HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, April 6, 2018

BREAKING NEWS: KAMATI YA RUFAA TFF YARIDHIA WAMBURA KUFUNGIWA MAISHA KUJIHUSISHA NA SOKA

Na Bakari Majeshi, Globu ya jamii
KAMATI ya Rufaa ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) imeridhia uamuzi wa Kamati ya Maadili ya Shirikisho hilo kumfungia maisha, aliyekuwa Makamu wa Rais wa shirikisho hilo Michael Wambura.

Taarifa iliyotolewa muda huu inaeleza Kamati ya Rufaa ya Shirikisho hilo imeridhia na uamuzi wa kufungiwa kwa Wambura.

"Kamati ya Rufaa ya Shirikisho la Kabumbu nchini  (TFF) imeridhia maamuzi ya Kamati ya Maadili ya Shirikisho hilo kumfungia maisha, aliyekuwa Makamu wa Rais(TFF), Michael Richard Wambura"imesema taarifa hiyo ambayo pia imesambaa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii.Hata hivyo taarifa zaidi zitakujia muda wowote kuanzia sasa.

Awali kamati ya maadili ya TFF ilikutana Machi 14 mwaka huu kupitia shauri linalomhusu Wambura aliyekuwa anashtakiwa na Sekretarieti ya TFF kwa makosa matatu ya kimaadili.

Sekretarieti ya TFF iliwasilisha mbele ya Kamati mashtaka matatu (3) ambayo ni kupokea /kuchukua fedha za  TFF za malipo ambayo hayakuwa halali ikiwa ni kinyume na kifungu cha 73(1) cha Kanuni za Maadili za TFF Toleo la 2013.

Pia anatuhumiwa kughushi barua ya kuelekeza alipwe malipo ya kampuni ya JEKC SYSTEMS LIMITED huku akijua malipo hayo si halali ikiwa ni kinyume na kifungu cha 73(7) cha Kanuni za Maadili za TFF Toleo la 2013.

Hivyo kufanya vitendo vinavyoshusha hadhi ya Shirikisho ikiwa ni kinyume na ibara ya 50(1) ya Katiba ya TFF (kama ilivyorekebishwa 2015).

Kutokana na tuhuma hizo Wambura alipelekewa mwito wa kufika mbele ya Kamati Machi 14 mwaka huu ili awasilishe utetezi kuhusu tuhuma zinazomkabili. 

Wambura alipewa hiari ya kutoa utetezi huo kwa mdomo, kutuma kwa maandishi, kuleta mashahidi au kutuma mwakilishi kama kifungu cha 58 cha Kanuni za Maadili za TFF toleo la 2013 kinavyoelekeza. 

Hivyo Wambura alimtuma mwakilishi wake, Wakili Emanuel Muga, aliyefika na kuthibitisha ametumwa na mteja wake (Wambura) kuwasilisha utetezi wake mbele ya Kamati.

Baada ya kuelezwa mashtaka yanayomkabili mteja wake, Wakili Muga aliiomba Kamati kuwa mteja wake anaomba kupewa muda wa kupitia shauri hilo ili aandae utetezi, vielelezo, na mashahidi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad