HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 26 April 2018

UNESCO yafunga mafuzo ya Mafundi Mitambo wa Radio za jamii 25

Na Ripota Wetu, Globu ya jamii
SHIRIKA la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (Unesco) limesema mafunzo ambayo wameyapata mafundi mitambo kutoka redio za jami 25 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar yalete tija na mabadiliko katika kutekeleza majukumu yao kwa maslahi ya jamii.

Pia limesema matumaini ya Unesco mafunzo hayo yatakuwa chachu kwa wale ambayo wameyapata lakini ni vema waliyoyapata nao wakaenda kuwaelimisha wenzao ambao wamewaacha maofisini na kufanya hivyo itakuwa na tija zaidi na kuleta mabadiliko kwa haraka na kubwa zaidi wameomba washiririki wa mafunzo hayo wasiwaangushe.

Akizungumza wakati akifunga mafunzo kwa mafundi mitambo hao ambayo yamefanyika kwa siku saba Kaimu Mkuu Ofisi ya Mkuu wa Kitengo cha Elimu Unesco Dar es Salaam Faith Shayo shirika lao linayo furaha kuona mafundi mitambo hao wamepata elimu ambayo inaendelea kuwajengea na imani yao watakuwa na mabadiliko kutokana na kile ambacho wamekipata kwa muda wa siku saba walipokuwa wakijifunza.

"Waliopata mafunzo hayo wapo 47 na kila mmoja akifanya kazi kwa kuonesha mabadiliko maana yake itakuwa na tija.Pia mafunzo yawe chachu ya huko mnakokwenda kwenye redio zenu tunajua wapo ambao mmewaacha basi nao mkawape elimu ambayo ninyi mmeipata,"amesema.

Amefafanua siku saba ambazo wamekuwa wakijifunza na baada ya kumaliza watakuwa na kitu cha kuwabadilisha maana kikubwa katika maisha ya binadamu ni kuwa na mabadiliko ambayo msingi wake yatatokana na elimu.

Amesisitiza elimu waliyoipata mafundi mitambo hao ilete mabadiliko katika kazi zao na kueleza jukumu la Unesco ni kutafuta fedha kwa wafadhili na kisha kutoa elimu hiyo lakini juhudi zitabaki kwa mhusika kufanyia kazi alichofundishwa.

"Huwa tunafuatilia baada ya mafunzo je kuna mabiliko yoyote kwa wahusika lakini la kufurahisha wengi wenu mmeonesha kubadilika na kuwa na matokeo yenye tija.

"Fursa ya kubadilika iko ndani yetu, sisi tunaweza kutoa fedha ili mafunzo yanapatikane lakini hatuna uwezo wa kukushika mkono bali hilo litabaki kuwa ni uwezo wa mtu mwenyewe na siku hizi kuna lugha ya kujiongeze.Hivyo baada ya mafanzo hayo naamini mtaendelea kujiongeza kwa kufanya mabadiliko sehemu za kazi,"amesema.

Ameeleza namna ambavyo Unesco ina matumaini makubwa na waliopata mafunzo hayo kwani ikiwangalia inawaona walivyo na ari ya kujituma na kuleta mabadiliko katika majukumu yao baada ya kuipata elimu hiyo.

Amewaambia kuwa wanaofadhili mafunzo hayo wao wanachoangalia baada ya elimu hiyo wahusika wamebadilika kwa kiwango gani na tija gani inayopatikana kupitia wao,hivyo akatumia nafasi hiyo kuwaomba wafanye kazi kwa weledi na ujuzi mkubwa na wasiwaangushe.
Kaimu Mkuu wa Ofisi za Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Faith Shayo akizungumza kuhusu UNESCO inavyoshiriki moja kwa moja kwenye jamii hasa kuzisadia Radio za kijamii ili kufanya kazi zake kifanisi wakati wa kufunga mafuzo ya mafundi mitambo kutoka redio jamii 25 zilizopo Tanzania Bara na Zanzibar yaliyofanyika kwa siku saba katika ukumbi wa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Mafunzo haya ya siku saba yameratibiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO).
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Ufundi kutoka TBC, Joseph Kambanga akizungumza namna TBC ilivyojitolea kuzisaidia Radio za kijamii ili kuimarisha upatikanaji wa habari na hata kuimarisha mitambo ya urushwaji wa matangazo kwenye jamii haraka wakati kufunga mafuzo ya mafundi mitambo kutoka redio jamii 25 zilizopo Tanzania Bara na Zanzibar yaliyofanyika kwa siku saba katika ukumbi wa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa Mafunzo kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Rose Mwalongo akisisitiza umoja wa mafundi mitambo waliopata mafunzo ili kuweza kufikia malengo waliyojiwekea wakati wa kufunga mafunzo hayo.
Fundi Mitambo wa Redio Jamii Orkonerei FM, Baraka David Ole Maika akitoa shukrani kwa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) pamoja na Shirika la utangazaji la Tanzania(TBC) kwa kuweza kutoa mafunzo kwa mafundi mitambo kutoka redio jamii 25 yalifanyika kwa Siku saba katika ukumbi wa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa Mafunzo kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Rose Mwalongo(wa kwanza kushoto) pamoja na walimu waliotoa mada mbalimbali katika mafunzo kwa mafundi mitambo wakiwa kwenye mkutano wa kufunga mafunzo hayo.
Baadhi ya mafundi mitambo wa radio za kijamii 25 wakifuatilia mada wakati wa kufunga mafunzo ya kuwajengea uwezo yaliyofanyika kwa siku saba katika ukumbi wa Uwanja wa Taifa na kuratibiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO).
Kaimu Mkuu wa Ofisi za Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Faith Shayo (kushoto) akiwakabidhi vyeti baadhi ya mafundi mitambo kutoka radio za kijamii 25 za hapa nchini. Katikati ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Ufundi kutoka TBC, Joseph Kambanga.
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Ufundi kutoka TBC, Joseph Kambanga (kushoto) akiwakabidhi vyeti vya kuhitimu kwa baadhi ya mafundi mitambo kutoka radio za kijamii 25 kutoka Tanzania Bara na visiwani.
Kaimu Mkuu wa Ofisi za Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Faith Shayo akiwa kwenye picha ya pamoja na wahitimu ambao ni mafundi mitambo kutoka radio za kijamii 25 mara baada ya kufunga mafunzo hayo yaliyofanyika kwa siku saba.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad