HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, May 22, 2018

WIZARA YA AFYA YAWAONYA WANATOA HUDUMA ZA KIMAABARA BILA VIBALI

Na Agness Francis, Globu ya Jamii
WIZARA ya Afya,Maendeleo ya Jami, Jinsia, Wazee na Watoto imewataka watoa huduma za kimaabara kwa wananchi kuhakikisha wanakuwa na vibali kwani kinyume na hapo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao kwa mujibu wa wa sheria.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo , Mkurugenzi Msaidizi Huduma ya uchunguzi na magonjwa Dk. Charles Massambu amesisitiza sheria itachukua mkondo wake kwa wale wanaohudumia wananchi shughuli za kimaabara bila lakini hawana vibali au kusajiliwa.

"Hakuna mtoa huduma atakaetoa huduma za maabara bila kusajiliwa.Tukibaini tutachukua hatua za kisheria," amesema Dk. Massambu.

Aidha Massambu ameeleza baraza linatambua uwezo na utaalamu katika kuelimisha jamii ya watanzania kuhusu majukumu katika kuwahudumia.Pia kutokana na changamoto za majibu ya vipimo kutofautiana kutoka sehemu moja hadi nyingine Wizara imechukua hatua ya uhakiki wa ubora wa vipimo.

"Tanzania kuna maabara 33 ambazo ni nyota moja mpaka nne,nyingine nane zilizo na hadhi ya kimataifa ambapo vipimo vyake huwa ni sawa na vya nchi nyingine za nje.

"Pia vigezo vya maabara hizo katika ngazi ya taifa na kanda vibali vimetolewa na Shirika la Afya Duniani ambapo waliamua kutoa nyota za viwango vya ubora hatua kwa hatua,"amefafanua.

Amewaomba waandishi wa habari kusaidia kutoa taarifa kuhusu huduma mbalimbali za kimaabara ili kuwasaidia wananchi kujua ni sehemu gani wanayoweza kupata matibabu sahihi zilizo na vibali.

Kwa upande wa Msajili wa Baraza la Wataalamu na maabara Theophil Malibiche amesema kisheria zipo gharama kidogo zinazoendana na usajili wa wataalamu wa maabara ambazo zimegawanyika katika usajili wa awali na wa kudumu kwa kiwango tofauti cha elimu ada ya kila ambayo kila mwaka.
 Mkurugenzi msaidizi wa huduma za uchunguzi wa Magonjwa Dkt Charles G Massambu akizungumza na waandishi wa habari leo katika ofisi zao Jijini Dar es Salaam akiwataka watoa huduma ya maabara wasio na vibali kutoka baraza la wataalamu la maabara  kujisajili au kuacha kufanya kazi hiyo.
 Msajili wa Baraza la wataalamu wa maabara akizungumza na waandishi wa habari leo katika ofisi zao Jijini Dar es Salaam akielezea kuhusu umuhimu wa kusajili huduma hizo.(Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad