HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, March 25, 2018

WARAMI WAPINGANA NA WARAKA WA MAASKOFU WA KKKT NCHINI


 Mkurugenzi wa Utafiti   wa Tasisi ya Watetezi wa Rasilimali wasio na Mipaka (WARAMI), Philipo Mwakibinga akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya kukosoa tamko lililotolewa na Maaskofu wa KKKT nchini.
Mkurugenzi wa Utafiti   wa Tasisi ya Watetezi wa Rasilimali wasio na Mipaka (WARAMI), Philipo Mwakibinga akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya kukosoa tamko lililotolewa na Maaskofu wa KKKT nchini katika ukumbi wa Traventine Magomeni.

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
 WATETEZI  wa Rasilimali wasio na Mipaka-WARAMI wameupinga waraka wa Ujumbe wa pasaka kutoka kwa baraza la maaskofu wa kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania (KKKT) uliotolewa jana, kwa madai kuwa ulikuwa wa kisiasa wenye lengo la kukososa utendaji wa serikali na kuleta hofu kwa jamii.

Akizungumza na wanahabari leo jijini Da res Salaam, Mkurugenzi wa Utafiti WARAMI, Philipo Mwakibinga amedai kuwa maskofu kama viongozi wa dini wanatakiwa kujikita katika masuala yanayohusu dini na si siasa.

“WARAMI tunaamini kwamba wajibu wetu ni kuhakikisha jamii inapata haki pasipo upendeleo wowote, kufuatia hili tumeona si sahihi kukaa kimya, tukaona tupaze sauti kuona tunaijenga jamii kulingana na tofauti zao. Kwenye nafsi zao wanavyo vyama vyao mbali na uongozi wa kidini. Hisia za kivyama zisilete mtafaruku kwenye Imani. Wajitafakari kuchagua aina ya maneno wanayotoa kwa jamii ili kulinda na kukuza amani,” amesema na kuongeza.

“Tunashangaa kwa nini waraka huu wa salamu za pasaka haukujikita katika kuwasisitiza waumini wake kujikita katika kuabudu, kumnyenyekea Mungu, kusoma biblia na maandiko mengine ya dini na badala yake wanajikita katika maoni yanayong’ata na kupuliza.”

Mwakibinga amedai kuwa, Miongoni mwa masuala yaliyoandikwa katika waraka huo ni malalamiko kuhusu mchakato wa katiba mpya na uhuru wa kutoa maoni, ambao ulikwamishwa na wansiasa wa upinzani waliosusia kushiriki mchakato huo.  

“Maaskofu wamezungumzia kuhusu utekwaji na mauaji ikiwemo utiaji wa hofu lakini hawajajikita kuelezea kwa kina kisa hasa ni kipi. Sisi tunafahamu kuwa wapo walioathirika moja kwa moja na matukio ya kutekwa na kuteswa kwa baadhi ya vijana ambayo yalipaswa kukemewa tangu siku ya kwanza ya kutokea kwake na si kuyasubiri mpaka leo,” amesema.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad