Na Ripota Wetu, China
BALOZI wa Tanzania nchini China Mbelwa Kairuki amesema zaidi
watu 1,000 wamepata fursa ya kutembelea banda la
Tanzania ambalo lilikuwepo kwenye maonesho ya utalii nchini
humo.
Idadi hiyo ya watu ambao wametembelea banda la Tanzania
imesaidia kuwapatia taarifa sahihi na za kutosha kuhusu utalii
wetu na ni moja ya eneo ambalo limetumika vema kutangaza
vivuto vilivyopo.
Balozi Kairuki ametoa kauli hiyo wakati akizungumza kwenye
maoesho ya utalii yaliyofanyika nchini China ambayo yamemalizika
hivi karibuni.
Akifafanua zaidi kuhusu Maonyesho ya biashara ya Utalii (China
Outboard Travel & Tourism Market COTTM) yaliyomalizika hivi
karibuni jijini Beijing China Balozi Kairuki amesema maonesho
hayo yamekuwa na mwitikio mkubwa.
"Zaidi ya watu 1,000 wameweza kutembelea banda la Tanzania
hatua ambayo imesadia watu wengi kupata taarifa za kutosha
kuhusu fursa za Tanzania.Naipongeza bodi ya utalii na mamlaka
zote za utalii Tanzania pamoja na mawakala wa utalii ambao
walishiriki kwa lengo la kuchangamkia fursa hiyo,"amesema.
Ameogeza soko la China ni jipya na linalokua kwa kasi,hivyo
matarajio yao hizo taasisi za bodi ya utalii, Hifadhi ya Ngorongoro
,TANAPA watapewa nguvu zaidi, watawezeshwa kibajeti ili
wakushiriki maonyesho mengi zaidi hapa China.
"Kwasababu China ni kubwa na inayo zaidi ya majimbo 21na ni
mita za mraba zaidi ya 940,000 ambayo ni kama mara kumi ya
Tanzania kwa hiyo wanahitaji kuja sana hapa China ili kuwafikia
watalii wengi zaidi,"amesema Balozi Kairuki.
Pia amesema "Hakuna kitu cha bure, tunapoona watalii wamekuja
wengi pale nyumbani na wanatumia fedha nyingi na sisi
tunafurahi kwamba sekta ya utalii imeingiza dola bilioni kadhaa,
hizi namba zinatokana na kazi kubwa inayofanywa na wadau wa
utalii (Bodi ya Utalii, TANAPA, hifadhi ya Ngorongoro na
Makampuni mbalimbali).
"Kwa hiyo wanahitaji kuungwa mkono na wadau wote ili wafanye
kazi hii kubwa zaidi ili hatimaye tufikie lengo letu la kufikia mpaka
watalii 100,000 ifikapo mwaka 2020,"amesema Balozi Kairuki
Ameeleza matarajio yaliyopo mwishoni mwa mwaka huu
kutaanzishwa safari za moja kwa moja za ndege kutoka Tanzania
hadi China katika mji wa Guangzhou, hatua itakayochangia
kukuza utalii wa Tanzania na kuwawezesha watanzania na
wachina wengi kutumia ndege hiyo kwenye Shirika letu la ndege la
ATCL kwa ajili ya kuja China kutalii na kufanya biashara.
Wakati huohuo amefafanua kuhusu uwepo wa maoeshomakubwa
Novemba mwaka huu yanayofahamika China International Import
Expo (CIIE)’ kwenye Mji wa Shanghai.
"Tunataka kwenye maonyesho hayo tutangaze mambo matatu ya
Tanzania kwa sababu dunia nzima itakuwa pale, kwa hiyo sisi
tunataka tujikite na vitu vichache cha kwanza ni utalii, pili ni
kuitangaza Tanzanite (Kutangaza madini ya Tanzanite ambayo
yanapatikana Tanzania pekee).
"Wachina wengi hawayafahamu haya madini tunataka
tuyatangaze wachina wayafahamu na jambo la tatu ni bidhaa za
Tanzania na tungependa tupate fursa ya kutangaza kahawa,
Korosho na mnvinyo wa Tanzania pamoja na bidhaa nyingine
kutoka nchini kwetu,"amesema Balozi Kagaruki.
Kwa upande wa Ofisa Habari Utalii kutoka Bodi ya Utalii Tanzania
Irene Mville amesema kupitia maonyesho hayo wameitangaza
vilivyo nchi ya Tanzania kupitia sekta ya utalii na wanayo
mategemeo makubwa ya ongezeko la wageni.
"China wamefanya kitu kizuri lakini kikubwa sana tunaishukuru
Serikali ya Tanzania ambayo imewezesha ushiriki wa mashirika
yake katika maonyesho hayo,"amesema Irene.
)fisa Mipango wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar Hassan Ameir Vuai
ni miongoni mwa washiriki wa maonyesho hayo ambapo amesema
lengo lao ilikuwa ni kutangaza vivutio vya utalii wa nchi ya
Tanzania na walifanikiwa kufikia lengo.
Naye Katibu Mkuu wa Shirikisho la Wanafunzi Watanzania nchini
China Remidius Emmanuel amesema mbali na maonyesho
hayo,Watanzania wanaosoma nje ya nchi, endapo wataendelea
kutumika kikamilifu katika kutangaza utalii na utamaduni wa nchi
yetu.
"Upo uwezekano mkubwa wa kuchochea ongezeko la watalii
hususani katika Taifa hili la China, maana fursa hizi katika vyuo
vyetu hakuna malipo au gharama yoyote , tukiendelea kuzitumia
vema fursa hizi itasaidia zaidi kuunga mkono juhudi za Serikali
yetu.
Tunaishukuru sana Serikali kupitia Ubalozi wa Tanzania nchini
Chin,"amesema.
Balozi wa Tanzania nchini China, Mbelwa Kairuki (Kushoto) akishiriki mahojiano maalumu yaliyolenga kutangaza Vivutio vya Utalii na Utamaduni wa Tanzania kupitia kituo cha runinga cha "Chinese Satelite Travel" chenye watazamaji zaidi ya Milioni 100 ndani na nje ya China. Mahojiano hayo yaliongozwa na Bi. Mei Qing mtangazaji maarufu wa Television hiyo.
Afisa Utalii kutoka Hifadhi ya Ngorongoro, Piter Makutian (Kushoto) akizungumza jambo katika mahojiano maalumu yaliyolenga kutangaza Vivutio vya Utalii na Utamaduni wa Tanzania kupitia kituo cha runinga cha "Chinese Satelite Travel" chenye watazamaji zaidi ya Milioni 100 ndani na nje ya China. Mahojiano hayo yalifanyika wakati wa Maonyesho ya Utalii yaliyofanyika Beijing China mapema wiki hii. Kulia ni Balozi wa Tanzania nchini China, Mbelwa Kairuki.
Mahojiano yakiendelea yaliyolenga kutangaza Vivutio vya Utalii na Utamaduni wa Tanzania kupitia kituo cha runinga cha "Chinese Satelite Travel"
Balozi wa Tanzania nchini China, Mbelwa Kairuki(katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa mahojiano kwenye kituo cha runinga cha "Chinese Satelite Travel"
Balozi wa Tanzania nchini China, Mbelwa Kairuki(kushoto) akipata maelezo kuhusu Maonyesho ya Utalii kutoka kwa Afisa Utalii Mwandamizi - Hifadhi ya Taifa Tarangire Theodora Aloyce (katikati), Wa pili kushoto ni Afisa Utalii habari - Bodi ya Utalii Tanzania, Irene Mville, Afisa Utalii- Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro, Piter Makutian (wa pili kulia) na Afisa Kutoka Ubalozi wa Tanzania nchini China, Lusekelo Gwassa
Afisa Mipango kutoka Kamisheni ya Utalii Zanzibar, Hassan Ameir Vuaiakizungumza juu ya mwenendo wa maonyesho hayo yalivyokwenda hadi kuhitimishwa
Afisa Utalii kutoka Hifadhi ya Ngorongoro, Piter Makutian akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hitimisho la Maonyesho ya Utalii yaliyofanyika Beijing China mapema wiki hii.
Balozi wa Tanzania nchini China, Mbelwa Kairuki akizungumza na waandishi wa habari wakati wa Maonyesho ya Utalii yaliyofanyika Beijing China mapema wiki hii.
Afisa Utalii Habari - Bodi ya Utalii Tanzania, Irene F. Mville akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hitimisho la Maonyesho ya Utalii yaliyofanyika Beijing China mapema wiki hii.
Katibu
Mkuu wa Shirikisho la Wanafunzi Watanzania nchini China, Remidius
Emmanuel(Kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji
wa Kampuni ya Compass Safari, Peter Larocque inayofanya kazi zake nchini
Tanzania.
No comments:
Post a Comment