HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, May 24, 2018

Mufti ahimiza uadilifu futari ya Standard Chartered

Na mwandishi wetu
Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir Bin Ally amesema Waislamu na walimwengu kwa ujumla wananafasi kubwa ya kujifunza mawaidha yanayotolewa katika mwezi Mtukufu wa Ramadhani ikiwamo kumcha Mungu na uadilifu.

Mufti alisema hayo kwenye futari iliyoandaliwa na benki ya Standard Chartered katika hoteli ya Serena.

Alisema katika hafla hiyo ambayo pia walikuwemo wageni wastahiki Balozi wa Indonesia nchini Tanzania, Mheshimiwa Prof. Dk. Ratlan Pardede na Balozi wa Heshima wa Siera Leone nchini Tanzania, Hussein Hamadi, kuwa mwezi wa Ramadhani ni chuo ambacho kinafunza mambo mbalimbali.

Alisema mafunzo hayo yanatarajiwa kutumika muda wote katika miezi 11 iliyobaki katika mwaka.

Alisema mambo ambayo yanazungumzwa katika Chuo hicho ni mengi lakini makubwa ni mahusiano katika masuala ya kiroho, kijamii, kiuchumi na kimaadili.

Alisema mafunzo yanayopatikana katika mwezi huo mmoja wa kumcha Mungu wenye siku takribani 29 hadi 30 yanatengeneza uaminifu si kwa Mungu pekee bali na kwa viumbe wake.

Aidha alisema amefurahishwa na Benki hiyo kutambua umuhimu wa mwezi huu kwa kutenga muda na mali ili kuwakutanisha wanajamii ili waweze kumcha Mungu na kujuana.

Alisema anaamini watu wa Standard Chartered ni waaminifu, waadilifu katika kutoa huduma na hilo ndilo Mungu analihitaji ugawaji wa haki kwa jamii katika usawa.

Katika futari hiyo Balozi wa Indonesia Prof Dk Ratlan Pardede aliwataka Waislamu katika umoja wao kuthamini matunda ya mwezi mtukufu wa Ramadhan na kutekeleza maagizo yake kwa manufaa yao ya kiroho, kijamii na kiuchumi.

Aidha Balozi wa Heshima wa Siera Leone nchini Hussein Hamadi alishukuru kwa hafla hiyo na kusema ni kitendo kinachokumbusha kuangalia haja ya umoja na kusaidia wasiokuwa nacho.

Naye Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo, Sanjay Rughani alisema kwamba hafla hiyo wameifanya kwa kutambua haja ya umoja katika tofauti za kidini zilizopo.

Alisema Benki yake imeandaa futari hiyo kwa kuzingatia kalenda yake katika kushiriki masuala ya kijamii yakiwemo matendo ya kidini.

Alisema matendo hayo ya kidini yanatekelezwa kwa lengo la kuheshimu dini za wateja wake na pia kuwakutanisha wateja na watendaji wakuu wa benki ili waweze kuwasilisha maoni yao.

Bw. Rughani pia alisema kwamba ili kuwawezesha wafanyakazi wake kushiriki kikamilifu katika mfungo wamefanya mabadiliko kadha yanayofanya mfungo kuwa rafiki na kazi zao.
 Mgeni rasmi Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir Bin Ally (kulia) akiongozana na Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered, Juanita Mramba (kushoto) pamoja na Mshereheshaji wa futari hiyo, Abdulssamad Ayoub (katikati) mara baada ya kuwasili kwenye futari iliyoandaliwa kwa wateja wa benki ya Standard Chartered katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 Balozi wa Indonesia nchini Tanzania, Mheshimiwa Prof. Dk. Ratlan Pardede (katikati) akiongozana na Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered, Juanita Mramba (kulia) pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Wateja wa Kawaida benki ya Standard Chartered nchini, Ajmar Riaz (kushoto) mara baada ya kuwasili kwenye futari iliyoandaliwa kwa wateja wa benki ya Standard Chartered katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani akisalimiana na mgeni rasmi Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir Bin Ally mara baada kuwasili kwenye futari iliyoandaliwa kwa wateja wa benki ya Standard Chartered katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Wengine ni na Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered, Juanita Mramba (wa pili kushoto) na Mshereheshaji wa futari hiyo, Abdulssamad Ayoub (kushoto)
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani (kulia) akisalimiana na Balozi wa Indonesia nchini Tanzania, Mheshimiwa Prof. Dk. Ratlan (katikati) mara baada ya kuwasili kwenye futari iliyoandaliwa kwa wateja wa benki hiyo katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Wateja wa Kawaida benki ya Standard Chartered nchini, Ajmar Riaz.
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani (kulia) akisalimiana na Mkuu wa Kitengo cha Wateja wa Kawaida benki ya Standard Chartered nchini, Ajmar Riaz (kushoto) mara baada ya kuwasili kwenye futari iliyoandaliwa kwa wateja wa benki hiyo katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 Mgeni rasmi Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir Bin Ally akitoa mawaidha kwa wateja wa benki ya Standard Chartered wakati wa futari iliyoandaliwakwa wateja wa benki hiyo katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani akizungumza na wateja pamoja na wageni waalikwa wakati wa futari iliyoandaliwa kwa wateja wa benki hiyo katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 Balozi wa Indonesia nchini, Prof Dk Ratlan Pardede akizungumza na wateja wa benki ya Standard Chartered wakati wa futari iliyoandaliwa kwa wateja wa benki hiyo katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 Balozi wa Heshima wa Siera Leone nchini, Mh. Hussein Hamadi akitoa salamu za mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa wateja wa benki ya Standard Chartered wakati wa futari iliyoandaliwa kwa wateja wa benki hiyo katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani akibadilishana mawazo na mgeni rasmi Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir Bin Ally (kulia) wakati wa futari iliyoandaliwa kwa wateja wa benki ya Standard Chartered katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 Mke wa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Bi Rughani (kulia) akisalimiana na baadhi ya wageni waalikwa wanaowasili ukumbini hapo kwenye futari iliyoandaliwa kwa wateja wa benki hiyo katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.


 Mgeni rasmi Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir Bin Ally (wa pili kulia) na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani (wa nne kulia) wakiongoza baadhi ya wateja na wageni waalikwa kupakua futari iliyoandaliwa kwa wateja wa benki hiyo katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 Kutoka kulia kwenda kushoto ni Mgeni rasmi Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir Bin Ally, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani, Balozi wa Indonesia nchini, Prof Dk Ratlan Pardede pamoja na Balozi wa Heshima wa Siera Leone nchini Hussein Hamadi wakiwa meza kuu wakati wa futari iliyoandaliwa kwa wateja wa benki hiyo katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 Mgeni rasmi Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir Bin Ally katika picha ya pamoja na meza kuu na baadhi ya viongozi wa Bakwata mara baada ya kumalizika kwa futari iliyoandaliwa kwa wateja wa benki ya Standard Chartered katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 Pichani juu na chini ni baadhi ya wateja na wadau wa benki ya Standard Chartered waliohudhuria futari iliyoandaliwa na benki hiyo katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani (katikati) akimkabidhi zawadi Balozi wa Heshima wa Siera Leone nchini, Mh. Hussein Hamadi (kushoto) ikiwa ni shukran kwa kushiriki futari iliyoandaliwa kwa wateja wa benki hiyo katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani akibadilishana mawazo na baadhi ya wateja wa benki hiyo mara baada ya kumalizika kwa futari iliyoandaliwa kwa wateja wa benki hiyo katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad