HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, April 11, 2018

SERIKALI KUZIFUTIA USAJILI NGOs ZITAKAZOFANYA KAZI KINYUME NA SHERIA

Na Mwandishi Wetu – Mwanza
Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,  Wazee na Watoto Idara ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGOs) imesema haitasita kulifutia usajali Shirika lolote lisilo la Kiserikali litakaloenda kinyume na Sheria na Taratibu za nchi.

Hayo yamesemwa leo Jijini Mwanza na Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Bw. Marcel Katemba alipokuwa akifungua kikao kati yake na Wasajili Wasaidizi wa Mashirka Yasiyo ya Kiserikali na Wadau wa mashirika hayo kwa Mkoa wa Mwanza.

Bw. Katemba amesisitiza kuwa kwa mujibu wa Sheria namba 4 ya Mwaka 2002 ya Mashirika Yasito ya Kiserikali inayataka Mashirika hayo kuzingatia Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo ya Nchi katika utendaji wa kazi zao kwa mujibu wa Katiba na majukumu yao kiusajili.

Ameongeza kuwa kikao hicho kimefanyika ili kuwakumbusha wadau wa NGOs kufanyakazi kwa kuzingatia Sheria za nchi zilizopo kwani baadhi ya mashirika hayo yamekuwa yakitumika kufanya mambo ambayo yapo kinyume na Sheria.

“Nawataka wamiliki wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kuzingatia matakwa ya usajili wao katika kutekeleza majukumu katika Mashirika yao” alisema Bw.Katemba

Bw.Katemba amesema kuwa mpaka sasa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali 4,868 ndio yamehakikiwa na kuyataka Mashirika ambayo hayajahakikiwa  yafanye utaratibu wa kuhakiki kwani mara baada ya kuzinduliwa kwa Tovuti mpya ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini Mashirika ambayo hayatakuwa yamehakikiwa hayataruhusiwa kufanya kazi nchini.

Naye mdau kutoka Shirika la Baraka Orphanage Bi. Patricia Kamugisha asema kuwa kikao hicho imewasaidia kujifunza mambo mengi ambayo walikuwa hawajafahamu na kuendelea kupata uzoefu utakaowasaidiza kuimarisha utendaji wa shughuli katika mashirika yao.

“Sisi kama wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali tunatakiwa kuzingatia Sheria na Taratibu zilizopo ili tuweze kufanya kazi bila kukinzana na Sheria” alisisitiza Bi. Patricia.
 Mkurugenzi wa  Idara ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali na Msajili wa Mashirika hayo Bw. Marcel Katemba akizungumza na Wasajili Wasaidizi wa  Mashirka Yasiyo ya Kiserikali kutoka katika Halmashauri na Wilaya za Mkoa wa Mwanza katika kikao baina yake na Wasajili Wasaidizi hao na wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kilicholenga kuboresha namna bora ya uendeshaji wa mashirika hayo mkoani humo.
 Mkurugenzi  wa Msaidizi Idara ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Bw. Leornald Baraka akiwakumbusha washiriki mambo muhimu yanayohitaji kuzingatiwa kabla na baada ya kusajili Shirika Lisilo la Kiserikali kwa wadau kutoka katika Mashirika hayo katika kikao kilichowakutanisha Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, Wasajili Wasaidizi na wadau hao mkoani Mwanza kilicholenga kuboresha namna bora ya uendeshaji wa mashirika hayo mkoani humo.
 Baadhi ya wadau kutoka Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Mkoani Mwanza wakifuatilia mada na mafunzo mbalimbali yaliyokuwa yakitolea na Msajili wa Mashirika hayo katika kikao kilichowakutanisha Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, Wasajili Wasaidizi na wadau hao mkoani Mwanza kilicholenga kuboresha namna bora ya uendeshaji wa mashirika hayo mkoani humo.
 Mmoja wa mdau kutoka Shirika la Kivulini Bi.Yunice Mayengera akiuliza swali  kuhusu utaratibu wa kuhakikiwa kwa mashirika ambayo awali yalisajiliwa chini ya Sheria nyingine kwa Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali katika kikao kilichowakutanisha Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, Wasajili Wasaidizi na wadau hao mkoani Mwanza kilicholenga kuboresha uendeshaji wa mashirika hayo kwa kuzingatia Sheria na miongozo mkoani humo.
 Afisa Maendeleo ya Jamii na Msajili Msaidizi wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali katika Manispaa ya Ilemela  Bw. Yusuph Omolo akitoa ufafanuzi  kuhusu masuala yahusuyo Usajili wa Mashirka Yasiyo ya Kiserikali kwa  wadau wa Mashirika hayo katika kikao kilichowakutanisha Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, Wasajili Wasaidizi na wadau hao mkoani Mwanza kilicholenga kuboresha uendeshaji wa mashirika hayo kwa kuzingatia Sheria na miongozo mkoani humo. Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW.   

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad