HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Sunday, 13 May 2018

IFM imeaswa kushirikiana na wadau mbalimbali katika kutoa elimu ya bima- Dk. Kijaji

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
SERIKALI imekitaka Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) kushirikiana na wadau mbalimbali katika kutoa elimu ya bima ili kuweza kuongeza pato la taifa pamoja na ukuaji wa uchumi.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango,Dk. Ashantu Kijaji wakati wa uzinduzi program za shahada za uzamili mbili na shahada moja za chuo cha usimamizi wa fedha (IFM) hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

Shahada uzamili zilizinduliwa ni Master of Scence in Social Protection Policy and Development , Master of Science Isuarance and Acturial Science  pamoja na bachelor of Science in Acturial Sciences.

Amesema mchango  wa sekta bima na hifadhi ya jamii ni mdogo kutokana na wananchi kukosa elimu na kufanya sekta ya bima na hifadhi ya jamii kuchangia asilimia moja katika  pato la Taifa.

Dk.Kijaji amesema kuwa chuo cha IFM kimeona mbali katika kuanzisha kozi mbili za uzazmili katika bima ili kuweza kujibu baadhi ya changamoto zilizopo katika  sekta hiyo.

Amesema nchi inakwenda  katika uchumi wa viwanda ambapo uchumi huo sehemu kubwa unashikwa na kilimo kutokana  na kuajiri idadi kubwa ya watanzania lakini idadi hiyo  haina  elimu ya bima.

Nae Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Thaudes Satta  amesema  chuo kimendelea kutoa elimu bora pamoja na kusimamia maadili na kufanya kuendelea kuongeza kozi katika kutatua changamoto katika baadhi ya maeneo ikiwemo sekta ya bima.

Amesema amesema kuwa kutokana na mahitaji ya bima chuo kitaendelea kufanya utafiti ili kuweza kuziba nafasi katika sekta hiyo na nchi kuweza kunufaika na bima.
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashantu Kijaji akizungumza wakati wa uzinduzi wa program shahada mbili za Uzamili na Shahada moja za Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) uliofanyika katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Baraza la Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Profesa Lettice Rutashobya akizungumza kuhusiana na kuanzisha kwa kwa shahada mbili za uzamili pamoja na shahada moja katika mwaka huu , katika halfa ya uzinduzi huo uliofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Chuo cha IFM, Profesa Thadeus Satta akizungumza kuhusiana na chuo kilivyojipanga katika kutoa elimu bora na kusimamia maadili ya chuo hicho katika hafla uzinduzi wa shahada mbili huo uliofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Mkuu wa Kitivo cha Bima na Hifadhi ya Jamii  wa Chuo Cha Usimamizi wa Fedha (IFM),Dk. Said Jafari  akitoa maelezo kuanzishwa program ya shahada za uzamili.
 .Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashantu Kijaji akikata utepe kuashiria uzinduzi wa program mbili za Uzamili pamoja na shahada moja.
Sehemu ya wanafunzi wahitimu  watendaji na watoa maada na wadau katika uzinduzi wa program shahada za uzamili

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad