HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Friday, 13 April 2018

YALIYOJIRI LEO BUNGENI MJINI DODOMA

 Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Viziwi kutoka Mkoa wa Dodoma pamoja na Shule ya Sekondari Tagamenda kutoka Mkoa wa Iringa wakifuatilia mijadala inayoendelea ndani ya Bunge ikiwa ni sehemu ya ziara yao ya Mafunzo Bungeni.
 Viongozi  Mbali mbali  wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kutoka Mkoa wa Mbeya na Wilaya zake wakifuatilia jinsi muhimili wa Bunge unavyofanya kazi yake, leo katika ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma.
 Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kulia) akisalimiana na Mheshimiwa Saul Amon (kushoto) leo katika Viwanja vya bunge Mjini Dodoma. Katikati ni Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mwenye miwani), anaefuata ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kutoka Mkoa wa Mbeya, Ndg. Jacob Mwakasole na wengine ni Viongozi Mbali mbali wa Chama cha Mapinduzi kutoka Mkoa wa Mbeya na Wilaya zake ambao ni wageni wa Naibu Spika wa Bunge.
Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (kushoto) akisalimiana na mmoja ya Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kutoka Mkoa wa Mbeya leo katika Viwanja vya bunge Mjini Dodoma. Kulia ni Mhe. Victor Mwambalaswa.
 Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai (wa saba kulia mbele), Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson (wa tisa kulia mbele) wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi Mbali mbali wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kutoka Mkoa wa Mbeya na Wilaya yake leo katika viwanja vya Bunge Mjini Dodoma. Wa nane kulia mbele ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kutoka Mkoa wa Mbeya, Ndg. Jacob Mwakasole
(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad