HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 22 May 2018

UN WATOA ELIMU YA MALENGO YA DUNIA KWA WATU WENYE ULEMAVU

Na Ripota Wetu, Globu ya jamii
SHIRIKA la Umoja wa Mataifa (UN) kwa kushirikiana na Shirika la Seed Trust wameanzisha timu ya vijana 20 wenye ulemavu wa aina mbalimbali kutoka vyuo sita vya elimu ya juu nchini.

Lengo la timu hiyo ni kufanya ushawishi na utetezi kwa wanafunzi wenye ulemavu ili kuwajengea uwezo wa kusaidia maendeleo endelevu ya kidunia.

Taarifa iliyotolewa leo kwa vyombo vya habari inaelezea kupitia mafunzo hayo ambayo yameshirikisha wanavyuo walemavu kutoka vyuo vikuu mbalimbali hapa nchini yanatoa nafasi ya kundi la watu wenye ulemavu kushirikishwa katika utekelezaji wa mwaka wa pili wa elimu ya malengo endelevu ya dunia yanayosema hakuna binadamu yeyote atakaye achwa nyuma.

Pia katika mafunzo hayo Umoja wa Mataifa umetoa machapisho maalum takribani 1000 yaliyoandikwa kwa lugha ya alama yatakayowezesha watu wenye ulemavu wa macho kusoma na kuelewa mipango ya maendeleo endelevu ya kidunia.

Hivyo katika kutekeleza malengo hayo vijana hao watafundishwa pamoja na kuzunguka kuhamasisha malengo hayo kwa walemavu wengine katika vipaumbele mbalimbali ikiwemo elimu na afya katika maeneo mbalimbali hapa nchini.
 Mkuu wa mawasiliano kutoka Umoja wa Mataifa Hoyce Temu akiongea na waandishi wa habari na kufafanua baadhi ya mambo  baada ya kikao cha mafunzo kwa vijana  20 wenye ulemavu uliofanyika mkoani  Morogoro.
 Mkurugenzi mtendaji wa shirika la Seed Trust Magreth Nkanga, ambaye pia ni mbunge mstaafu aliyekuwa akiwakilisha kundi la walemavu akishukuru un kwa kutoa machapisho maalum takribani 1000 yaliyoandikwa kwa lugha ya alama, yakihusu mkakati ya elimu ya malengo endelevu ya dunia.
 Kijana mwenye ulemavu wa macho Godbless Muro, mwanafunzi wa Shahada ya sayansi ya siasa na utawala, Chuo kikuu cha Dodoma akisoma moja ya chapisho iliyoandikwa kwa maandishi ya nundunundu yenye ujumbe wa maendeleo endelevu ya kidunia.
 Vijana mbalimbali wenye ulemavu sambamba na waandishi wa habari wakisikiliza kwa makini wakati wakikao cha utoaji elimu ya malengo endelevu ya dunia kilichofanyika mkoani Morogoro.
Mwenyekiti wa bodi ya shirika la Seed Trust kushoto Steven Mashishanga akimkabidhi katibu tawala msaidizi, mkoa wa Morogoro Ernest Mkongo moja ya chapisho maalumu kwa watu wenye ulemavu la mpango wa elimu ya maeneleo ya dunia, katikati Mkuu wa mawasiliano kutoka Umoja wa Mataifa Hoyce Temu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad