya vijana wenye umri kati ya miaka 15 and 35 ni
takribani watanzania milioni 12.5 ambao
ni sawa na asilimia 56 ya nguvu kazi yote ya nchi yetu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu) Mh. Jenista Mhagama akizungumza na wananchi wa mkoa wa Iringa wakati wa maadhimisho ya kitaifa ya siku ya kupambana na dawa za kulevya Duniani yaliyofanyika katika kiwanja cha Kichangani mkoani Iringa leo.
No comments:
Post a Comment