HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, April 24, 2018

Pelum yafanya mdahalo kwa wakulima, kupunguza migogoro ya ardhi Morogoro vijijini

Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii
IMEELEZWA kuwa watu pekee  wanaoweza kumaliza migogoro ya ardhi nchini ni pande mbili zinazogomnana, na wataalamu wakienda ni kwa ajili tu kuweka mipaka ya kisheria ili mgogoro usijirudie tena.

Mwenyekiti wa Halmashaui ya Wilaya ya Morogoro Kibena Kimu amesema hayo leo wakati wa ufunguzi wa mdahalo wa  haki za ardhi wilayani ya Morogoro uliondaliwa na Shirika la mradi la PELUM Tanzania unaofanyika kwa siku mbili na kushirikisha vijiji vitano vya Mikese Lubungo, Newland na Mfumbwe  vya wilayani humo.

Amesema huwezi kumaliza siku bila kupata taarifa ya mgogoro wa ardhi kutoka kwa wakulima na wafugaji au kijiji na kijiji, kuhusu mipaka kuwa kila mmoja akidai kaingiliwa na mwenzake, mara  huyu kaniingilia na huyu naye akidai kaingiliwa, lakini hata wataalamu wakienda na GPS hawawezi kutatua mgogoro huo.

"Mara  nyingi wataalamu wakifika kila mmoja anaonesha mpaka wake, mwingine anasema mpaka wa kimila ni huu hapa hali inayofanya kutopatikana kwa ufumbuzi.

"Nimekuwa nikiwashauri wakae pande zote mbili zinazogombana na kuwataka wakubaliane kwa pamoja kama eneo linalogombewa ni hatua 10 basi wakubalianae kila mmoja atoe tano na mwingine tano watengeneze hata barabara ili kumaliza tatizo," amesema.

Amefafanua ushauri huo umepokelewa na wengi na wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa.

Amesema, elimu inayotolewa na PELUM kuhusu ya kutambua rasilimali ardhi namna gani ya kumiliki na kufikia mahali kuwa wanatatua migogoro inayojitokeza imesaidia sana wananchi kwani  Vijiji vyote vina mabaraza ya ardhi lakini elimu waliyopata pengine haijatosheleza.
“Nawashukuru sana PELUM kwa kazi wanayofanya na elimu wanayotoa ya kuweza kusimamia matumizi bora ya ardhi kwenye halmashauri yetu ya Morogoro, kwani rasilimali pekee tuliyonayo watanzania ni ardhi kitu ambacho nchi zingine hakipo. 


“Tumeona ujio wa watu wengi wakija kwa ajili ya kuchukua na kumiliki na kuwekeza kwenye miuondombinu ya ardhi yetu,  tusipokuwa na uwezo wa kumiliki ardhi, tunaweza kuja kuwa watumwa kwenye nchi yetu kwani wengi wtu tunaendsha maisha  yetu kwa kilimo na hali ya kawaida.
Aidha Kimu amesema, mpango unaofanywa na PELUM wa kuwapimia vipande vya ardhi wananchi wa kawaida na kuweza kuwatengenezea hati miliki za kimila ni jambo la msingi sana kwa wananchi kwani hati hizo za kimila zitawawezesha  kwenda kukopa kuweza kuenedeleza au kuwekeza kwenye maendeleo yeetu, kutengeneza viwanda vidogo, ukizingatia isis moron i wakulima na wafugaji na hata mazao ya biashara.


“Hati hizi za kimila zitawawezesha kukopa kwenye mabenki na kuwapa uwezo wa kujenga viwanda vidogo na hata pale wanapokuwa na changamoto za mvua na bei ya mazao basi wanaweza kuyafanya kuwa mazao ghafi na kuyatunza katka uborampaka pale yatakaposafirishwa. 


  Mwenyekiti wa Halimashauri ya Wilaya ya Morogoro, Kibena Kimu ambaye ni mgeni rasmi wa kongamano la haki za ardhi wilaya ya Morogoro akizungumza na wadau wa ardhi kuashiria ufunguzi wa kongamano hilo linalofanyika mjini Morogoro humo kwa siku mbili.

Mada kubwa katika kongamano hilo ni usimamizi sahihi wa mpango wa matumizi ya ardhi na uundwaji wa vyombo vya utatuzi wa migogoro ya ardhi jinsi vinavyosaidia kupunguza migogoro hiyo vijijini.
 Meneja Miradi wa PELUM Tanzania, Rehema Fidelisi akizungimza juu kuwapatia hati miliki za kimila wanakijiji kutoka vijiji vya Mikese, Lubungo, Newland na Mfumbwe vilivyopo Wilayani Morogoro.
 Afisa mradi wa  mradi wa ushirika wananchi katika kusimamia sekta ya Kilimo (Sego), Anna Marwa akielezea na kuchambua mafanikio na Changamoto za utekelezaji wa mradi huo, katika mdahalo wa haki za ardhi wilaya ya Morogoro unaofanyika Wilayani humo kwa siku mbili.
Mhadhiri kutoka chuo cha Kilimo Sokoine ambaye ni mshereheshaji  Emmanuel Malisa akizungumza katika Mdahalo wa haki za ardhi wilayani Morogoro.
Afisa Ardhi wa Maliasili Wilaya ya Morogoro, Wahida Beleko, akizungumza katika Mdahalo wa haki za ardhi wilayani humo unaofanyika kwa siku mbili mfululizo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad