HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, 26 June 2018

MEDDIE KAGERE ATUA SIMBA KWA DAU LA MILIONI 120

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Mabingwa wa ligi kuu Tanzania BaraKlabu ya Simba imefanikiwa kunasa saini ya mshambuliaji wa Gor Mahia FC Meddie Kagere kwa donge nono kuja kuwatumikia wanamsimbazi hao kwa kandarasi ya miaka miwili.

Simba wamewapiku mahasimu wao wakubwa Yanga ambao walionesha nia ya kumtaka kabla ya kuzidiwa kete na wanamsimbazi hao.

Kagere aliyetua jana nchini akiambatana na wakala wake amesaini donge nono la Dola 603,000 sawa na milioni 120 na mshahara wa dola 4,500 sawa na Milion tisa kwa mwezi.

Mshambuliaji huyo wa kutumainiwa katika klabu ya Gor Mahia mwenye asili ya Rwanda ataanza kutumikia klabu ya Simba baada ya kumalizika kwa mashindano ya Kombe la Shirikisho hatua ya makundi ambapo wapo kundi moja na Yanga.

Kagere alikua moto wa kuotea mbali katika mashindano ya Sportpesa yaliyofanyika mwaka huu nchini Kenya akiwafunga Simba katika mchezo wa fainali.

Baada ya usajili huo Simba imeonyesha kulipa kisasi kwa Yanga wakikumbuka msimu wa 2012 na 2013 wakiwapita njia za mkato na kuwasajili Haruna Niyonzima na Mbuyu Twite ambapo kwa sasa Simba wamewasha moto wakionekana wamedharia kuunda kikosi bora kwa msiku wa 2018/19.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad