HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, 13 May 2018

LUKUVI ATATUA MGOGORO MKONGWE WA ARDHI SOMJI- BOKO JIJINI DAR

Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Willium Lukuvi  ametatua mgogoro mkongwe wa ardhi huko Boko kata ya Dovya maarufu kama kwa Somji  jijini Dar es salaam.

Akizungumza na wananchi Lukuvi  ameeleza Rais John Magufuli amempa maelekezo sambaba na kumaliza mgogoro huo.

Amesema  kuwa ardhi hiyo ni mali ya Serikali na wananchi waliojenga makazi yao ni wavamizi kwani eneo hilo la hekari 366 lilichukuliwa na serikali rasmi mwaka 1975 kutoka kwa Somji ambaye alikuwa mmiliki wa eneo hilo.

Aidha ameeleza  kama Serikali haiwezi kuvunja majengo ya wakazi hao ila lazima wafuate taratibu zilizowekwa ili kupata umiliki halali wa viwanja hivyo.

Lukuvi ameeleza lazima mipaka yote ya shamba la Somoji la mwaka 1952 ipimwe ili iweze kujulikana pia ofisi za mipango miji za wizara na Manispaa iangalie kama kuna mipango yoyote ilitokea kuhisiana na eneo hilo.

Ameeleza kwa wenye hati na michoro lazima ihakikiwe kama ipo sahihi sambamba na maelezo ya ya wamiliki kuhusiana na umiliki wao.

Lukuvi ameeleza kuwa kamati iliyoundwa itashirikiana na wataalamu wa wizara ambao watapima maeneo hayo na kugaiwa kwa wananchi na kuanza kuyalipia kodi rasmi na zoezi limalizike mwezi Septemba mwishoni ili wananchi wakabidhiwe hati zao rasmi.

Ameeleza kuwa fedha hizo ndizo zitakazolipa fidia kwa Somji, na amesisitiza gharama zitalipwa kulingana na eneo la umiliki.

Mbunge wa Kawe Halima Mdee amemshukuru waziri kwa jitihada za kutatua mgogoro huo na amewaomba wakazi hao kutunza maeneo hayo na wawe walinzi kwa ardhi hiyo.

Naye mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ally Hapi amemshukuru Rais  kwa kukubali ardhi irudishwe kwa wananchi na amehaidi kupambana na matapeli wowote dhidi ya utapeli utakaofanywa juu ya viwanja hivyo na ameiomba kamati itoe taarifa kwa kila hatua ya utekelezaji huo.

Kuhusiana na mgogoro huu Lukuvi ameeleza kuwa hati ya kwanza ya eneo hilo ilitolewa mwaka 1952 likiwa na hekari 366 na baadae kumilikiwa na Somji mwaka 1971 na kufikia mwaka 1975 serikali ilichukua hekari 8.5 kwa ajili ya matumizi ya umma na ilitangazwa kwenye gazeti la serikali na kufikia mwaka 2002 Serikali ilitwaa  hekari 357.5 zilizosalia  na Somji hakulipwa fidia.

Kufikia mwaka 2003 Somji alifungua mashtaka dhidi ya serikali na walishindwa kesi kwa mahakama kuunga mkono maamuzi ya Serikali ya kuchukua ardhi hiyo na kilichobaki ilikuwa ni Somji kulipwa fidia.
Waziri wa Ardhi, Mhe. William Lukuvi, akizungumza  katika mkutano  wa hadhara na  wananchi wa Boko ambapo ametatua mgogoro wa ardhi uliodumu kwa  zaidi ya miaka 40 katika eneo la Somji lenye hekari 366 jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuele Massaka wa Globu ya jamii)
 Mbunge wa Kawe Halima Mdee akizungumza na wananchi katika mkutano huo wa kutatua mgogoro wa ardhi ambapo ameishukuru serikali kwa kutatua mgogoro huo.
 Waziri wa Ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi, William Lukuvi  akiteta jambo na Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Ally Hapi katika mkutano wa hadhara na wananchi wa Boko ambapo ametatua mgogoro wa ardhi uliodumu kwa  zaidi ya miaka 40 katika eneo la Somji lenye hekari 366 jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Ardhi, Mhe. William Lukuvi akijibu maswali mabalimbali aliyoulizwa na wananchi wa  Boko ambapo ametatua mgogoro wa ardhi uliodumu kwa  zaidi ya miaka 40 katika eneo la Somji lenye hekari 366  jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuele Massaka wa Globu ya jamii)
 Baadhi ya wananchi wa Boko wakimsikiliza Waziri wa Ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi William Lukuvi katika mkutano huo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad