HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 25 April 2018

REX ENERGY YAWAANDAA VIJANA 100 KUTOKA DIT KABLA YA KUWAPA AJIRA

Na Ripota Wetu, Globu ya jamii
MKURUGENZI Mkuu wa Rex Energy inayojuhusisha na utoaji wa huduma ya umeme wa jua Francis Kibhisa ameamua kutoa mafunzo ya vitendo kwa wahandisi 100 ambao wamehitimu Dar es Salaam Institute Technology(DIT)na baada ya hapo atawapa ajira huku akifafanua ipo haja ya kuhakikisha vijana wa kitanzania wanapata ajira.

 Kibhisa ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam ambapo amesema wameamua kuja na utaratibu wa kuwachukua wahitimu wa vyuo mbalimbali nchini na kisha kuwapata elimu kwa vitendo kabla ya kuwapa ajira na wale ambao wataonekana wanamudu majukumu yao basi watapewa ajira.

Amesme wameanza na Mkoa wa Dar es Salaam kwa kuchukua wahitimu hao 100 kutoka DIT na baada ya mafunzo hayo watawasambaza kwenye matawi yao yaliyopo Dar es Salaam na mikoani ambapo watakuwa kwenye majaribio kwa mwaka mmoja na baada ya hapo watapata ajira.

Amefafanua ndani ya muda huo watakuwa wanalipwa baadhi ya stahiki zao kama ambavyo wanapewa walioajiriwa ili wajikimu kimaisha wakati wanaendelea na majukumu yao.

"Sisi tumeanza na tutaendelea, kuna vijana wengi ambao wamehitimu vyuoni lakini hawana pakwenda, kwetu tumeamua kuwapa ajira vijana hao na kabla ya kufika kwenye ajira tumeamua kwanza tuwape elimu ya kile ambacho watakwenda kukifanyia kazi.

"Bahati nzuri kauli mbiu ya Serikali ni watu kufanya kazi na hivyo wameona wanayo nafasi ya kuhakikisha wanaunga mkono kauli mbiu hiyo kwa kuwaajiri vijana wa kitanzania nao wawe sehemu ya ujenzi wa maendeleo ya nchi yetu.

"Ushauri wangu wenye uwezo wa kuajiri ni vema wakafanya kila linalowezekana kuajiri vijana wa kitanzania.Tumeanza na wahandisi hao zaidi ya 100 ambapo tutawapa mafunzo kwa siku tatu na baada ya hapo watakwenda kwenye maeneo yao ya kazi,"amesema.

Ameongeza Rex Energy wamekuwa kwenye soko sasa kwa miaka 18 huku akielezea changamoto kubwa iliyopo ni kuingizwa kwa vifaa ambavyo havijakidhi ubora , hivyo ameomba waaoingiza vifaa hivyo hasa vinavyohusu masuala ya Sola wakazingatia ubora unaohitajika kimataifa.

Ametoa rai kwa vijana nchini wanapaswa kufanya kazi kwa bidii na kueleza Mhandisi wa sasa atakombolewa kwa kufanya kazi kwa bidii na si vinginevyo.

Kuhusu mafunzo ambayo wanayaotoa kwa vijana hao kabla ya kuwapingia maeneo ya kufanyia kazi, Kibhisa amesema wanafundisha namna ya kuhudumia mteja, mhandis wa sasa atakombolewa kwa kufanya kazi kwa bidii.

Baadhi ya vijana wanaopatiwa mafunzo hayo na Rex Energy akiwamo Coletha Jackson na Nyaronga Nguka wamesema yameongeza maarifa zaidi ya yale ambayo wameyapata wakiwa DIT.

Pia wamewashauri vijana badala ya kukaa vijiweni kuchangamkia fursa kama ambayo wameipata wao baada ya kuona kwenye mtandao kuhusu taarifa ya Rex Energy waliomba na hatimaye wamepata.
Mkurugenzi Mtendaji wa Rexy Energy, Francis Kibhisa akizungumzia jijini Dar es Salaam leo kuhusu mafunzo wanayoyatoa kwa wahitimu 100 wa DIT ambao wamewachukua kwa lengo la kuwaajiri.
Baadhi ya vijana wakiendelea kuwepewa mafunzo kutoka kwa watalaam wa Rexy Energy jijini Dar es Salaam

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad