HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, April 30, 2018

UN yataka vyombo vya habari kukazania uwajibikaji

Na Mwandishi Wetu, Morogoro
Umoja wa Mataifa (UN) umetaka Vyombo vya Habari nchini kuweka mkazo katika kuandika na kutangaza masuala ya maendeleo na ya kiutu, hasa yale yanayoweza kujenga uelewa zaidi na kuchochea vitendo na uwajibikaji kwa manufaa ya Watanzania walio wengi.
Kauli hiyo imetolewa na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Alvaro Rodriguez, katika mkutano wa ndani wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF)  uliofanyika mwishoni mwa juma mjini Morogoro.
Katika hotuba yake hiyo iliyosomwa na Mkuu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa nchini Hoyce Temu alisema, kwa kuwa Vyombo vya habari ndiyo kiunganishi kikuu kati ya watu, serikali na mashirika ya kimataifa hivyo ni wajibu wao kuandika habari zinazochochea maendeleo.
Aidha alisema kwa namna ya pekee, angependa kusisitiza umuhimu wa kuandika habari za hatua zinazopigwa katika utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) na Mpango wa Taifa wa Miaka Mitano na vilevile MKUZA II na III.
“Haya ni maeneo muhimu kwa sababu aina ya mabadiliko tunayotaka kuyaona nchini Tanzania katika miaka michache ijayo yatawezekana tu ikiwa mipango hii mitatu itatekelezwa kwa ufanisi na kikamilifu kwa kuzingatia muda uliopangwa. Ni wajibu wenu, kama waandishi wa habari wanaojua kazi yao kushiriki kikamilifu katika wajibu huu wa kusimamia na kutolea taarifa masuala haya ili kuimarisha uwajibikaji” alisema Rodriguez.
Aidha alisema kwa kuwa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania unatekeleza mpango wa UNDAP II, ambao ni mpango wa Miaka Mitano wa Maendeleo unaolenga kuainisha vema programu ya ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na Timu ya UN ya Nchi, ambao hatimaye utaimarisha fursa za maendeleo ya kijamii, kiuchumi na kisiasa, vyombo vya habari vitaweza kusaidia kuhakikisha kwamba hakuna yeyote anayeachwa nyuma.
Serikali ya Tanzania na Timu ya Nchi ya UN zinashirikiana Dira ya Taifa na SDGs kwa kushughulikia maeneo matano ya kimaudhui  ambayo ni Utawala wa Kidemokrasi, Haki za Binadamu & Usawa wa Jinsia—kuleta taasisi zenye uwazi na zenye kuwajibika na kuleta usawa wa jinsia.
Maeneo mengine ya kimaudhui ni Uwezo wa kujinusuru kwa kuimarisha usimamizi wa mazingira, upatikanaji wa nishati na kusaidia usimamizi wa wakimbizi na wahamiaji na kujenga taifa lenye ustawi kwa kuimarisha upatikanaji wa huduma za afya, maji safi, usafi wa mazingira; kuimarisha lishe kwa wanawake na watoto wa chini ya umri wa miaka mitano.
Aidha maeneo mengine ni Ukuaji jumuishi ambao unasaidia, kupunguza umaskini na kuongeza fursa za kuongeza ajira, upatikanaji wa elimu ya msingi na usalama wa kijamii hasa kwa makundi ya maskini/wanyonge na mwisho  ni kuwezesha mawasiliano, Huduma za Uwandani, Utetezi na Ushirika
Wakati huo huo  UN na TEF wametiliana saini mkataba utakaowezesha kujenga  uwezo kwa  waandishi wa habari kufuatilia utekelezaji wa malengo ya Dunia yalihuishwa katika Mpango wa Taifa wa Miaka Mitano na Mkuza III.
Mpango huo ambao umo ndani ya UNDAP ll unashirikisha maarifa, uvumbuzi mpya, utetezi na kutomwacha yeyote nyuma na kuunga mkono sera mpya ambazo zitasaidia utekelezwaji wa Malengo ya Dunia.
“Tuna matumaini makubwa na ushirikiano huu na TEF ili kuhakikisha mpango wetu kama unavyoelewa katika Kanuni za Ushirikiano ambao tumetia saini leo unatekelezwa kikamilifu na kuleta matokeo yanayotakiwa.” Alisema Zaman.
Ushirikiano kati ya TEF na UN kwa sasa una miaka mitano.
 Kaimu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF), Deodatus Balile akifungua kikao kati ya Jukwaa hilo na Umoja wa Mataifa wakati wa mkutano wa ndani wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) uliofadhiliwa na UN pamoja wadau mbalimbali uliofanyika mwishoni mwa wiki mjini Morogoro.
 Mkuu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa, Hoyce Temu akisoma hotuba kwa niaba ya Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa, Alvaro Rodriguez wakati wa mkutano wa ndani wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) uliofadhiliwa na UN pamoja wadau mbalimbali uliofanyika mwishoni mwa wiki mjini Morogoro.
 Mtaalamu wa Mawasiliano wa Shirika linaloshughulikia Watoto la Umoja wa Mataifa, Usia Nkhoma-Ledama  akizungumzia uhusiano na ushirikiano kati ya TEF na mashirika ya Umoja wa Mataifa wakati wa mkutano wa ndani wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) uliofadhiliwa na UN pamoja wadau mbalimbali uliofanyika mwishoni mwa wiki mjini Morogoro.
 Washiriki wa kikao cha Jukwaa  la Wahariri (TEF) wakifuatilia kwa umakini mada ya Malengo ya Dunia na ushirikiano wa kuwezesha malengo hayo kutekelezeka wakati wa mkutano wa ndani wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) uliofadhiliwa na UN pamoja wadau mbalimbali uliofanyika mwishoni mwa wiki mjini Morogoro.
 Allan Lawa wa Mwananchi Communications akizungumzia ushirikiano kati ya TEF na UN wakati wa mkutano wa ndani wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) uliofadhiliwa na UN pamoja wadau mbalimbali uliofanyika mwishoni mwa wiki mjini Morogoro.
 MwenyekitI wa zamani wa Jukwaa la Wahariri (TEF) ambaye pia ni mmoja wa waanzilishi wa TEF, Theophil Makunga akitoa maoni yake kuhusu namna ambavyo Umoja wa Mataifa na TEF wanavyoweza kushirikiana wakati wa mkutano wa ndani wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) uliofadhiliwa na UN pamoja wadau mbalimbali uliofanyika mwishoni mwa wiki mjini Morogoro.
 Zourha Malisa wa Mwananchi Communications akielezea umuhimu wa ushirikiano wa UN na Jukwaa la Wahariri kuhusisha pia Vyombo vya Mitandaoni na Bloggers wakati wa mkutano wa ndani wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) uliofadhiliwa na UN pamoja wadau mbalimbali uliofanyika mwishoni mwa wiki mjini Morogoro.
 Katibu wa Jukwaa la Wahariri (TEF), Neville Meena akielezea kwa undani namna ambavyo mafunzo yaliyo katika mkataba wao na UN yatakavyoendeshwa wakati wa mkutano wa ndani wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) uliofadhiliwa na UN pamoja wadau mbalimbali uliofanyika mwishoni mwa wiki mjini Morogoro.
 Mkuu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa, Hoyce Temu akisaini kanuni za ushirikiano kati ya TEF na UN kwa niaba ya Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Alvaro Rodriguez wakati wa mkutano wa ndani wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) uliofadhiliwa na UN pamoja wadau mbalimbali uliofanyika mwishoni mwa wiki mjini Morogoro.
Mkuu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa, Hoyce Temu na Kaimu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF), Deodatus Balile wakibadilishana nakala za ushirikiano kati ya TEF na UN wakati wa mkutano wa ndani wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) uliofadhiliwa na UN pamoja wadau mbalimbali uliofanyika mwishoni mwa wiki mjini Morogoro.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad