HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Monday, 7 May 2018

MAMIA YA WANAWAKE DAR WAPIMA SARATANI MLANGO WA KIZAZI, MATITI

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
MAMIA ya wanawake wa Mkoa wa Dar es Salaam wajitokeza kupima saratani ya mlango wa kizazi bure kutokana na uhamasishaji uliotolewa na muandaaji wa kipindi cha Ng’ari ng’ari, cha redio Clouds FM Sakina Lyoka .

Akizungumza wakati wa upimaji wa saratani ya mlanngo wa kizazi Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni  Edith Mboga amesema tatizo la saratani ya mlango wa kizazi ni kubwa, hivyo wanawake wanatakiwa kupima ili  wakikutwa katika hatua ya kwanza waanze kutibiwa na kuondoka kwa saratani hiyo.

Mboga amesema wanawake wamehasika katika upimaji wa saratani ya mlango wa kizazi kutokana matangazo yaliyokuwa yakirushwa kupitia kipindi cha Ng’ari ng’ari.

Kwa upande wa Mwandaji wa kipindi cha Ng’ari ng’ari, Sakina Lyoka amesema kama mama hawezi kubaki nyuma huku wanawake wengine wakiteseka kutokana na kushindwa kufikiwa na huduma za za upimaji wa satatani ya mlango wa kizazi pamoja matiti.

Ameongeza jambo ambalo limemfurasha ni idadi ya wanawake ambao wamejitokeza kupima saratani ya mlango wa kizazi na matiti.Hivyo imempa moyo wa kuendelea kuihamasisha jamii katika upimaji wa afya zao na hasa kupima saratani.
Mwakilishi Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni, Edith Mboga akizungumza na waandishi wa habari wakati wa upimaji wa afya ya saratani ya Mlango wa Kizazi na Matiti, upimaji huo uliofanyika viwanja vya Escpe One jijini Dar es Salaam.
Mwandaji wa kipindi cha Ng’ari ng’ari, Sakina Lyoka akizungumza na waandishi habari kuhusiana na mwitikio wa wanawake kupima saratani ya mlango wa kizazi  na matiti , upimaji huo uliofanyika viwanja vya Escpe One jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni, Edith Mboga akikabidhi cheti kudhamini upimaji wa wa saratani ya Mlango wa Kazazi na Matiti Mkurugenzi wa  Jadore Hair & Beuty,  Ruth Urio  wakati wa upimaji huo uliofanyika katika viwanja vya Escape one , jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya wanawake waliojitokeza katika upimaji wa saratani ya mlango wa kizazi na matiti.
Wadhamini wa upimaji wa Saratani ya Mlango wa Kizazi na matiti wakiwa katika picha ya pamoja na Mwakilishi Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni,Edith Mboga wakiongozwa na Mwandaji wa kipindi cha Ng’ari ng’ari, Sakina Lyoka.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad