HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Friday, 13 April 2018

CHUO CHA UTALII CHAWATUNUKU VYETI MAMA LISHE, MADEREVA TAKSI 50 DAR

Na Karama Kenyunko,Globu ya jamii
CHUO cha  Maliasili na Utalii jijini Dar es Salaam leo  kimewakabidhi vyeti Mama Lishe na madereva taksi 50 baada ya kuhitimu mafunzo ya utalii ikiwa ni muendelezo wa kukuza na kuboresha huduma za utalii nchini.

Akizungumza na wahitimu wa mafunzo hayo yaliyochukua takribani wiki moja katika ukumbi wa chuo hicho Dar es Salaam,  Mkurugenzi wa Jiji  Sporah Liana amesema, mafunzi hayo yatakuwa ni muendelezo wa kukuza shughuli za utalii nchini na kuongeza uelewa wa Mama lishe na madereva taksi ambao mara nyingi wamekuwa wakitoa huduma kwa watalii bila elimu ya kutosha

"Tumegundua shughuli za utalii zinafanyika katika kila kona ya Jiji hili, tumegundua pia watallii wanapenda kula chakula kwa Mama lishe kwani ambao wengi wao hawana mafunzo ya kutosha.

"Tunajua wanaofanya kwenye mahoteli makubwa wengi wao wanasoma katika Chuo hiki tofauti na mama lishe ambao hawana mafunzo yoyote, tumeonelea no vizuri na mama lishe pia tuwalete katika mafunzo  ili waweza kujua namna  ya kutoa huduma kwa watalii wetu" amesema Liana.

Amesema, katika mafunzo hayo, wahitimu hao  ambao kwa kuanzia na mama lishe wamejifunza customer care na namna ya kupika vile vyakula vya kitalii na pia madereva taksi  wamepewa mafunzo hayo kwa kuwa huwa wanatoa huduma za usafili kwa watalii.

Amesema, mafunzo hayo ni awamu ya kwanza na yataendelea hadi wahakikishe wanamaliza mnyororo mzima wa  Utalii ndani ya nchi haswa haswa Jiji zima la Dar es Salaam ambapo ndio linatembelewa kwa wingi na watalii kwa kuwa ni kama mlango haswa wa watalii maana wakiingia wanaingilia jijini na kutokea hapo hapo.

"Pia tutaleta wadau wote wanaouza bidhaa kwa watalii mfano hata wale wanaofanya biashara mkonobi maana wao wanauza bidhaa ambazo hazina lebo ya bei, mtalii akifika anatajiwa bei  mdomoni ambayo wakati mwingine wanahisi kuwa wanadanganywa," amesema Liana.

Kwa upande wa Ofisa Mtendaji Mkuu wa chuo hicho Dk.Shogo Sedoyeka, amesema mafunzo hayo yatawasadia wadau wote  wa sekta ya utalii  kuelewa nini maana ya utalii na maana ya kutoa huduma zenye  viwango ili kuhakikisha mteja anarudi  tena na tena kwenye sehemu hiyo ya biashara na kuhakikisha wanaongeza thamani ya bidhaa zao ili waweze kujiongezea kipatao .

"Tumewafundisha jinsi ya kutoa huduma ya usafiri na chakula na hapo baadae tutaongeza mafunzo mbali mbali yakiwemo ya lugha,"amesema Dk.Shogo.
 Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Sporah Liana akizungumza alipokuwa anafunga mafunzo kwa wajasiriamali ambao ni mama lishe na madereva 50 baada ya kuhitimu mafunzo ya utalii ikiwa ni katika uboreshaji na kukuza huduma za utalii nchini.
Baadhi wahitimu wa mafunzo hayo ya utalii kwa wajasiriamali mama lishe na madereva wa taksi wakisikiliza nasaha za mgeni rasmi 

 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Utalii Dr Shogo Mlozi Sedoyeka akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mafunzo hayo ambayo yatawasaidia wajasiriamali hao katika kutoa huduma zenye viwango na kuongeza thamani ya huduma zao.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad