HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Friday, 4 May 2018

Uhuru wa habari sio kuiangalia tu serikali - Mwakyembe

Na Mwandishi wetu
VYOMBO vya habari nchini vimekumbushwa kwamba uhuru wa habari sio kuiangalia tu serikali, bali kujiangalia  wenyewe na pia vyombo vyao vya habari.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe wakati akihutubia hadhira ya waandishi wa habari katika kilele cha sherehe za maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari duniani, sherehe zilizofanyika kitaifa katika hoteli ya Morena Jijini Dodoma.
Katika hotuba yake baada ya kusikiliza hoja kadha kutoka taasisi mbalimbali kuhusiana na uhuru wa vyombo vya habari nchini na hisia kwamba vinaminywa Waziri huyo alisema kwamba ipo haja ya tasnia kujiangalia yenyewe kama inatenda haki na weledi kwa taifa hili.
“Kalamu ya mwanahabari ina nguvu sana, ina nguvu sawa na ya silaha, ikitumiwa vizuri ni mlinzi na ikitumiwa vibaya ni maafa” alisema Dk. Mwakyembe
Alisema katika mazingira ya sasa ambako kuna walimu wengi kuna baadhi ya watu wanapiga kelele kuhusu kufuatwa kwa sheria wakisema sio demokrasia, huku wakifahamu fika kwamba hata katika nchi zao hicho wanachoimba demokrasia hakipo.
Akihutubia kama mgeni rasmi alisema kwamba ingawa dirisha lipo wazi kwa majadiliano, serikali haitarudi nyuma kutokana na haja mahsusi ya udhibiti wa yanayoendelea katika mitandao kwa manufaa ya taifa hili leo na kesho.
 “Kuhusu Kanuni za Maudhui Mtandaoni, hili tunaweza kukaa na kujadili lakini kama Serikali hatutarudi nyuma katika hili.
 “Kupitia mtandao, bila kuweka udhibiti kuna mambo mengi yanapita ambayo hatuwezi kukubaliana nayo”  alisema Dk Mwakyembe.
Akiwasilisha salamu za Jukwaa la wahariri nchini TEF, Kaimu Mwenyekiti Deodatus Balile alisema kwamba ipo haja ya kuendesha mdahalo wa kitaifa kuhusu mustakabali wa uhuru wa habari nchini Tanzania ambao hatima yake ni amani na maridhiano.
Alisema haja ya mdahalo huo unatokana na kuwapo kwa matukio mfulululizo dhidi ya wanahabari iwe Dar es salaam, Dodoma, Iringa na Mbeya yanayoonesha kuwapo na viashiria ambavyo havina afya kwa uhuru wa habari.
Pia alisema hata hatua zinazochukuliwa na TCRA ni hatua ambazo zinakatisha tamaa na kuingiza woga katika utendaji wa shughuli za vyombo vya habari.

Wazungumzaji wengi katika siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari, walizungumzia haja ya kukaa na kuzungumza kuhusiana na sheria za vyombo vya habari na kuona nia njema ya serikali katika kutengeneza uwajibikaji kwa sekta hiyo muhimu kwa maendeleo ya nchi.
Makamu mwenyekiti wa UTPC (Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa Habari) Jane Mihanji yeye aliitafadhalisha kutimiza wajibu wake kwa kupanua wigo wa habari.
Alitaka waandishi kujengewa mazingira bora ya kufanyakazi ili waweze kutekeleza wajibu wao  kwa manufaa ya taifa.
Ofisa Programu wa Baraza Huru la Habari nchini (MCT) Paul Mallimbo aliwataka wananchi, wadau wa habari na serikali yenyewe kuangalia upya sheria katili ambazo zinadumaza uhuru wa vyombo vya habari na wanahabari wenyewe na kuwafanya kufanyakazi kwa woga.
Alisema kuna sheria nyingi zinazominya uhuru wa habari na kutaka zirekebishwe ili kuhakikisha kuwapo kwa uhuru ambao pia unazungumzwa katika katiba na kwenye haki za binadamu ambapo nchi imetia saini.
Pamoja na wazungumzaji wawakilishi kutoka kwa wadau mbalimbali wa tasnia ya habari pia wakubwa wa mashirika ya kimataifa nayo yalikuwepo kuelezea hisia zao kuhusiana na uhuru wa vyombo vya habari na nini kifanyike.
Naye Mwenyekiti wa MOAT, Dk Reginald Mengi  ameitaka serikali kuendelea kusaidia uhai wa vyombo vya habari kwa kuvipa matangazo kutoka serikalini kwenyewe na kwenye taasisi zake.
Katika hotuba yake iliyosomwa na Katibu wa MOAT, Henry Muhanika alisema ipo haja ya kutolewa kwa fursa sawa za matangazo kwa vyombo vya habari kwa kuwa vyote vinachangia maendeleo ya nchi na vinahitaji navyo kujiendesha.
Pia alitaka kuangaliwa kwa vipengele tata vya sheria ambavyo vinakatili uhuru wa habari ili kuwezesha tasnia kusonga mbele na majukumu yake ya kusaidia serikali kuchochea maendeleo.
Katika siku hiyo ya habari pia maveterani wakiwakilishwa na Kiondo Mshana walizungumza kuhusu tasnia ya habari wakitaka waandishi kutokuwa waoga na kutekeleza wajibu wao kwa weledi.
Aidha alisema kwamba ni vyema waandishi wakawaibua watu hao wasiojulikana kwa kuwa ni kazi yao kufanya hivyo kwani wakati mwingine watu hao wasiojulikana nia yao ni kuchonganisha serikali na wananchi wake kwa kukaa katikati na kufanya ujambazi.
Aidha aliwakumbusha haja ya kuagana na nyonga wakitaka kuruka ili shughuli wanazofanya ziwe makini na za uhakika. Pia alikemea uhusiano wa paka na panya kati ya serikali na waandishi akisema hiyo haileti afya.

Naye MKurugenzi wa TAMW, Edda Sanga akitaka umakini katika ustawi wa jamii kwa kupiga vita ukatili kwa watoto.
Nayo Wakfu wa Vyombo vya Habari Tanzania (TMF) imesema serikali ina wajibu mkubwa wa kuhakikisha haki inatendeka na kunakuwapo na utawala wa sheria.
Akizungumzia mafanikio katika siku ya kuadhimisha Uhuru wa Vyombo vya Habari duniani, Mkurugenzi wa Mpito wa TMF Fausta Musokwa alisema vyombo vya habari na waandishi wa habari wana nafasi ya kipekee katika kuchochea maendeleo ya nchi.
Alisema vyombo hivyo vinavina nafasi ya kuwajibisha watu wote nchini ili malengo ya maendeleo yaliyowekwa kama nchi yanafikiwa kwa kufanya kazi yao kwa weledi, maadili na umakini, bila uoga.
Alisema kazi ya sekta ya habari ni kutafuta na kuchambua taarifa ili kutengeneza na kutoa habari kwani upatikanaji wa habari sahihi kwa wakati ni daraja la maendeleo.
Naye Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya Friedrich Ebert Stiftung Tanzania, Andreas Quasten alitaka waandishi wa habari kujengewa uwezo katika kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao ya kila siku. 
Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA-TAN), Salome Kitomari aliitaka serikali kuhakikisha kwamba haki za waandishi wa habari hasa zile zinazohusiana na usalama wao zinazingatiwa.
“Tunaitaka Serikali kupitia jeshi la PolisiTanzania kuwatafuta waliohusika na kupotea kwa Mwanahabari AzoryGwanda na kuwachukulia hatua stahiki” alisema Salome Kitomari.
 Mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe akizungumza na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa Unesco ambaye pia ni Mshauri wa Masuala ya Mawasiliano Kanda ya Afrika Mashariki ofisi ya Unesco Nairobi, Jaco Du Toit (kulia) mara baada ya kuwasili kwenye kilele cha sherehe za maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yaliyofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma. Wengine ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA-TAN), Salome Kitomari (katikati), Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Edda Sanga (wa pili kulia) pamoja na Afisa Utawala Msaidizi na Itifaki wa ofisi za Unesco Dar es Salaam, Rahma Islem (kushoto).
 Mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe akisalimiana na Naibu Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU), Charles Stuart mara baada ya kuwasili kwenye kilele cha sherehe za maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yaliyofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma. Wengine katika picha ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA-TAN), Salome Kitomari (wa kwanza kushoto), Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Habari Unesco nchini, Nancy Kaizilege ( wa tatu kushoto), Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya Friedrich Ebert Stiftung Tanzania, Andreas (wa pili kulia) pamoja na Meneja Programu wa Tanzania Media Fund (TMF), Razia Mwawanga (kulia)
 Mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe akisalimiana na Meneja Programu wa Tanzania Media Fund (TMF), Razia Mwawanga mara baada ya kuwasili kwenye kilele cha sherehe za maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yaliyofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.
 Mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe akipata maelezo kutoka kwa Afisa Programu wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Paul Mallimbo (katikati) kuhusu ripoti ya uvamizi wa kituo cha habari cha CLOUDS wakati alipotembelea mabanda ya maonyesho kwenye kilele cha sherehe za maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yaliyofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.
 Mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe akipata maelezo kutoka kwa Ofisa wa Tehama na Programu za Vyombo vya Habari wa TMF, Baraka Kiranga (kushoto) kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na taasisi hiyo wakati alipotembelea mabanda ya maonyesho kwenye kilele cha sherehe za maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yaliyofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma. Wengine ni Mwandishi wa kujitegemea Adelina Johnbosco (katikati) pamoja na Mtayarishaji bora wa makala na vipindi vya TV kuhusu utalii na uhifadhi, Anwary Msechu (kulia).
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe akimpongeza Mtayarishaji bora wa makala na vipindi vya TV kuhusu Utalii na Uhifadhi, Anwary Msechu ambaye alishinda tuzo mbili za Sinema Zetu International Film Festival (SZIFF) katika kipengele cha mwandaaji bora wa makala na makala bora iliyohusu malipo duni ya kwa wapagazi Mlima Kilimanjaro wakati alipotembelea mabanda ya maonyesho kwenye kilele cha sherehe za maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yaliyofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.
 Mratibu wa Miradi wa Taasisi ya Friedrich Ebert Stiftung, Amon Petro akitoa maelezo kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe kuhusu malengo ya taasisi hiyo ambayo ni Kukuza Demokrasia, Utawala Bora na Haki Jamii ambapo alieleza ili kufikia malengo hayo wanafanyakazi na asasi mbalimbali za kiraia, vyama vya siasa na vyama vya wafanyakazi pamoja na waandishi wa habari wakati alipotembelea mabanda ya maonyesho kwenye kilele cha sherehe za maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yaliyofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.
 Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Mkuu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu nchini (THRDC), Onesmo Ole Ngurumwa, Mwandishi wa kujitegemea Adelina Johnbosco,  Mdau wa tasnia ya Habari na Afisa Mawasiliano wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Innocent Mungy pamoja na Mtayarishaji bora wa makala na vipindi vya TV kuhusu Utalii na Uhifadhi, Anwary Msechu ambaye alishinda tuzo mbili za Sinema Zetu International Film Festival (SZIFF) katika kipengele cha mwandaaji bora wa makala na makala bora iliyohusu malipo duni ya kwa wapagazi Mlima Kilimanjaro wakiwa kwenye picha ya pamoja banda la maonyesho la TMF wakati wa kilele cha sherehe za maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yaliyofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.
 Mshehereshaji wa kilele cha sherehe za maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari, Neville Meena akitambulisha meza kuu katika maadhimisho hayo yaliyofanyika kwenye Hoteli ya Morena jijini Dodoma.
 Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Edda Sanga, Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa Unesco ambaye pia ni Mshauri wa Masuala ya Mawasiliano Kanda ya Afrika Mashariki ofisi ya Unesco Nairobi, Jaco Du Toit, Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA-TAN), Salome Kitomari, Mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe pamoja na Naibu Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU), Charles Stuart wakati wa kilele cha sherehe za maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yaliyofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.
 Mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe akizungumza kwenye kilele cha sherehe za maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yaliyofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA-TAN), Salome Kitomari akitoa salamu za MISA-TAN wakati wa kilele cha sherehe za maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yaliyofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.
 Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa Unesco ambaye pia ni Mshauri wa Masuala ya Mawasiliano Kanda ya Afrika Mashariki ofisi ya Unesco Nairobi, Jaco Du Toit, akitoa salamu za Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Audrey Azoulay wakati wa kilele cha sherehe za maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yaliyofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.
  Afisa Programu wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Paul Mallimbo akitoa salamu za Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Kajubi Mukajanga wakati wa kilele cha sherehe za maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yaliyofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.
 Katibu wa Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari nchini (MOAT), Henry Muhanika akitoa salamu kwa niaba ya Mwenyekiti wa MOAT, Dk. Reginald Mengi wakati wa kilele cha sherehe za maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yaliyofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Wakfu wa Vyombo vya Habari Tanzania (TMF), Fausta Musokwa akitoa salamu za TMF wakati wa kilele cha sherehe za maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yaliyofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.
 Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya Friedrich Ebert Stiftung, Andreas Quasten akizungumza wakati wa kilele cha sherehe za maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yaliyofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.
 Kaimu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF), Deodatus Balile akitoa salamu za TEF wakati wa kilele cha sherehe za maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yaliyofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.
Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa Habari nchini (UTPC), Jane Mihanji akitoa salamu za UTPC wakati wa kilele cha sherehe za maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yaliyofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.
 Mwakilishi waandishi wa habari wakongwe (Veterans), Kiondo Mshana akitoa salamu za Ma-Veterans ambapo alisema amani tuliyonayo inadumu kutokana na weledi wa uandishi wa habari nchini wakati wa kilele cha sherehe za maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yaliyofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.
 Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Edda Sanga akitoa salamu za taasisi hiyo wakati wa kilele cha sherehe za maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yaliyofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.
 Naibu Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU), Charles Stuart akitoa salamu za Umoja huo wakati wa kilele cha sherehe za maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yaliyofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.
 Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa Unesco ambaye pia ni Mshauri wa Masuala ya Mawasiliano Kanda ya Afrika Mashariki ofisi ya Unesco Nairobi, Jaco Du Toit akichambua ripoti  inayohusu uhuru wa kujieleza na maendeleo ya vyombo vya habari kabla ya kuikabidhi kwa Mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe wakati wa kilele cha sherehe za maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yaliyofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.
 Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa Unesco ambaye pia ni Mshauri wa Masuala ya Mawasiliano Kanda ya Afrika Mashariki ofisi ya Unesco Nairobi, Jaco Du Toit akimkabidhi Mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe nakala ya ripoti inayohusu uhuru wa kujieleza na maendeleo ya vyombo vya habari wakati wa kilele cha sherehe za maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yaliyofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma. Katikati anayeshuhudia tukio hilo ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA-TAN), Salome Kitomari.
 Mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe akizundua Ripoti ya tathimini ya Hali ya Habari Tanzania 2017 - So This is Democracy? Iliyoandaliwa na MISA-TAN wakati wa kilele cha sherehe za maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yaliyofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma. Wanaoshuhudia tukio hilo Kulia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA-TAN), Salome Kitomari, Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA-TAN), Gasirigwa Sengiyumva (wa pili kushoto) pamoja na Afisa Mawasiliano Msaidizi wa MISA-TAN, Fredy Njeje (kushoto aliyeketi).
 Mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe akisalimiana na Mtaalamu wa Masuala ya Vyombo vya Habari na Mkufunzi wa Kujitegemea, Rose Haji Mwalimu wakati wa kilele cha sherehe za maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yaliyofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.
 Mkuu wa wilaya ya Kongwa na Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Deogratius Ndejembi akizungumza na washiriki wakati akifunga kilele cha sherehe za maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yaliyofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.
 Mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe na meza kuu wakiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa habari wakongwe (Veterans) mara baada ya kuhutubia kilele cha sherehe za maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yaliyofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.
 Mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe na meza kuu wakiwa katika picha ya pamoja na Wahariri, Mameneja wa Redio za Jamii na Waandishi wa habari mara baada ya kuhutubia kilele cha sherehe za maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yaliyofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.
Mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe na meza kuu wakiwa katika picha ya pamoja na washiriki, wadau wa habari na wanafunzi wa Dodoma College of Jorunalism mara baada ya kuhutubia kilele cha sherehe za maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yaliyofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad