HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, April 24, 2018

RAIS MAGUFULI AUFAGILIA MFUKO WA PENSHENI WA PSPF KWA UWEKEZAJI WENYE TIJA DODOMA

 Rais wa Jamhuri ya Muunganio wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli mwenye mkasi), akiungana na baadhi ya mawaziri na viongozi wengine kukata utepe ikiwa ni ishara ya uzinduzi rasmi wa jingo la kitegauchumi la Mfuko wa Pensheni wa PSPF, (PSPF DODOMA PLAZA), mjini humo Aprili 23, 2018. Jengo hilo lenye urefu wa ghorofa 12, tayari limepangishwa kwa takriban asilimia 100.
 Rais Magufuli, akimpongeza Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, mara baada ya kufunua kitambaa ikiwa ni ishara ya uzinduzi rasmi wa jingo la kitega uchumi la Mfuko huo mjini Dodoma.


NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, Dodoma


RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, amefurahishwa na uwekezaji uliofanywa na Mfuko wa Pensheni wa PSPF wa kujenga jingo la kitegauchumi mkoani Dodoma.


Kilichomfanya Rais Magufuli kufurahishwa na uwekezaji huo ni kuona jengo hilo lenye ghorofa 12 tayari limepangishwa kwa asilimia 100 hata kabla ya uzinduzi rasmi uliofanyika Aprili 23, 2018.
“Ninyi mmemaliza tu tayari asilimia 100, mliangalia kwamba Dodoma ni makao makuu na mahitaji ya nahitajika kwa ajili ya majengo, hongereni sana kwa kupanga mikakati yenu vizuri kisayansi.” Alisema Dkt. Magufuli na kutoa hakikisho, “Pamoja na kuunganishwa kwa Mifuko hii ya Hifadhi ya Jamii ninyi wafanyakazi wa PSPF mjihesabu kuwa hamtapoteza nafazi zenu, lakini pia jengo hili limeboresha na kupendezesha mandhari ya Dodoma ambako ni makao makuu ya nchi yetu.” Alisema Rais Magufuli wakati akihutubia kwenye uzinduzi wa jengo hilo uliokwenda sambamba na ufunguzi rasmi wa makao makuu ya NMB Bank (Kambarage) ambao ni miongoni mwa wapangaji wakubwa kwenye jingo hilo lililoko barabara ya kuelekea chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).
Rais pia alifurahishwa na ushiriki wa watanzania katika ujenzi wa jengo hilo.
“Nimefurahi kusikia kuwa jingo hili limesanifiwa na ujenzi wake kusanifiwa na watanzania, ma contractors na consultants na kwamba takriban watanzania 250 walipata ajira wakati wa ujenzi.” Alipongeza.
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, alisema, PSPF ndio Mfuko wa kwanza wa Hifadhi ya Jamii kuweka kitegauchumi cha jingo mkoani Dodoma na hivyo kuisaidia serikali ya awamu ya tano katika azma yake ya kuhamia makao makuu ya Nchi, mjini Dodoma.
Aidha Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu,
akielezea historia ya uwekezaji huo alisema, Mfuko ulipewa viwanja vya mradi huu na iliyokuwa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA) mwaka 2012 kwa ajili ya ujenzi wa jengo la kuendeshea shughuli za Mfuko pindi inapotokea dharura (business continuity) pamoja na kibiashara. Kazi ya usanifu na ujenzi wa jengo hili lilianza Julai 2015 na kukamilika Januari 2018 na kwa sasa jengo liko kwenye kipindi cha uangalizi (Defect Liability Period) ambacho kitaisha Januari 2019. Gharama tarajiwa za mradi yaani “contract sum” ni shilingi bilioni 37.02. Mpaka sasa Mfuko umeshalipa kiasi cha Shilingi za Kitanzania bilioni 30.56.
Jengo hili lina minara miwili, mmoja ukiwa na ghorofa 11 na mwingine ukiwa na ghorofa 3. Ukubwa wa jengo ni mita za mraba 15,741.60 pamoja na eneo la maegesho kwa ajili ya magari 161. Matumizi ya jengo ni kwaajili ya ofisi na shughuli za kibiashara.
“Hadi sasa jengo limepata wapangaji ambao kwa uchache ni kama ifuatavyo; NMB Bank, AZANIA Bank, TIB Corporate Bank, Benki ya Kilimo, GIZ, Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), TASAF, TANAPA, TBS, Gaming Board, PPRA, Makao Makuu ya TARURA, Wizara ya Mambo ya Ndani, Sekretarieti ya Maadili ya Watumishi wa Umma, Baraza la Usimamizi wa Mazingira (NEMC), ambao hawa pamoja na wengine wanafanya jengo kuwa limepangishwa kwa asilimia 98. Na kufikia leo Mfuko umeshakusanya kiasi cha Shilingi za Kitanzania 1.06 bilioni kutokana na malipo ya  pango na tunatarajia kukusanya kiasi cha Shilingi bilioni 4.7 kwa mwaka na kufikia miaka minane mradi utakua umerejesha fedha zote zilizowekezwa.”Alibainisha Bw. Mayingu.
 Rais akitoa hotuba yake.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya PSPF, Mhandisi Musa Iyombe, akitoa hotuba yake.
 Bw. Mayingu akitoa hotuba yake.
 Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Dkt. Bernard Kibese, (kulia), akibadilishana mawazo na Mkuu wa Majeshi, Jenerali Venance Mabeyo, (wakwanza kushoto), na Mkuu wa Jeshi la Polisi, (IGP), Simon Siro, wakati wa uzinduzi huo.
 Wakurugenzi wa PSPF
 Mameneja wa PSPF
 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Binilith Mahenge, (kushoto), akipokewa na Afisa Mwandamizi wa Uhusiano wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi wakati akiwasili kwenye eneo la tukio.
 Rais, baadhi ya mawaziri na viongozi wengine, wakiwa katika picha ya pamoja na Bodi ya wadhamini na wafanyakazi wa PSPF.
 Hili ndio jingo la PSPF DODOMA PLAZA lenye ghorofa 12 lililozinduliwa na Rais John Magufuli mjini Dodoma.
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, akitoa hotuba yake.
 Baadhi ya Mawaziri na Naibu Mawaziri, kutoka kushoto, Mhe. Luhaga Mpina (Waziri wa Mifugo na Uvuvi), Mhe.Juliana Shonza, (Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo), Mhe. Profesa Joyce Ndalichako, (Waziri wa Elimu) na Mhe.Jumaa Aweso, (Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji).
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, (kulia), akimpongeza Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, mwishoni mwa hafla hiyo.
Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Ndani wa PSPF, Bi.Costantina Martin, (kushoto), akibadilishana mawazo na Msemaji Mkuu wa Serikali ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari Maelezo, Dkt. Hassan Abass, (katikati) na Afisa Mwandamizi wa Uhusiano wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi.
Kikundi cha Sanaa kikitumbuiza kwenye hafla hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad