HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 25 April 2018

ELIMU MATUMIZI YA ARDHI INAYOTOLEWA NA PELUM TANZANIA IMESAIDIA PUNGUZA MIGOGORO YA ARDHI

Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii
OFISA Mradi wa mradi wa Ushirika wa wananchi katika kusimamia sekta ya kilimo, Anna Marwa amesema, kupitia elimu ya matumizi ya ardhi inayotolewa na Pelum Tanzania migogoro ya ardhi imepungua kwa asilimia 80.

Aidha amesema, kupungua kwa migogoro hiyo kumetokana na kuongezeka kwa uelewa kwa wananchi na kuwepo kwa mpango wa matumizi ya ardhi ambao umeanisha maeneo na matumizi yake huku mafunzo pia yakisaidia uelewa wa haki ya ardhi kupanda kwa asilimia 30.

Marwa ameyasema hao leo mjini Morogoro kwenye mdahalo wa haki za ardhi wilayani Mvomero ambapo mada kuu ni Usimamizi sahihi wa mpango wa matumizi ya ardhi na uundwaji wa vyombo vya utatuzi wa migogoro ya ardhi vimesaidiaje kupunguza migogoro ya ardhi kijijini.

Amesesema mbali na mafanikio hayo, wamekuwa wakikutana na changamoto mbalimbali, ikiwemo kushindwa kuwafikia wananchi wengi zaidi kuwapimia vipande wa ardhi kwani katika kila kijiji walikuwa wakikaa siku nne tu na idadai ya watu ni wengi  na kushindwa kuwapimia wanakijiji wengi.

Pia uelewa wa haki ya ardhi bado haujafikia watu wengi na kuongeza kwenye mafunzo yao wamegundua suala la arddhi ni mtambuka na linahitaji ushirikishwaji wa Serikali, wadau na mashirika binafsi ili kukabiliana na changamoto za ardhi.

Akitoa maoni yake baada ya kupata mafunzo hayo, Mwenyekiti wa kijiji cha Melela wilayani humo amesema,  migogoro ya ardhi imepungua kwa kiwango kikubwa na kila eneo limetengwa kwa shughuli maalum, watu wametambua maeneeo wanayotakiwa kufanyia shughuli zao.

Pia kama eneo limetengewa kwa ajili ya malisho au kilimo basi yatumike kwa malengo yaliyopangwa na amefafanua mpango wa matumizi ya ardhi kutoka PELUM umerahisisha kazi kwa wanakijiji na viongozi  kwa asilimia 30 kwani hivi sasa watu wanajitambua na wamewarahisishia kazi viongozi wa kijiji.

Naye Ofisa Mtendaji wa Meela Jonathan Mwambo amesema  mafunzo wanayoyapata kutoka Pelum yammesaidia kupunguza migogoro ya ardhi vijijini.

“Mpaka sasa tumeishapunguza migororo ya ardhi zaidi ya 10, kwa kipindi cha miezi sita tu.Tulikuwa na migogoro 21 n sasa imebaki mitatu tu ambayo nayo iko hatua nzuri kuimaliza,"amesema.

 Mjumbe wa Kamati na Mkulima, Abdallah Dihemba amesema, mpango wa Pelum umeondoa mvurugano kwa kutenga maeneo ya kilimo, malisho, makaburi na maeneo mengineyo tofauti na awali ambapo kulikuwa na uholela wa kutumia ardhi bila uhalali na kupelekea ugomvi vurugu na kero na migogoro .
 Mwenyekiti wa kijiji cha Melela, Amin Membe akielezea namna mafunzo ya Pelum juu  mpango wa matumizi ya ardhi katika kijiji hicho yalivyosaidia kupunguza migogoro ya ardhi  na kuwa sasa ardhi inatumika kwa malengo yaliyokusudiwa kwa sehemu husika.
 Afisa mradi wa  mradi wa ushirika wananchi katika kusimamia sekta ya Kilimo, Anna Marwa akielezea wanakijiji wa wilaya ya Mvomero, mafanikio na Changamoto za utekelezaji wa mradi wa mafunzo ya elimu juu ya shughuli za ardhi katika mdahalo wa haki za ardhi wilaya ya Morogoro uliomalizika leo Mjini Morogoro.
 Afisa Mtendaji wa Mela, Jotham Mbwambo akieleza wadau hawapo pichani namna walivyojifunza na kuweza kupunguza migogoro ya ardhi katika kijiji cha Meela na kwani kwa kipindi cha miezi sita kati ya migogoro 21 wamefanikiwa kutatua migogoro kumi na nane na kubakia mitatu tu.
 Mfalme Ole Kerei ambaye ni Mjumbe wa Halmashauri ya kijiji cha Mela  akitoa maoni yake katika mdahalo  wa haki za ardhi wilaya ya Mvomero uliofanyikia Mjini Morogoro.
 Diwani wa kata ya Sungaji katika Halimashauri ya Wilaya ya Mvomero mkoa wa Morogoro, Deogtratious Daniel  ambaye pia ni mgeni rasmi katika mdahalo wa haki za ardhi Wilaya ya Mvomero akizungumza na wadau mbali mbali wa ardhi wakati wa ufunguzi wa mdahalo huo uliofanyika leo Mjini Morogoro.
Daniel amemwakilisha Kaimu Mwenyekiti wa Halimashauri ya Morogoro katika mdahalo huo.
Wadau wa ardhi, wakulima na viongozi wa vijiji mbalimbali walioshiriki mdahalo wa haki za ardhi wilaya ya Mvomero wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa mdahalo huo Mjini Morogoro.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad