HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 8 May 2018

Halmashauri ya Kishapu yakabidhi maabara kwa Shule ya Mangu

Na Robert Hokororo, Ofisi ya Mkurugenzi
Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu imekabidhi jengo la maabara kwa Shule ya Sekondari Mangu iliyopo Kata ya Shagihilu baada ya ujenzi wake kukamilika.
Maabara hiyo iliyokamilika gharama ya thamani ya Sh. Milioni 10.1 linatarajiwa kuwa msaada mkubwa kwa wanafunzi wa shule hiyo wa mchepuo wa sayansi kwa vitendo.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Mang’era Mang’era akikabidhi jengo hilo alisema litachochea ufaulu wa wanafunzi ambao awali walikosa mazoezi ya vitendo.
Alisema lengo la Halmashauri ni kuhakikisha elimu inakua na hivyo inaendelea kuboresha miundombinu ya shule zake ikiwemo ujenzi wa maabara kwa ajili ya sayansi.
Mang’era Mang’era aliwataka walimu na wanafunzi kuwa kitu kimoja na kuitendea haki maabara hiyo kwa kushirikiana ili wawe na ufaulu mzuri katika mitihani inayohusisha mazoezi ya vitendo.
Alisema kuwa ufaulu kwa wanafunzi katika shule hiyo na zingine utafaleta sifa kwa wananchi wa kata hiyo pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu kwa ujumla.
Mang’era ambaye pia ni Afisa Mipango aliwataka wanafunzi kuwa na nidhamu na kusoma kwa bidii ili kuweza kufikia malengo yao ya baadaye katika kitaaluma.  
Aidha aliwashukuru wananchi kwa kushiriki katika shughuli za maendeleo ikiwemo kuchangia nguvu kazi katika kufanikisha ujenzi wa jingo hilo la maabara.
Alisema juhudi za wananchi zimefanikisha ujenzi wa maabara hiyo ambao wamekuwa wakichangia nguvu kazi katika maendeleo yao kama ambavyo Serikali imekuwa ikisisitiza.
Shule za sekondari Mangu yenye wanafunzi wa kidato cha kwanza hadi cha nne inatarajiwa kupandishwa hadhi na hatimaye kuanza kuchukua wanafunzi wa kidato cha tano na sita,
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Mang’era Mang’era akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa jengo la maabara Shule ya Sekondari Mangu.
 Viongozi mbalimbali wakiangalia maabara ya Shule ya Sekondari Mangu baada ya kuziduliwa rasmi na kukabidhiwa baada ya ujenzi wake kukamilika.
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Mang’era Mang’era (kulia) akiwa na Afisa Elimu Sekondari, Paul Kasanda wakiangalia vifaa mbaimbali vya maabara hiyo.
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Mang’era Mang’era akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mangu (hawapo pichani) wakati wa makabidhiano ya jengo la maabara.
 Diwani wa Kata ya Shagihilu, Mhe. Mohamedi Amani akitoa neno la shukrani katika hafla hiyo.
 Muonekano wa maabara hiyo wakati viongozi mbalimbali walipotembelea baada ya kufunguliwa rasmi.
 Afisa Elimu Sekondari, Paul Kasanda akizungumza wakati wa hafla hiyo.
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Mang’era Mang’era akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mangu.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari Mangu, Hangaya Hangaya akitoa maelezo mafupi kuhusu jengo la maabara iliyokamilika ujenzi wake kabla ya kuzinduliwa na kukabidhiwa shule hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad