HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, April 20, 2018

WANNE WANAODHANIWA KUWA NI MAJAMBAZI WAUWAWA WAKATI WAKIJIBIZANA KWA RISASI NA POLISI MKOANI PWANI

Na Mwamvua Mwinyi, Kisarawe
WATU wanne wanatuhumiwa kuwa majambazi wamefariki dunia baada ya kujibizana risasi na askari polisi ,wakati wakijaribu kufanya tukio la ujambazi katika nyumba ya Juliana Shirinde ambae ni Mhasibu wa kikundi cha vikoba Ushelisheli,wilayani Kisarawe mkoani Pwani.

Aidha jeshi la Polisi mkoani Pwani,limenasa gari ndogo yenye namba za ubalozi ambazo ni namba bandia T 17 CD 220 ambayo ilikuwa inatumiwa na majambazi kufanya uhalifu.

Akitoa taarifa ya tukio hilo la kukamatwa kwa majambazi hao, Kamanda wa Polisi mkoani humo, ( ACP) Jonathan Shanna ,amesema tukio hilo limetokea April 20 mwaka huu saa moja usiku eneo la Kibaoni wilayani hapo.

Amesema majambazi hayo yanasadikiwa yalikuwa matano wakitumia gari hilo, ambapo mmoja wao alishambuliwa kwa risasi lakini alifanikiwa kutoweka .

Kamanda Shanna, alimtaka jambazi alietoweka kujisalimisha ndani ya saa 24 .

Ameeleza zipo tetesi zinazodaiwa baadhi ya waganga wa kienyeji ,ama matabibu ambao huchukua jukumu la kuwatibu majambazi waliojeruhiwa, hivyo ametoa salamu kwao kuwa atakaebainika watamkamata na kumchukulia hatua kali za kisheria .

Pia amesema wakati wa mashambulizi hayo Polisi wamefanikiwa kuwashambulia majambazi wanne na mmoja amekimbia akiwa majeruhiwa.

Amesema mbali ya hayo, walipopekua gari walikuta silaha mbalimbali ikiwemo silaha ya kisasa ya kivita AK 67 inayotumia risasi 30 kwa wakati mmoja,magazine mbili , bunduki mbili na risasi 54 .

Pia wamekamata Pisto mbili bandia ,toy la umbile la kiume,na plate namba mbili zenye namba za usajili halisi , redio call plasta ngumu ya kuziba mdomo,kofia nyeusi ya kuficha macho na pingu .

Kwa upane wa Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama mkoani Pwani ambaye ni Mkuu wa Mkoa huo Mhandisi Evarist Ndikilo amesema mkoa bado upo shwari kwani wapo vizuri kudhibiti uhalifu wowote utakaojitokeza.

"Kauli mbiu yetu ya mkoa ni Utaingia kwa hiari yako lakini hautotoka salama ,kwa kuwa mkoa huu ni wa viwanda na uwekezazji tunahitaji amani na utulivu,"amesema.

Mhandishi Ndikilo amefafanua hakuna nafasi ya kufanya mambo ya ajabu ajabu na atakayethubutu atapata malipo anayoyahitaji.

Mganga mfawidhi wa Hospital ya Wilaya ya Kisarawe ,Dk.Yona Kabata amekiri kupokea miili ya marehemu ya watu wanne kutoka kwa maafisa wa polisi leo saa nne asubuhi.
Kamanda wa polisi Mkoani Pwani, ( ACP )Jonathan Shanna akionyesha silaha na vitu mbalimbali, ikiwemo silaha ya kivita inayokaa na risasi 30 kwa wakati mmoja, ambazo walizikamata katika gari walilolitumia majambazi waliofanya tukio la ujambazi wilayani Kisarawe.
 Kamanda wa polisi Mkoani Pwani,( ACP ) Jonathan Shanna akionyesha gari lililotumika kufanya ujambazi Kisarawe likiwa na namba za bandia za kibalozi huku akiwa ameshika  namba halisi zilizokuwa zimewekwa ndani ya gari hiyo.
 Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama Mkoani Pwani ambaye pia ni mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo akizungumzia  tukio la ujambazi lililotokea Kisarawe na kuwahakikishia wananchi wa Mkoa huo umejipanga kudhibiti wale wasioutakia mema.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad