HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, April 24, 2018

MZISIMAMIE NGOs ZIFANYE KAZI: MSAJILI NGOs

Na Anthony Ishengoma WAMJW
Msajili wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali NGOs Marcel Katemba amewataka Wasajili Wasaidizi wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini kuzisimamia NGOs ili zifanye kazi kwa kuzingatia Sheria na taratibu za nchi.

Ameyasema hayo jijini Dar es Salaam wakati wa kikao kazi cha Wasajili Wasaidizi ili kutoka mafunzo kwa ajili ya kukumbashana majukumu yao Kama wasajili wasaidizi wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali.

Amesema kuwa kimsingi Mashirika yasiyo ya Kiserikali bado hayatambui umuhimu wenu hivyo tutawakutanisha na Mashirika haya kwa ajili kufahamiana kiutendaji na kutambuana. 

Aidha Katemba amesema Mashirika yasiyo ya Kiserikali wakati mwingine yanakosa majibu muhimu kutoka kwa Wasajili Wasaidizi  hivyo kusababisha waone kuwa Maafisa Maendeleo ya Jamii sio watu sahihi kusimamia shughuli zao.

"Lengo la Mafunzo haya nikukumbashana mambo muhimu ambayo yatawafanya muweze kutoa majibu stahiki kwa Mashirika haya na kuyasimamia ipasavyo baada ya kujua shughuli wanazozifanya"alisisitiza Bw. Katemba.


Naye Mkurugenzi Msaidizi Idara ya NGOs ya Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Bw. Baraka Leornard amewaambia wajumbe wa mafunzo haya kutoka Halmashauri zote kuzisimamia NGOs ili ziweze kuhudumia Wananchi. 

Bwana Baraka ameongeza kuwa kimsingi mafunzo haya ni ya kuwajengea uwezo wasajili wasaidizi wa serikali ili waweze kujua utaratibu wa kusajili na kuyasimamia Mashirika haya kwa matumizi mazuri ya fedha za umma wanazopata kupitia wafadhili wao.

"Pamoja na Masharika yasiyo ya Kiserikali kupata fedha kutoka kwa wafadhili ni muhimu wakatambua fedha hizo ni mali ya umma na ninyi wasajili wasaidizi mnayo haki yakujua matumizi ya fedha hizo".Alisisitiza Bw. Baraka. 

Mafunzo kama haya yamekuwa yanatolewa nchi nzima na Msajili wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali kwa  Wasajili Wasaidizi wa Mashirika haya ambao ni maafisa Maendeleo wa Jamii wa Halmashauri za Wilaya hapa Nchini.
 Mkurugenzi wa Idara ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali na Msajili wa Mashirika hayo Bw. Marcel Katemba akizungumza na Wasajili Wasaidizi wa Mashirka Yasiyo ya Kiserikali kutoka katika Halmashauri na Wilaya za Mkoa wa Dar es Salaam katika kikao baina yake na Wasajili Wasaidizi hao na wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kilicholenga kuboresha namna bora ya uendeshaji wa mashirika hayo mkoani humo.
 Baadhi ya Wasajili Wasaidizi wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Mkoani Dar es Salaam wakifuatilia mada na mafunzo mbalimbali yaliyokuwa yakitolea na Msajili wa Mashirika hayo katika kikao kilichowakutanisha kujadili namna bora ya uendeshaji wa mashirika hayo mkoani humo kilichofanyika katika Ukumbi wa Karimjee.
 Mkurugenzi Msaidizi Usajili wa NGOs Bw. Baraka Leonard na Mkurugenzi Msaidizi Ufuatiliaji Bi. Tausi Malima wakijadiliana jambo wakati wa kikao kazi kati ya Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali na Wasajili wasaidizi wa Mashirika hayo mkoani Dar es Salaam kilichofanyika katika Ukumbi wa Karimjee  kilicholenga kuboresha namna bora ya uendeshaji wa mashirika hayo mkoani humo.
 Mkurugenzi wa Msaidizi Idara ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Bw. Leornald Baraka akiwakumbusha washiriki mambo muhimu yanayohitaji kuzingatiwa kabla na baada ya kusajili Shirika Lisilo la Kiserikali kwa Wasajili wasaidizi wa Mashirika hayo kutoka katika Halmashauri za Mkoa wa Dar es Salaam  katika kikao kilichowakutanisha Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, Wasajili Wasaidizi kilichofanyika katika ukumbi wa Karimjee kilicholenga kuboresha namna bora ya uendeshaji wa mashirika hayo mkoani humo.
 Mkurugenzi Msaidizi Ufuatiliaji NGOs Bi. Tausi Malima akizungumza na Maafisa Maendeleo ya Jamii kutoka Halmashauri za Mkoa wa Dar es Salaam na wasajili wasaidizi wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali mkoani humo kuhusu umuhimu wa ufuatiliaji wa ufanyaji kazi wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali baada ya kupata usajili wake katika kikao kilichowakutanisha Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali na Wasajili Wasaidizi kilichofanyika katika ukumbi wa Karimjee kilicholenga kuboresha namna bora ya uendeshaji wa mashirika hayo mkoani humo.
 Afisa Maendeleo ya Jamii na Msajili Msaidizi wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali katika Manispaa ya Temeke Bw. John Bwana(kushoto)akiomba ufafanuzi zaidi kuhusu masuala yahusuyo Usajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali katika kikao kilichowakutanisha Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali na Wasajili Wasaidizi hao mkoani Dar es Salaam kilichofanyika katika ukumbi wa Karimjee  kilicholenga kuboresha uendeshaji wa mashirika hayo kwa kuzingatia Sheria na miongozo mkoani humo.
Afisa Maendeleo ya Jamii na Msajili Msaidizi wa Mashirka Yasiyo ya Kiserikali Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bi. Given Sure(kulia) akiuliza swali kuhusu masuala yahusuyo Ufuatiliaji wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kwa Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini katika kikao kilichowakutanisha na Msajili wa NGOs na Wasajili Wasaidizi mkoani Dar es Salaam kilicholenga kuboresha uendeshaji wa mashirika hayo kwa kuzingatia Sheria na miongozo mkoani humo. Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad