BIA YA KILIMANJARO YAFANIKISHA NDOTO ZA WATANZANIA 10 KUONA MECHI ZA KOMBE LA DUNIA 2018, URUSI - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, 17 June 2018

BIA YA KILIMANJARO YAFANIKISHA NDOTO ZA WATANZANIA 10 KUONA MECHI ZA KOMBE LA DUNIA 2018, URUSI

Meneja wa Mawasiliano ya Wateja wa TBL, David Tarimo,(kushoto) akiwapa maelekezo baadhi ya washindi wa safari ya Urusi wakati wa hafla ya uzinduzi wa kuangalia mechi za kombe la Dunia iliyofanyika jijini Dar es Salaam.  Ili kushiriki kinachotakiwa ni kununua bia ya Kilimanjaro na kushiriki mara 6 kutuma namba iliyopo chini ya kizibo kwenda namba 15451 na droo ifafanyika kila wiki kwa kipindi cha wiki kumi.
Baadhi ya washindi wakiwa na Meneja wa Mawasiliano ya wateja wa TBL,David Tarimo (wa pili kutoka kushoto).
Shamrashamra za hafla ya uzinduzi wa kuangalia mechi za kombe la Dunia jijini Dar es Salaam
Baadhi ya wafanyakazi wa TBL katika hafla hiyo

*Wengine waendelea kujishindia fedha taslimu shilingi milioni moja

Wakati mashindano ya soka ya kombe la dunia 2018 la FIFA, yameanza ,bia rasmi ya kwanza ya Tanzania katika mashindano hayo ya Kilimanjaro Lager, kupitia promosheni yake inayoendelea imefanikisha ndoto za watanzania 10 kwenda nchini Urusi kushuhudia mechi za mashindano hayo makubwa ya soka dumiani mubashara.

Washindi kupitia promosheni ya bia ya Kilimanjaro ya Kombe la Dunia, iliyozinduliwa mapema mwezi uliopita wako katika maandalizi ya safari kwenda Urusi mapema mwanzoni mwa wiki ijayo.

Baadhi ya washindi walipohojiwa jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki kuhusiana na safari hiyo walisema kwa furaha kuwa mwanzoni walikuwa hawaamini baada ya kupewa taarifa za ushindi wa droo za promosheni hiyo lakini hivi sasa baada ya kukabidhiwa tiketi zao wameamini safari ipo.

Charles John, mmoja wa washindi hao kutoka mkoani Geita,ameeleza kuwa anajisikia furaha kupata fursa kama hii ambayo alikuwa haitegemei,ameishukuru kampuni ya TBL kwa kuandaa promosheni kubwa kama hii ambayo imefanikisha ndoto za wateja wake kuona mechi za kombe la Dunia Live.

Mshindi mwingine, Leodgard Isaac,alisema kupata nafasi hii ni moja ya jambo ambalo limeleta furaha maishani mwake na kuongeza kuwa mbali na kuona mechi za kombe la Dunia Live pia anafurahi kuona kinywaji kutoka Tanzania cha bia ya Kilimanjaro, kimetumika kuitangaza Tanzania katika mashindano haya makubwa ya mchezo wa soka duniani.

Naye Kaijage Kironde, mkazi wa Dar es Salaam,alisema ni mpenzi wa mchezo wa soka kwa miaka mingi,na amefurahi kupata nafasi ya kushuhudia mchezo wa kombe la dunia mwaka huu nchini Urusi kupitia promosheni ya bia ya Kilimanjaro.

Meneja wa Mawasiliano ya Wateja wa TBL, David Tarimo, alisema,promosheni inaendelea kwa washindi wa fedha taslimu milioni moja kila wiki na muda wa maongezi inaendelea na katika droo iliyofanyika mwishoni mwa wiki washindi 4 wamejishindia fedha, “Lengo kubwa la promosheni hii ni kuwazawadia wateja wetu ili waburudike katika msimu huu wa shamrashamra za kombe la dunia la FIFA 2018”, alisisitiza.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad