HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Monday, 7 May 2018

Ufunguzi wa Kombe la Mkuu wa Majeshi (CDF CUP 2018) kufanyika kesho

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kesho tarehe 8 May, 2018 litafungua rasmi mashindano ya Kombe la Mkuu wa Majeshi (CDF CUP) kuanzia saa 6:00 mchana katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Mashindano hayo yakiwa katika mzunguko wa  Tano (5) yatafanyika  kuanzia tarehe 8 Mei , 2018 hadi tarehe 18 Mei, 2018 katika Uwanja wa Uhuru na viwanja vilivyopo katika Kambi ya Jenerali Abdalah Twalipo,  Mgulani.

        Michezo itakayoshindaniwa ni ifuatayo:-
        1.     Mpira wa Miguu -  Wanaume.
        2.     Mpira wa Pete -  Wanawake.
        3.     Mpira wa Kikapu  ­- Wanaume na Wanawake.
4.     Mpira wa Wavu - Wanaume na Wanawake.
5.     Mpira wa Mikono -  Wanaume na Wanawake.
6.     Ngumi za Ridhaa  - Wanaume.
7.     Riadha – Wanaume na Wanawake.
        8.     Ulengaji   Shabaha – Wanaume na Wanawake.
        Washiriki wa Mashindano hayo ni Wanajeshi kutoka Kamandi  za  JWTZ ambazo ni:-
1.     Kamandi ya Makao Makuu ya Jeshi (NGOME).
2.     Kamandi ya Jeshi la Nchi Kavu  (Nyika).
3.     Kamandi ya Jeshi la Anga (AFC).
4.     Kamandi ya Jeshi  la Wanamaji (NC)
5.     Kamandi ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
        Mgeni rasmi katika siku ya ufunguzi anatarajiwa kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni  Sanaa na Michezo  Mhe.  Dkt. Harisson  George Mwakyembe (MB).
        Wanahabari na Wananchi Wote wapenda Michezo mnakaribishwa  kwa upendo mkubwa.
        Hakutakuwa na Kiingilio  kwenye Viwanja hivyo katika siku zote za mashindano hayo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad