HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 22 May 2018

KAMPENI YA MWAKA YA BENKI YA EXIM YAFIKA HOSPITALI YA SEKOU TOURE MWANZA

 Mkuu wa kitengo cha Rasilimali watu wa Benki ya Exim Fredrick Kanga, akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi vitanda arobaini na magodoro yake kwa  Hospitali Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekou Toure, kushoto ni  Mganga Mkuu wa Mkoa huo Rutachunzibwa Thoma na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella. 
 Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella(aliyevaa kofia) akipokea vita nda  arobaini na magodoro yake kutoka kwa Mkuu wa kitengo cha Rasilimali watu wa Benki ya Exim Fredrick Kanga, wakati wa hafla ya makabidhiano iliyofanyika kwenye Hospitali Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekou Toure, kushoto ni Mganga Mkuu wa Mkoa huo Rutachunzibwa Thoma.
 Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella, akiwashukuru na kuzungumza na wauguzi wa  Hospitali Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekou Toure, wakati wa kukabidhi vitanda arobaini na magodoro yake kwa hospitali hiyo yaliyotolewa na Benki ya Exim.
 Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Rutachunzibwa Thoma, akizungumza wakati wa kupokea vitanda arobaini na magodoro yake yaliyotolewa na Benki ya Exim kwa ajili ya Hospitali Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekou Toure, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella, Mkuu wa kitengo cha Rasilimali watu wa Benki ya Exim Fredrick Kanga na Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Benki hiyo Stanley Kafu(kulia). 
 Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella, akisalimiana na wauguzi wa  Hospitali Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekou Toure, wakati wa kukabidhi vitanda arobaini na magodoro yake kwa hospitali hiyo yaliyotolewa na Benki ya Exim.

BENKI ya Exim Tanzania leo imekabidhi vitandana magodoro 40 kwa Hospitali ya SekouToure ya mkoani Mwanza. 

Benki ya Exim Tanzania iliadhimisha miaka 20 ya huduma, mwezi wa Agosti mwaka jana, kwa kuzindua mradi wa  mwaka mzima unaoitwa “miaka 20 ya kujalijamii” ambao Benki hiyo itawekeza katika sekta ya afya Tanzania hasa kwenye kuboresha huduma za afya zinazotole wa kwa wakina mama na wanawake. 

Katika kukabiliana na uhaba huu unaosumbua taifa, benkiya Exim Tanzania, yenye uwepo wa kimataifa imeanzisha mradi unaolenga kusaidia upungufu wa vitanda katika wodi za wazazi kwenye hospitali nchini.

Hivyo benki ya Exim itatoa magodoro na vitanda 500 katika hospitali za serikali katika mikoa 13 nchini kamasehemu ya kampeni yake ya mwaka yenye lengo la kushirikiana na jamii.

 Mkuu wa mkoa wa Mwanza, JohnMongella alipongeza Exim Bank Tanzania kwa msaada wake na kuhimiza taasisi mbalimbali kutekeleza ishara ya Benkiya Exim Tanzania katika kusaidia kuboresha huduma ya afya hapa nchi.

Akizungumza katika hafla hiyo ya makabidhiano, Mkuu wa idara ya rasilimali watu wa benki ya Exim, Bwana Frederick Kanga amesema, “Benki imetambua umuhimu wajumuiya zinazozunguka eneo la biashara yetu na ndio maana shughuli za kijamiini muhimu sana kwa Benkiya Exim. Tuna amini kwamba tuna sehemu kubwa katika kufanya mabadiliko mazuri katika sekta mbalimbali katika jamii zetu. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad