HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 8 May 2018

Chuo cha biashara cha Rungwe na Taasisi ya Yemco zimetiliana saini kuwajengea uwezo wajasiliamali

Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii.
Chuo cha kimataifa cha Biashara na Ujasiriajari Rungwe na Taasisi ya Youth Empowerment and Mindset Change Organization (Yemco) leo zimetiliana saini mkataba wa makubaliano wa kuendeleza jamii na kuwajengea uwezo wa ujasiriamali vijana, akina mama na wanavicoba.

Mwakilishi wa Mkuu wa Chuo cha Rungwe, Dk Lenny Kasoga amesema makubaliano hayo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam,  yataongeza chachu ya kuboresha uwezo wa jamii na kuwa na wataalam wengine wenye ujuzi tofauti tofauti  katika maeneo ya ujasiriamali na kuleta maendeleo haraka hasa kwa vijana, akina mama na wanavicoba.

Amesema, Taasisi hizo  hazitajikita kwenye kutoa elimu ya ujasiriamali pekee Bali pia zitajihusisha katika kufanya tafiti kwa nia ya kutatua changamoto zinazojitokeza katika jamii na kutoa majibu.

Kasoga ambaye pia ni mhadhiri Mwandamizi wa uchumi na biashara amesema utekelezaji wa mkataba huo utakuwa na manufaa ikiwa ni pamoja na kuongea idadi ya wajasiriamali watakaokuwa na uwezo wa kubainisha fursa na kuzitumia vilivyo kwa kuanzisha biashara  za kati na zenye kuleta ajira na pato kwa Taifa.

Ameongeza kuwa ushirikiano huo unawezekana kutokana na dhamira ya Serikali katika kujenga mazingira bora ya kisera, kisheria na utendaji  yanayolenga kuleta maendeleo endelevu kwenye ujasiriamali  na hivyo kuchochea ukuaji wa uchumi.

Dk Kasoga aliwahakikishia wananchi kuwa ushirikiano huo utajikita kwenye kutengeneza ajira kwa vijana, akina mama na wanavikundi wa Vicoba kwa kuhakikisha viwanda vidogo na vya kati ambacho ni tofauti na vilivyopo vinaanzishwa.

"Nia yetu ni kuona wananchi na wadau wanashiriki ipasavyo na kwa usawa katika kujenga nchi yetu yenye fursa nyingine za kiuchumi." Alisema Dk Kasoga.

Mkurugenzi wa Yemco, Mohammed Bassanga alisema makubaliano hayo utoaji wa mafunzo hayo ya ujasiriamali na vicoba endelevu utahusisha na watu wenye ulemavu  ili waweze kujiletea maendeleo na kupambana na changamoto za kimaisha.

Alibainisha kuwa  makubaliano hayo yataxhangia juhudi za  serikali ya Muungano wa Tanzania katika kuchochea ukuaji wa uchumi hapa nchini.

Mwakilishi wa bodi ya Chuo cha Rungwe, Mwanasheria Benjamin Mwakagamba alisema  ni Mara chache Taasisi binfsi zinaungana kufanya kazi ya kumsaidia jamii na kupongeza.
 Mwakilishi wa Mkuu wa Chuo cha Kimataifa cha Biashara na Ujasiriamali Rungwe Dk Lenny Kasoga akitiliana saini mkataba wa makubaliano ya kuendeleza jamii kwa kuijengea uwezo wa ujasiriamali  kwa vijana, akina mama na wanavicoba na Mkurugenzi wa Yemco Mohammed Bassanga wakishuhudiwa na mwakilishi wa bodi Chuo cha Rungwe Benjamin Mwakagamba na mwanasheria Isabella Mwaipopo.
Mwakilishi wa Mkuu wa Chuo cha Kimataifa cha Biashara na Ujasiriamali Rungwe, Dk Lenny Kasoga(wa pili kushoto)  akionyesha mkataba waliotiliana saini ya makubaliano na Mkurugenzi wa Yemco, Mohammed Bassanga(wa pili kulia)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad